Bonyeza hapa Download App ya MAHABA |
Kwa nini baadhi ya wadada wanatafuta limbwata na madawa ya kuushika moyo Wa Mume wako na limbwata unayo wewe mwenyeo?
Limbwata ya kwanza:-
JICHO LAKO
Unapomuangalia mumeo lainisha jicho liwe laini na mkiongea muangalie machoni na pa kurembua urembue
SAUTI YAKO
Ongea na mumeo kwa sauti ya upole ya kubembeleza,sauti nyororo,usiwe mropokaji hakikisha kua unaweka sauti special kwa ajili yake.
MAVAZI YAKO
Unapokua na mumeo faragha Usivae madera na majuba , Vaa mavazi ya kimtego mtego , full kujiachia , Vimini ama jifunge kanga ama mtandio mwepesi au Vaa Nguo za Kulalia ( Night Dress ) - Inatosha sana Kumleta Karibu Kimahaba na akikubeep tu Mpigie.
UBUNIFU WAKO
Ubunifu kwenye mapenzi ni limbwata ya aina yake , Usifanye mazoea kwenye suala hili kila siku buni mbinu mpya, Usione tabu kusoma makala za wanasaikolojia ya mapenzi na Muda Mwingine hata kumuuliza Mwenzako anatakaje .Bonyeza hapa Download App ya MAHABA
USAFI WAKO
Mara zote napenda kusisitiza juu ya hili - Usafi Wa chumba , Nyumba na mwili wako , hakikisha unakua msafi mda wote kwani huwezi kujua mda gani atakuhitaji.
MANUKATO NA MAPAMBO
Unaponukia unamfanya mumeo asogee karibu yako - Jihadhari Usinuke Maana manukato mengine yanakera Usimlazimishe Mwenzako hata kama wewe unayapenda na hakikisha kila kiungo kimevaliwa pambo lake stahiki.
MANENO MATAMU NA BASHASHA
Wadada hakuna mwanaume anaependa gubu - acha tabia ya kununa nuna ovyo na Kuropoka ropoka mambo bila kupima uzito wake , neno NAKUPENDA MUME WANGU litamke kila Mara na mkumbatie bila sababu maalum - Kukumbatiana kunajenga mapenzi , Urafiki na kunaondosha hasira Usizozijuwa Pamoja na tofauti baina yenu .
MAPOKEZI MAZURI NA KUMUAGA VIZURI
Jenga mazoea ya kumuaga kwa kukumbatiana na mabusu na uwe unamsindikiza , kumuombea dua na mpokee kwa bashasha na kumpa pole ya machofu anaporudi kutoka kazini.
KULA NAE NA KOGA NAE
Bonyeza hapa Download App ya MAHABA
Kukoga pamoja ni sunna kubwa sana tusiiwache na pendelea kula pamoja na kulishana kila siku.
Ukaribu wako kwake ndio limbwata itayomfanya akukumbuke popote atapokua ukijumlisha na msg za mapenzi Mara kwa Mara,hakuna mkate mgumu mbele ya supu.
💓 NYONGEZA 💓
Hakikisha TV au Redio yako haijiongelei tu inavyotaka Vingine Vinaongeza Stress Badala ya Kupunguza - Wakati Wewe Unahangaika Kumuweka Sawa Mumeo , Hakikisha Nyumbani Kwako Una nyimbo Mahususi Kwa ajili ya Kumliwaza Mwenza Wako na Video - na Ukigundua hazipendi Usigombane naye Mbembeleze Kiutu Uzima Kwa Kuwa Nazi siku zote huwa haishidi Jiwe.
UKIYAPENDA YAFANYIE KAZI
0 Maoni