Ticker

6/recent/ticker-posts

MCHUMBA WANGU KANIRUDIA BAADA YA MCHUMBA WAKE KUFARIKI!

Mimi ni kijana wa miaka 28, sijaoa lakini nina mchumba wangu ambaye tulianza mahudiano tangu tukiwa chuoni. Baada ya kumaliza chuo mimi nilipata kazi Mwanza yeye alibaki Dar, alikuja kupata kazi katika Benki moja, tulikua na mipango ya kuoana kwani tulikua tunapendana sana, lakini baada ya kukaa kama miezi sita mbalimbali mwenzangu alianza kubaidlika. Alianza kuacha kupokea simu zangu, hajibu meseji zangu na kila nilipokua nikimuuliza alitoa sababu sababu zisizoeleweka.

Mwanzoni nikiwa Dar nilikua nashukia kwake lakini baadaye alianza kutoa sababu sababu nyingi ili tu nisishukie kwake. Kama mwanaume nilijiongeza na nilipomuuliza kama ana mtu mwingine aliwaka na kusema kama simuamini ni bora tuachane. Kweli nilikubaliana na hali na kuacha naye lakini roho ilikua inaniuma sana kwani ni mtu ambye nilikua na malengo naye na sikujua sbabau.

Nilijitahidi sana kuongea naye na kutaka hata aniambie sababu ili nijirekebishe lakini aligoma na kuniambia upendo umeisha. Niliamua kumpotezea na kumuambia kwaheri, nilikata mawasiliano kabis ana sikutaka tena masuala yake. Lakini baada ya kama mwaka mmoja baadaye alinitafuta, alikuja mpaka Mwanza nilipokua naishi na kuja kuniomba msamaha, aliniambia umbali ulikua ndiyo sababu na alihisi nina mwanamke mwingine.

Aliniambia amejaribu kunisahau ameshindwa na hawezi kuendelea na maisha bila mimi. Kusema kweli bado nilikua nampenda na kwakua nilikua sijaingia kwenye mahusiano mengine niliamua kumsamehe na kusahau. Sikutaka kusubiri tena niliamua kuanza mipango ya harusi, nilienda kwao kujitambulisha, lakini nikiwa kule ndiyo nilisikia maneno maneno. Kumbe kuna mwanaume mwingine alishaenda kumtambulisha na yule mwanaume alikufa kabla hawajaoana.

Niliamua kufuatilia na kugundua ni kweli alikua anatembea na mfanyakazi mwenzake ndiyo sababu akaniacha na walipanga kuoana lakini alifariki kwa ajali ya gari. Roho imeniuma sana kwani nawaza kua kaja tena kwangu kwakua kafiwa na si kwasababu ananipenda. Niliongea naye akaniambia nikweli na kuniomba msamaha ila roho yangu haitaki kwani najiona kama chaguo la pili, niko njia panda nifanyeje, niahirishe kila kitu au niendelee na mipango ya ndoa? Toa Naoni yako sambaza nawengine washauli. 

Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();