Ukipenda usijiulize kwanini unapenda au unapenda nini kwake.
UKweli wa Mambo Upendo ni Kitu cha Ajabu sana Unaweza kumpenda mtu ukawa kwake husikii, huambiliki, Anaweza kukufanyia Mabaya lakini kwasababu ya Upendo ulonao kwake unaona sawa. Ndio maana ya Msemo MOYO ukipenda MACHO huwa hayaoni._*
Kupenda sio jambo baya kabisa lakini kupenda msichana au mvulana kuliko unavyo jipenda ni hatari sana..Katika maisha lazima ujipende wewe kwanza na ukiamua kuwa na mahusiano penda kiasi ata ukiachwa usiwe na athali mbaya..Mtu anajiua kisa mapenzi kapenda kupita maelezo anaona hawezi kuishi bila Mpenz wake..Kuna wasichana wamediriki Kufanya Zinaa, wengine kitendo cha Qaumu Lut kwa kuogopa akimnyima mpenzi wake ata muacha au hatomuoa, Mwisho wake wana baki na majuto ya milele. Kuna ambao wapo jela kwa sababu ya kupenda sana kuliko wanavyo jipenda wengine wamebaki walemavu wa maisha..Penda lakini usipende kuliko unavyo jipenda._*
Tuwaangalie wanafalsafa Wa masuala mbalimbali Duniani wengine hawakuwahi kuoa wala kuwa Na mahusiano ya kudumu.
Mwisho Wa siku walijitimisha tu kuwa *Kinahitajika kiasi Kwenye kila jambo*!
UKIPENDA PENDA KIASI. NA UKICHUKIA CHUKIA KIASI._*
Too much of everything is harmful*!
Sasa kiasi hicho tunakipimaje?
Utajuaje kupenda kiasi?
Simama Na yeye anaejalia heri Na baraka.
Muombe yeye anayempa amtakae.
Mtegemee yeye mtoaji Na msimamizi Wa mambo yote.
Ni yeye aliye mkuu Na mmoja Wa pekee...
Kwa masuala ya ndoa kama ushauri, Na usuluhushi Wa migogoro.
Toa maoni
Share
0 Maoni