Ticker

6/recent/ticker-posts

Zawadi Kwa Wanandoa: KUMCHEZEA MKE- مداعبة الزّوجة

Hakika katika jambo ambalo ni muhimu kwa mume kulichunga na kulilinda ni kumchezea chezea mke wake na haswa kabla ya kumuingilia, hili lina athari kubwa sana kati ya wanandoa wawili katika mahusiano yao ya kiroho na ya kijinsi.

Katika kufikia kilele cha raha ya kiwiliwili kunahitaji kwa mwanamme awe na diplomasia ili aweze kumpa mke wake hamu na matamanio ya kweli, na ushiriki mzuri ulio kamili na mapenzi yaliyokita.

Mke mwenye hekima anaweza kwa diplomasia aliyokuwa nayo na mapambo yake na usafi wa kiwiliwili chake kumvuta mume wake na kumtamanisha. Hivyo basi kumhimiza katika kuwasiliana kwa kiwiliwili vyao kwa urahisi na wepesi zaidi, mahaba siku zote yanatimiza furaha.

Ama kumuingilia mwanamke bila ya kuwepo vitangulizi huwa ni jambo lisilofaa na la kinyama la kutosheleza mahitaji ya mwanamme, kisha haupiti muda mrefu kamaliza haja na kukaa mbali ya mwanamke hali ya kuhema!.

Mwanamke siku zote hupendelea mumewe ashirikiane nae katika hisia zake kwa upole na wema na acheze nae kwa muda unaotosha kupandisha hamu na nyege zake. Na hivi vitangulizi vya jimai husaidia kuwafikisha wanandoa wawili katika utulivu kamili na hivyo kufikia kilele cha raha ya tendo la ndoa.

Kwa hilo na mengineyo Uislamu unahimiza suala hili la kuchezeana na kumchezea mke, amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) :

كلّ شيئ ليس من ذكر الله , لهو ولعب إلاّ أن يكون أربعة: ملاعبة الرّجل امرأته و تأديب الرّجل فرسه ومشي الرّجل بين الغرضين وتعليم الرّجل السّباح

“Kila kitu katika lahau na mchezo si katika dhikri ya Allah ila iwe ni kimoja katika hivi vinne: 1)  Mwanamme kumchezea mke wake. 2)  Mtu kumfundisha farasi wake. 3) Na mtu kutembea katika kamba mbili za juu au milingoti miwili. 4) Na mtu kujifunza kuogelea.” (At-Tirmidhiy)

Na katika kuchezeana suala muhimu ni upole na ulaini na kumsubiri mkeo hadi amalize haja yake kwani wakati mwingine huchelewa, ni bora kwa mwanamme ajipambe na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) :

لا يؤمن أحدكم حتى يحبّ لأخيه ما يحبّ لنفسه

“Hatoamini mmoja wenu hadi ampendelee nduguye lile analolipendelea katika nafsi yake.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

na ukweli ni kwamba hakuna aliyekuwa karibu kufanyiwa hayo isipokuwa ni mke.

Tukiulizana ni vipi mwanamme anafika kilele cha ladha ya jimai? Utaona kwamba ufumbuzi unapatikana katika hali zifuatazo. Kuamini kuwa tendo la Ndoa ni Ibada:

1. Tendo la Ndoa ni Ibada - النّكاح عبادة

Uislamu umenyanyua hadhi ya suala la tendo la ndoa na kulifanya kuwa ni ibada, ibada ambayo wana ndoa wakiifanya hulipwa. Kwani kwa ndoa yao hii ya halali wamejiepusha na maasi na uchafu na wakaishi katika sakafu moja katika mazingira ya kufahamiana, kupendana, kushibana na mahusiano mazuri ya kubadilishana mapenzi yenye kulandana.

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  juu yake amani na salamu anasema:

في بضع أحدكم صدقة

“…na katika kumuingilia mkeo ni sadaka.”(Muslim)

Tendo la ndoa ni sadaka anayotoa mume kwa mkewe, na katika ukamilifu wa neema ni mtu kuhisi kuwa haja zake zinashibishwa na ndipo hapo nafsi inapopata utulivu na malipo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala).

Ibn al-Qayyim (Rahimahu Allaah)  anasema: kila ladha husaidia ladha ya siku ya mwisho, ladha hiyo hupendwa na Inaridhiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na mtendaji hupata ladha katika sura mbili:

Upande wa mwanzo ni kule kustarehe na kujifurahisha na kupata utulivu wa macho.

Upande wa pili ni kule kumridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  na huko ni  kuifikisha nafsi katika daraja la ladha iliyo bora zaidi.

2. Kubusu kabla ya Kuingiliana - القبلة قبل الجماع

'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)  amesema:

“Hakika Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  alikuwa akiwabusu wake zake kisha akitoka kuelekea kuswali na hakuwa akitawadha.”

*ADMIN MAMA HUDHAIFAH.  *

Tendo la kubusu lina athari muhimu sana katika mapenzi na hukurubisha zile hisia za mapenzi na mwisho hupelekea kuridhika.

                Share

Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();