Ukidhani Kila Mwanamke Aliye Kwa Mume Jibu La Hitaji La Moyo Wake Ni Pesa Basi Utampoteza
Unaweza Ukampa Hizo Pesa Ukaamini Unamjali Lakini Ukitoka Tuu Nyuma Mkeo Yualia
Unapo Rudi Nyumbani Anafuta Machozi Na Anatabasamu Ili Usijue Kuwa Hujatimiza Wajibu Wako Kwa Kumpa Kile Anacho Kipenda Moyoni Mwake
Jali Hisia Zake Uwepo Wake Thamani Yake Na Haki Zake Kwani Ni Wajibu Wako Kwa Mkeo Mpe Mkeo Kile Kitu Roho Yake Inapenda Muhimu Tuu Heshima Ifuate Mkondo Wake Katika Kumpa
Ukimpenda Mkeo Na Kumjali Naye Atakupa Haki Zako Zote Kama Mumewe Atajinyima Mengi Ili Ahakikishe Mda Wote Umeridhika Kwa Kila Jambo Akufanyialo
Atakosa La Kukulipa Kwa Jinsi Unavyo Mjali Bali Atasalia Kujihisi Mwenye Deni Kubwa Mbele Yako Na Hapo Ndipo Itaijua Maana Ya Kutwii Kwa Matendo
Usipomjali Mkeo Basi Jiandae Kutumia Nguvu Nyingi Ili Akupende Na Kukutwii Pole Sana Kakangu Kama Tayari Una Kinywea Kikombe Hicho
Mkeo Kuwa Na Kiburi Si Ajabu Ila Jipeleleze Wewe Mwenyewe Kama Umekosea Wapi...? Hakuna Furaha Na Utiifu Utakao Jengwa Juu Ya Pesa Bali Ni Tamaa Ambayo Itafika Ukomo Wake Bali Mapenzi Ya Kweli Na Kuthamini Ndiko Utakakokupa Utulivu Amani Na Furaha Ya Kupenda Maishani Mwako
Kama unapenda makala hii comment hapo chini sema nimeipenda.
Naomba Sambaza kwa wengine
0 Maoni