Bonyeza hapa Download App ya MAHABA |
Hii ni kwasababu hujakivaa wewe, mara nyingi ndoa au mahusiano yanapovunjika wanaolaumiwa ni wanawake. Tena hasa kama wakiachana na watu ambao ni ma handsome, wana pesa na usoni wanaonekana ni wastaarabu, mbele ya jamii wale ambao huonekana kama vile wanajali.
Utasikia huyu dada sijui hata anahangaika nini? Yaani kamuacha Kaka wawatu mstaarabu na hela zake kaenda kutafuta yule hohehahe anahangaika na maisha. Hii ni kwasababu mwanaume ni kiatu, huwezi kujua kama kina bana, kama kina mwiba au kama kinaumiza mpaka ukivae wewe.
Wanadamu wanaona yale ambayo yapo dhahiri yale ya mchana nnje ya kuta za nyumba, lakini hawayaoni yale ya usiku. Lakini wanawake ni wasiri sana, wanavaa tabasamu juu ya shati la moto, wanavumilia mengi lakini nao wakichoka basi huamua kuvua viatu.
Bonyeza hapa Download App ya MAHABA
Hivyo kabla ya kumhukumu mtu kwa kuvua kiatu chake ambacho kinaonekana ni kizuri hembu kivae wewe kwanza ndiyo utajua maumivu yake. Ndiyo najua kuna wanawake vichomi lakini matatizo mengi kaika ndoa husababishwa na wanaume ambao wameshindwa kuwa wanaume katika ndoa zao.
0 Maoni