Ticker

6/recent/ticker-posts

DALILI ZINAZOONESHA MDADA HANA MPANGO NA WEWE KAKA YANGU

Wakaka wengi wamekuwa ni watu wa kulazimisha mambo. Au wanatumia Nguvu kubwa sana kuhakikisha Mahusiano au ukaribu na mdada uendelee. Lakini ngoja nikwambie kitu, Mdada akiwa hana mpango na wewe kimahusiano au hata kirafiki huwa kuna dalili ambazo huwa anazionesha.

1. *Nipo Bize*

Mdada kila mara anakwambia kuwa yupo Bize pale ambapo hajibu sms zako, au hakupigii simu. Ukiona hivi jua kuwa Hana mpango na wewe kaka yangu. Kwa maana hakuna mtu aliye bize masaa 24. Kama wewe unaumuhimu wowote katika maisha yake atatenga muda wa kukutafuta tu.

2. *Anatumia majibu ya mkato*

Hii huwa ni dalili kubwa sana kuonesha mdada hana mpango na wewe. Unakuta anatuma sms za neno moja moja na haanzishi mazungumzo. Unakuta wakati mwingine Badala ya kuandika "Poa" anaandika "P" au anajibu kama vile anajibu mtihani. Ukiona hivi unajua hana mpango na wewe na anajisikia uvivu sana kuchati na wewe kwa maana anakuona ni kero sana na msumbufu.

3. *Anachelewa sana kujibu sms yako*

Unaweza mtumia sms saa mbili asubuhi akajibu saa tisa mchana. Na akijibu hatoi sababu yoyote kwanini amechelewa. Jua hapo mdada hana mpango na wewe na wewe yani sio wa muhimu kwake, kuna watu wa muhimu kwake kuliko wewe.  Kama ungekuwa wa muhimu angekuwa anakujibu haraka sana.

4. *Anakutafutia kosa*

Mdada akikuchoka au akiwa hana mpango na wewe tena, atakutafutia kosa ili wewe mkaka ndio uonekane unatatizo.  Atatafuta Chochote tu hata kama kidogo sana ili tu akulaumu na kukufanya ujisikie vibaya.

*NINI CHA KUFANYA?*

1. *Tambua kuwa kila Mdada  unayemuona anamatatizo yake.*

Unaweza sema, "Ah namuacha huyu naenda kwa mwingine", ila ukakuta anatatizo kubwa zaidi kuliko wa kwanza. Ukitambua hilo, utaanza kufikiri ni kwa jinsi gani uishi naye kwa akili.

2. *Mawasiliano hayalazimishwi*

Ukiona mdada anakujibu majibu mafupi, au anachelewa kujibu  au hajibu kabisa sms zako, usilazimishe we acha kumtafuta, akijiskia atakutafuta  wewe.

3. *Jifunze kukaa kimya*

Wadada wengi ni wazuri kukariri unachokisema hasa mkiwa mmegombana atakuja kutumia maneno yako, baadae kukulipizia kisasi, we Jifunze kukaa kimya.

Kama unataka ushauri zaidi Karibu kwa maoni

Karibu sambaza kwa wengine.

Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();