Ticker

6/recent/ticker-posts

LEO NAWAKUMBUSHA MAMBO MUHIMU ILI KUILINDA NDOA YAKO NA IWEZE KUDUMU

Hivi unajua kua  kila mwanamke anauwezo wa kuifanya ndoa yake idumu au ianguke, kuimarisha au kuidhoofisha,,,

Jion hii ya leo Tukumbushane kwa haya machache  yanaweza kukusaidia ,kuijenga, Kuongeza mapenzi ktk ndoa yako, na kwa wale watarajiwa wengne wayajue hayo. .....

Kwa Asilimia mia ukimfanyia mumeo hayo kila kukicha mmeo atakusifu na atakutamkia hajajutia kua nawewe kila siku atakumwagia sifa na wengne furaha zao mpaka wanamwaga machozi ,,,Jitahid uwe mke mwema kwa mume wako hili linawezekana bila shaka ukizingatia mafundisho ambayo unaona yapo sahihi uwenda yatakusaidia ktk ndoa yako,,,,,

⏩⏩Kua mwenye KAULI nzuri ya KUBEMBELEZA,,,,mda wote kwa mumeo ,Wewe kama 

mwanamke jaribu,Jitahid ukiwa na mume wako mda wote mlegezee sauti ,maneno matamu mda wote yawe yenye kumtulizisha akili, sio katoka na stress nje  ,Au kazin anarudi nyumban nawewe unamjazia stress kwa kumjazia lawama za apa na pale, km kuna kitu ujapendezwa nacho msubiri atulie atoe machovu ,akishatulia hayo mengne utamweleza badae kwa upole na utaratibu sio kuchonga mdomo uo aifai bibi wee hapo ujengi unabomoa,,,,,

⏩Kua mwenye SUBRA 

Maisha kuna kupata na kukosa ,,mkipata sema Alhamdullilah na mkikosa pia sema Alhamdullilah RIDHIKA na Hali yenu, ,sio leo umeenda kwa shoga ako umekuta kanunuliwa kitu kipya na mumewe naww unarud kwako linakuuma rohoni unaanza kupanic ooh kwanini sijanunuliwa,,ukirud nyumban unaanza kumtupia lawama mumeo fulani kanunuliwa iki mimi mpk leo hujaninunulia,,,,hapo unatoa lawama wakti hali ya mumeo unaijua haiku sawa ,,,,

Jaribu wakti mko wenyewe wawili faragha mnakula rahaaaa za hapa na pale mueleze darling wako kwa sauti ya upole nahtaji unifanyie kitu flani km anaouwezo wakukuletea basi atakuletea, ,na Kama hana atakwambia subiri kidogo kama hakiwezi pia atakwambia hawezi ndio mana ukaambiwa ndoa uvumilivu,,,,, unaona watu wemeishi miaka 50 /70 ktk ndoa sio km awajapitia changamoto hizo bali wamevumiliana mpaka leo wamezeeka pamoja 

Baadh Wanawake wasasa subra,uvumilivu vinawashinda mtu anataka mambo kwa pupa anataka kutimiziwa jambo kwa lazima ajui subiri kwanza,,,,atambui mume wake anapomwambia hana yeye anakuja juu, kama mume wako anakupenda na kukujali pia kwann asikufanyie unachohtaji lakn wakt mwingne hana mfuko hauruhusu lakn mke aliekosa subra anaona atumiziwi ndio mana leo ndoa zimekua fashion mtu anaolewa January anaachwa aprili kwa kukosa subra na uvumilivu hatambui km ni kipindi tu kitapita inshaAllah mambo yatakua sawa utatimiziwa ukitakacho. 

Mwanamke jifunze ,Jitahid uwe MSAFI 

Ndio usafi uwe wenye kumvutia mume mda wote na hata kutamani asitoke nje na hata akitoka basi  akuwaze ,akutamani na kupanga kurudi mapema ili awe naww mda wote, ,Hakikisha mda wote nyumba yako ni safi kuanzia Chumbani mpk nje ya nyumba,Wewe mwenyewe Hakikisha mda wote uko msafi  na, Mpaka mumeo Hakikisha akitoka umtizame kama yuko okey. 

Nguo zake umezinyoosha pasi ,umuweke sawa yaan awe smat ndio atoke,,,sio mume anarudi kazini akukute na Nguo alokuacha nayo asbui mpk jion bado unayo inanuka shombo inahuuu, ,mume akirudi akukute umejipamba umependeza ,unanukia ,,nyumba nayo inanukia na Nguo ya mtego umemvalia 

Muelewa kuna wanaume wengne wanapenda usafi yaan utakuta anakupenda tu asikii aoni kwasababu ya usafi wako,,,sio mwanamke ujipatilizi mpk anaona aibu kuja hata na rafik kwa jins nyumba ilivyo RAFU badilika bibi wee uchafu unaweza kukupelekea ukaiyangusha ndoa yako utakuta wengne mume ndio msafi kuliko mke badilika mtoto wakike.


            Share

Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();