Ticker

6/recent/ticker-posts

DUDU WASHA-40


.
Ilikuwa ni aibu kwa Secilia pia Didi ambao
walipewa muda wa kuwatosha kujiweka sawa
ambapo walioga vyema na kuvaa mavazi
mengine kisha wakaketi sebuleni kwa ajili ya
kuzungumza na Junior,hofu kubwa ya Secilia ni
kwamba Martin akijua suala hilo itakuwa aibu
kubwa sana na ndoa yake inaweza kuvunjika
,,,kwahiyo shemeji nakusikiliza,japo kidogo tu
nikuonje na mimi,,,aliongea hivyo Junior ambapo
alimkera kweli Secilia aliyekuwa hana namna ya
kufanya
,,,nakuomba kaka umsamehe tu,tufanyie
ubinadamu,,
,,,tena ukae kimya we kijana,Pumbavu,toka hapa
sebuleni,umepewa lifti sasa umepiga Honi mpaka
umechoka,kenge wewe!,,,alifokewa hivyo Didi
ambaye alinyanyuka na kuondoka hapo
Sebuleni,akawaacha Secilia na Junior
,,,haya sasa,niambie lini utakuja kwangu,na
uhakikishe utakaa masaa zaidi ya matatu,,,alisis
itiza hivyo Junior ambapo alimsogelea kwa karibu
kabisa
,,,jamani,Junior hilo suala ni gumu sana na wewe
unajua,,,
,,,ugumu unauleta wewe mama,,!,mbona Didi
umempa,sikiliza,naona nikupangie Ratiba
kabisa,leo alhamisi,Jumapili nakuhitaji majira ya
saa mbili asubuhi mpaka saa sita au saba
kabisa,,,
,,,naomba unisamehe Junior,tusifanye hiko
kitu,naomba unipe njia nyingine nitafanya kwa
hilo ni ngumu kwangu,,,
,,,sawa,hamna shida,ukiweza fanya haya mambo
mawili na nitakuacha huru,moja,,,mwambie kaka
Martin ulichokifanya na Didi pia umwombe
msamaha mbele yangu,mbili,,,niruhusu
nimwonyeshe hizi picha zenu wakati
mnashughulika,haya sasa kazi kwako,usinambie
kama utashindwa au utaweza,ukija Jumapili
nitajua umeshindwa kumwambia kaka na
usipokuja,tena ukichelewa hata dakika moja
tayari nitakuwa nimeshamtumia kaka hizi
picha,,,,alimaliza kuongea hivyo Junior kisha
akaondoka bila kuongeza neno lolote
,,,hivi ndio nitaachika,,?,Martin akisikia haya
itakuwaje jamani,,mungu wangu nisaidie,,,na Didi
sijui ataenda kuishi wapi masikini wa mungu,,,au
nikimbie tu hii nyumba,,Junior,,!,kwanini imekuwa
hivi,,?,nina uhakika ameathirika,sasa kwanini
anafanya hivi jamani,,,au nijiue nikwepe hii
aibu,,?,,,alijiuliza maswali hayo kichwani mwake
ambapo bado alikuwa njia panda asielewe ni
uamuzi upi auchukue kukwepa aibu kubwa kama
hiyo
Moja kati ya vitu ambavyo unatakiwa kuwa
macho sana katika maisha ni NDOA,unatakiwa
kuilinda mchana usiku,ni zawadi ya kipekee kama
heshima ambayo wengine wanaililia kila siku ila
wanaishia kuchezewa na wanaume mwishowe
kuzalishwa na kutelekezwa japo hakuna
anayependa kufanyiwa hayo,pia wapo wanaume
wanaokesha kutafuta wanawake kwa ajili ya
kutulia nao katika maisha na kufunga nao Ndoa
lakini hawapati japo kwa asilimia ndogo
Jambo la kwenda nyumbani kwa Junior na
kufanya naye mapenzi lilimuumiza sana kichwa
Secilia aliyekuwa analia tu,wakati mambo hayo
yanaendelea Martin hakujua chochote,muda
mwingi aliutumia kwa Halima mwanamke
aliyeshika ujauzito wake,Didi alichokuwa
anawaza ni maisha yake jinsi yatakavyokuwa
baada ya Martin kugundua jambo hilo
Tukirudi kwa upande wa Sefu ambaye taarifa
zilienea sana kuwa ameathirika kwani watu
walishaanza kupata nyepesi za mtaani kuwa
Sefu ni mmoja kati ya waliotembea na
Walda,uwoga ulimjaa Sefu ambaye hakuwa na
amani ya moyo hata kidogo,alichokifanya
Sefu,alifungua safari mpaka Hospitarini ambapo
jambo hilo lilikuwa kati yake na Mungu
wake,moja kwa moja alipima damu yake ambapo
alipopewa majibu hakuamini kabisa macho
,,,dokta,embu naomba uniambie kama ninao au
sina,,,aliongea hivyo Sefu huku kijasho
chembamba kikimtoka,alionekana kuchoka bila
hata kufanya kazi ngumu
,,,usijali,punguza Jazba kwanza,jazba yako
haiwezi kubadilisha majibu,hivyo ni vyema
ukatulia mtoto mzuri na kusikiliza majibu yako
sawa eeh?,,aliongea kwa ukarimu Daktari huyo
aliyekuwa mama Fulani wa kikubwa
,,,haya Daktari,,,alijibu Sefu kwa upole
,,,unajua,haijalishi majibu yatakavyokuwa,u
natakiwa kuyapokea kama yalivyo,ukiwa hauna
Ukimiwi haimaanishi wewe ni mzima sana,na
unatakiwa kuzingatia ngono salama,pia usiwe
mtu wa kufanya mapenzi na wanawake tofauti
tofauti,hiyo huatarisha maisha sana hususani
kwenye maambukizi ya magonjwa mbalimbali sio
UKIMWI tu,,,,vile vile ukiwa na UKIMWI sio
mwisho wa maisha kijana wangu,wengi hudhani
hivyo na kukata tamaa mpaka kufikia hatua ya
kujiua au kuchukua uamuzi wa kuueneza kwa
makusudi madai yao hawataki kufa peke
yao,lakini amini nakuambia hiyo ni dhambi kubwa
sana katik aulimwengu huu,,,
,,,ndio nimeshaathirika hivyo jamani,ukiona
Maongezi yanakuwa mengi ujue tayari
hivyo,,,Sefu alianza kulia kabisa huku chozi
likimtoka kwani alikariri kwamba maelezo yakiwa
marefu ujue tayari umeathirika
,,,hapana kijana wangu,nilikuwa nakupa ushauri
tu,tena usilie kwani machozi yako yanaweza
kuwa uchuro kwako,wewe ni mzima kabisa,,,
,,,Dokta unasema,,?,,Sefu hakuamini alivyoambiwa
ni Mzima alirukaruka huku akishangilia chumba
kizima
,,,tulia mwanangu,sasa sio kwamba ni mzima
basi ndio ikawa fungulia nyuki au mbwa,utulie pia
nakushauri baada ya miezi mitatu kupita uje
upime tena,sawa,,?
,,,sawa Daktari wangu,nakupenda sana,,,Sefu
alijikuta akisema hivyo na kuchukua majibu kisha
kuondoka huku akiwa na furaha isiyo na
kifani,huku Nyuma Daktari yule mama wa
kikubwa aliishia kucheka tu alipomsikia Sefu
akimwambia anampenda sana
Ile Sefu kabla hata hajafika mbali kutokea hapo
Hospitari akasikia anaitwa jina lake kwa nyuma
na sauti nyororo ya mrembo,,,,jamani
Sefuuu,,kha,,!,alipogeuza shingo yake alikutana
uso kwa uso na Shani yule anayaishi mitaa ya
kwa Zungu,ndiye yule aliyekutana naye kwenye
basi mpaka wakafikia gesti na kusuguana,,,,Sefu
jamani,mwenzio nilikuwa nimebanwa kweli
nyumbani hivyo leo niko na rafiki zangu
nimewasindikiza Hospitari,naomba utafute mahali
pazuri tutakapotumia hata masaa matatu tu
unitoe hii hamu niliyokuwa nayo,maana zimejaa
haswa,kuhusu gharama nitalipa kikubwa ni wewe
tu mpenzi wangu,,,,aliongea hivyo Shani bila
kumpa nafasi Sefu ya kuzungumza ambapo
alipomaliza kuongea hivyo,marafiki zake
walimvuta mkono na kuondoka naye,,,,tutawas
iliana,,,ilikuwa ni kauli ya Shani aliyompa Sefu
baada ya kuvutwa na rafiki zake,,,,
Itaendelea

#Wanaotaka mwendelez njo inbox kwa maelezo zaidi tunaishia hapa Fb siku njema

        Like share comment
Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();