KARIBU mwanandoa mwenzangu katika safu tubadilishane mawazo na kujuzana mambo kadhaa kwa wanandoa au mchumba. Leo tutazungumzia Chanzo au sababu zinazopelekea ndoa za vijana(mume na mke) wengi kutodumu kimapenzi muda mrefu.
Kadri siku hadi siku, wanandoa au vijana
wengi wamekuwa wakioa na kuachana swali je Sababu ni nii? na hali ya kuwa wameridhia kuwa pamoja katika mahusiano yao.
Ndoa za wazee wa zaamani zilidumu sana hadi wakuwa wazee wako pamoja, na wana wajukuu ,vitukuu na wamepitia vipindi vigumu sana katika Ndoa yao.Hizi na baadhi ya Sababu Ndoa za vijana wa sasa kutodumu.
kutojuana kiundani vizuri:
Kutokupata muda wa kuelewana vizuri baadhi ya vijana sasa hukukurupuka kwa kumpenda msichana kukutana naye baa,kituo cha dalaldala kisa mrembo na kupendana , bila kumjua mpenzi wako background yake vizuri tabia, tamaduni na familia yao mmke au mme.Ili kukusaidia kufanya uamuzi wa kuoa au kuoana. Hali hii husababisha vijana ndoa kuvunjika mara baada ya kubaini tabia halisi muda mfupi baada ya kuoa au kuoana mfana mkorofi, mchoyo wali akuonyesha hii tabia na mambo mengine.
Suala la Uvumilivu
Mapenzi yanahitaji wote muwe na uvumilivu mme na mke katika changamoto mnazozipitia kipindi cha ndoa kwa kushirikishana na kushauriana ili kubaini namna ya kutatua, mfano uchumi umeyumba mmoja hapa anakuwa si mvumilivu hutoa lawama tu. Muda mwingine hawasemeshani ndani hata kitu kidogo cha kujadili na kusameheani mmoja hataki.
Kuwa na Tamaa ,uvumilivu:
Kutaka vitu vizuri hali ya kuwa ndani mme au mke mwjiriwa kuna badhi ya mambo nyumbani hayaendi sawa hata akimshirikisha mke hana ushirikianao ,ila ana tabia ya kupenda vitu vizuri ni rahisi kuchepuka nje ya ndoa. Kumpenda mtu kwa sababu ya kitu alichonanacho mtu huchangia sana kuvunjika kwa ndoa.Kwa mfano mwanadada anayempenda mwanaume kwa sababu ya mali alizonazo,siku mwanaume akifilisika ni dhahiri shahiri kuwa ndoa itakuwa mashakani.
Kutokuwajibika na usili.
Katika maisha ya ndoa kila mmoja mme na mke wanapaswa kuwajibika katika utafutaji, mapenzi ya dhati na kusaidia baadhi ya majukumu ili kuwa na furaha.Ikitokea yale mapenzi au upendo kipindi cha uchumba hamna au yamepungua na kila mme akioji ugomvi, husababisha ndoa kuwa hatiani.Hata hivyo usili wa kuficha mambo.
Mapenzi ya ulaghai na usaliti:
Kuwepo na mapenzi ya uongo ndani ya ndoa tabia hii imekuwa fashioni kwa wanandoa wa sasa,Mme kuwa mahusiano ya kimapenzi nje na mwanake mwingine,bila mkewe kujua, hali kadhalika mke naye ana mtu au mtoto, hali ya kuwa ameolewa na amezaandan ya ndoa. Kifupi ni tabia hatarishi sana mume akifahamu huwa ugomvi mkubwa.
kutaka kumbadilisha:
kumbadilisha mpenzi wako kuwa haraka mfano muonekano, marafiki na makundi
yake zamani kumtaka achane nayo. Mme na mke mnapaswa kujadili tabia na kuwa na malengo katika mapenzi au ndoa yenu. Hapa huwa kuna tatizo sana kwani mwanaume atataka afanye anachokitaka yeye na mwanamke afuate anachoambiwa yani aishi kwa kadiri ya atakavyo mwanaume na wakati huohuo mwanamke naye anataka mwanaume aishi kwa kadiri ya yeye anavyotaka.Hali hii husababisha mgongano ndani ya ndoa na mwisho wake huwa ni kuachana.
Misigi ya ndoa na malezi;
Ndoa za leo hii vijana wengi hukurupuka kfanya mamuzi pindi migogoro inapo jitokeza, bila kushirikisha wazee kwa kuomba ushauri au wahenga waliobarik ndoa yao. Katika kesi ya malezi kila mmoja amelelewa kivyake , shida njia ipi sahihi ya kuishi na kumbadili ili mpenzi wangu afanane na mimi mfano ache umalaya, maadili mema na kupenda ndugu zangu na mawasiliano kukatika.
Ushauri Mahusiano ya uchumba yanapokuwa yamechukua muda mfupi chini ya mwaka mmoja ni hatari katika uhai wa ndoa, kwa kuwa na migogoro mngi ambayo huenda kam wangekuwa na muda wa kutosha miaka miwili,kuwa na mawasiliano,Inasaidia kufahamia vizuri mambo mengi hivyo huenda matatizo yasingejitokeza. Tafiti zinaonyesha wachumba wengi sasa huchua muda mfupi
kwenye uchumba.
Like share comment
0 Maoni