baada ya salam Leo ni vyema tukapata darasa kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu
HIRSUTISM NI NINI?
Ni ugonjwa ambao wanawake hupatwa na mabadiliko ya kuotwa manyoya sehemu ambazo kikawaida wao hua hawaoti manyoya maeneo hayo
mfano ndevu kidevuni, manyoya kifuani, usoni, na mgongoni wakati mwingine manyoya magumu kama ya kiume miguuni na mikononi
Kikawaida wingi wa manyoya mwilini mwa binadamu hutegemea sana vimelea vya ukoo husika, kitaalamu kama genetics make up lakini mwanamke anapokua na manyoya mengi kama ya mwanaume hasa ndevu kuna mambo makuu mawili kwamba anaumwa au ukoo wake uko hivyo japokua waathirika wengi wa shida hii ni wagonjwa
Image result for
Bonyeza hapa Download App ya MAHABA |
HIRSUTISM
DALILI ZA HIRSUTISM
Kawaida gonjwa wa hirsutism huwa na dalili za kua na manyoya mengi kama nilivyotaja hapo juu lakini pia mgonjwa huweza kua na sauti nzito kama kama mwanaume, kuota kipara, kinembe kua kikubwa, chunusi na kupungua ukubwa wa matiti
CHANZO/VISABABISHI VYA TATIZO
Kawaida mwanamke akibaleghe huanza kutengeneza homoni za kiume na za kike ndio maana manyoya huota kwapani na maeneo ya uke hivyo homoni za kiume zikiwa nyingi kitaalamu kama adrogens mwanamke hupata hali hii ya kuota manyoya sehemu ambazo hazihusiki kama nilivyotaja hapo juu
lakini pamoja na hali hii ugonjwa huu una vyanzo vingine kama vifuatavyo.
POLYCYSTIC OVARY SYNDROME: huu ni ugonjwa unaotokana na kutokuwa na uwiano sawa wa homoni za mwanamke kitaalamu kama homornal imbalance hivyo mwanamke hupata mzunguko wa damu ambao sio wa kawaida, kua mgumba, kunenepa na kupata uvimbe kadhaa kwenye ovari za kutengeneza mayai yake.
MATUMIZI YA DAWA NA VIPODOZI VYENYE KEMIKALI
hii huenda ndio ikawa chanzo kikuu cha wanawake wengi kuota ndevu na manyoya kwa tabia ya kutumia dawa fulani bila maelekezo ya daktari pia siku hizi kuna maduka ya urembo yanauza dawa hizi na kuzigeuza dawa za urembo wakati ni hatari sana kiafya kwa watumiaji. kuna dawa kitaalamu zinaitwa steroids huingilia mfumo wa kiungo kinachohusika na utengenezaji wa homoni{ adrenal gland] hivyo zikitumika kwa muda mrefu huleta manyoya ambayo sio ya kawaida kwa wanawake mfano predinisolone vidonge na cream, sonaderm, candiderm,genta
line c, na dawa zingine zote zenye mchanganyiko huu kwani zipo nyingi ila mchanganyiko ni uleule ila majina tofauti ya viwanda. Dawa hizi hutakiwa zitumike kwa angalau wiki moja tu kutibu ugonjwa wa ngozi lakini wengine wamezigeuza kama mafuta ya kujipaka hivyo kama na wewe unapaka hizo aina za dawa ujue ndevu ziko njiani.
Bonyeza hapa Download App ya MAHABA |
UVIMBE WA KANSA
kansa za kiungo hichi kilichopo juu ya figo[adrenal gland] huongeza wingi wa homoni hizi kwenye mfumo wa binadamu na kuleta ndevu na manyoya magumu ya mwili.
CONGENITAL ADRENAL HYPERPLASIA:
huu ni ugonjwa wa adrenal gland ambao mtu huzaliwa nao na kuanza kutoa homoni nyingi za uzazi na matokeo yake mtu huota ndevu na manyoya mengi mwilini..
CUSHING SYNDROME:
hali hii hutokea baada ya mgonjwa kupata matibabu ya dawa zenye homoni ya cortisol mwilini mwake kwa muda mrefu. Mfano matumizi ya dawa ya prednisolone vidonge kwa wagonjwa wa allergy na asthma.
Wakati mwingine ugonjwa huu hutokea bila sababu yeyote hasa kwa jamii za kiarabu na kihindi
VIPIMO:
Mgonjwa anashauriwa kupima kipimo kuangalia wingi wa homoni mwilini wake hasa testosterone kama zitakua zipo juu Au kupiga picha ya ultrasound ya ovary kuangalia kama kuna tatizo lolote au kupima kuangalia uvimbe wa adrenal gland mara nyingi ni moja ya vyanzo vikuu.
MATIBABU
Mara nyingi kutafuta chanzo cha ugonjwa na kutibu ni moja ya matibabu bora zaidi lakini pale ambapo chanzo hakionekani dawa zifuatazo zinaweza kutumika kutatua tatizo hilo
DAWA YA KUPAKA YA EFLORNIRITHINE;
Dawa ya Eflornithine kitaalamu hutumika kupakwa maeneo yalioathirika na nywele nyingi kuzuia kasi ya kukua lakini hazitoi manyoya yaliyopo.
Bonyeza hapa Download App ya MAHABA |
LASERS THERAPY
hii ni miale ya mwanga ambayo inapita ndani ya ngozi kuzuia vyanzo vya ngozi{hair follicles} kuota tena mara nyingi hufanya kazi vizuri lakini gharama yake ni kubwa mno na huenda haipatikani kirahisi.
VEET CREAM :
hii ni cream inayopatikana madukani kwa bei za kawaida ukipaka inanyoa manyoya yote japokua baada ya muda yataota tena lakini inasaidia sana hasa ukipaka mara mara kwa mara au mara moja au mbili kwa wiki.
ELECTROLYSIS:
hii inahusisha kuweka sindano ndogo maalumu kwa kila shimo la unywele na kuharibu chanzo chake ni moja ya matibabu mazuri ila ina maumivu makali sana na dawa za nganzi za kupakwa hutumika kupunguza maumivu hayo.
Bonyeza hapa Download App ya MAHABA |
NOTED; kama wewe ni mwanamke una ndevu au manyoya ambayo sio ya kawaida na huenda mwanzoni hayakuepo angalia kwa makini vipodozi vyako huenda ndio vinasababisha lakini pia nenda hospitali ukachunguzwe wingi wa homoni na upigwe picha ya viungo vya uzazi kama viko salama. ushauri wa bure ni kwamba serikali imekua ikipiga marufuku baadhi ya vipodozi na kuvichoma moto lakini watu wanahisi wanaonewa na kuvitafuta kwa magendo, ukiona kitu kimepigwa marufuku achana
Kama unaswali lolote andika nami ntakujibu araka iwezekanavyo.
0 Maoni