Ticker

6/recent/ticker-posts

MBINU ZA KUDUMISHA MAPENZI NA NDOA YAKO IWEZE KUWA NA FURAHA NA AMANI WAKATI WOTE

Bonyeza hapa Download App ya MAHABA

1, Usitangaze udhaifu wa mkeo kwa

familia na marafiki, kila mmoja

anamtunzia mwenziwe hadhi yake.

2, Usiwe na mtizamo mbaya wala

kuzungumza naye kwa hisia kali

huwezi kujua atatafsiri vipi.!

3, Usimlinganishe mkeo na wanawake

wengine, huwezi kujua hao wanawake

wengine wanapitia hali gani kimaisha.

4, Usisahau kwamba ni mkeo

umemuoa, yeye si kijakazi,

muhudumie kama malikia na

atauonyesha ulimwengu kwamba

Mumewe ni mfalme na utamtawala

maishani.


5, Mpe kipaumbele na ni wajibu wako

binafsi kumfanyia jambo na sio watu

wengine.

6, Usimlaumu mbele za watu hata

kama kakosea, mlinde, muhimize,

mrekebishe faraghani, ukifanya hivyo

kamwe hatokusahau.

7, Usimnyime huduma za kitandani

kwa kujifanya mgonjwa/kuchoka ama

kutokuwa na hamu. Kumbuka

Bonyeza hapa Jisajiri utengeneze dollar 10

wanaume wengine wanatafuta nafasi hiyo.

8, Usimlinganishe mkeo na mtalaka

wako ama mkeo aliyefariki maana

wewe ni mume wa pekee kwake.

9, Usimkemee wala kumkosoa mbele

ya watoto, ni malezi mabaya kwa

watoto maana wewe ni Mwalimu wao,

wanakutazama wewe japo unadhani

ni watoto tu!.

10, Mtazame mkeo kama kavaa vizuri

kabla hajatoka maana akipendeza

jisajiri kutengeneza dollar 10

yeye na wewe unaheshimika na

ukipendeza wewe yeye anaheshimika.

11, Usikubali marafiki kuwa karibu na

mkeo, weka mipaka maana hujui nia

zao.

12, Usitoke kuoga na haraka haraka

ukavaa nguo ukatoka pasi yeye

kukukagua, mkeo kazungukwa na

wanaume wanadhifu wanaojali

mazavi na utanashati.

13, Wazazi, ukoo na marafiki sio

waamuzi kwa mambo ya mkeo,

usipoteze muda kutafuta uamuzi wa

mwisho kutoka kwao, ithibiti Ndoa

yako.

14, Mapenzi yako yasiwe kwa sababu

ya mazingira au kihali hata kama

ulimuoa kwa misingi hiyo kwa sasa ni

mkeo mpende bila masharti. Hali

uweza kubadilika na ikiwa ndio msingi

basi ndoa itavunjika.

15, Mkeo anahitaji umakinike kwake

na umsikilize kama mtoto, usiwe mkali

msikilize kwa makini na atakupenda.

16, Usijilinganishe na mkeo, yeye ni

mke kwa hivyo msaidie tu maana

ndoa ni kusaidia.

17, Usimuhukumu mkeo, ni msaidizi

wako na kiumbe dhaifu mchukulie

kwa mtazamo huo na utapata utulivu

wa akili.

18, Mume mzembe hajali. Haogi.

Jiweke nadhifu ukiwa na yeye nukia

vizuri, harufu mbaya inamkirihisha ila

hawezi kukwambia.

19, Usiwe na urafiki na waume walio

na mtazamo mbaya kuhusu Ndoa.

Watakuharibu mawazo.

20, Mkeo ana thamani kubwa sana

ndio maaana ukatoa vitu vya thamani

kumuoa. Penzi lenu lifanye jipya,

uzembe haufai.

21, Kuzaa ni majaaliwa, mpende mkeo

awe na watoto au asiwe nao,

usiwabague watoto kwa jinsia

wafunze dini na watakuwa wacha

Mungu hadi maishani mwao.

22, Hauwi mzee kwa mkeo katika

kumburudisha, usiwe na ugomvi naye

mutakuwa katika kheri. Usiwache

kuwajali watoto wako na mkeo kwa

sababu ya wanawake wengine au

sababu yoyote ile. Wao ni wewe na

wewe ni wao.

23). Mume anayedumu na ibada ana

usalama, omba kila siku, muombee

mkeo na watoto.

TUKIYAFANYA HAYA TUTAKUWA NA

NDOA BORA!!.

Bonyeza hapa Download App ya MAHABA

Asante sana msomaji unae endelea kusoma makala zangu karibu kwa maoni.

Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();