Bila kuwa na amani katika nafsi yako huwezi kufanya kazi kwa bidii, huwezi kusoma vizuri huwezi ‘kuenjoy’ hata kusikia au kula kitu kizuri. Kwanini uwe na mtu ambaye ni chanzo cha wewe kuwa katika hali hii.
Hayo si mapenzi ndugu. Yachunguze vizuri mahusiano uliyopo huenda unatumika tu ndiyo maana thamani yako haionekani. Unamwambia nakupenda anakujibu sawa. Unamletea zawadi hata kusema ahsante hasemi badala yake ndiyo kwanza anaanza kuitoa kasoro tena kwa maneno ya dharau na nyodo. Unamtuma ‘sms’ ndefu yeye anajibu “K”! Maana yake nini?
Bado utasema na wewe upo katika mahusiano ya kimapenzi? Hapana. Labda upo katika mahusino ya kingono tu, mapenzi hayapo hivyo. Anayependwa hayuko kama wewe. Anayejaliwa hafanani na vile unavyofanyiwa. Anayethaminiwa hakaribiani na wewe kwa lolote. Ila anayetumikia katika mapenzi anafanana na wewe kabisa. Huwezi kuwa na furaha katika mapenzi ya namna hiyo. Hayo ni mapenzi jina.
Wakati wenzako wakifaidi upamoja wao, wewe ndiyo kwanza unajutia mapenzi. Kila siku tunakusikia eti mapenzi balaa, mapenzi mateso, mara mapenzi ni utumwa. Wala mapenzi hayako hivyo. Ila kuna watu wako hivyo. Mmoja wapo ni huyo uliyenaye. Anakupa mateso na mabalaa kisha unaamini ipo siku atakupenda kama umpendavyo. Hivi nani kakwambia kuwa wewe ni mtu wa mtumba hivyo hustahili amani na vitu vizuri muda huu?
Katika hali ya utulivu jiulize nini kitatokea baadaye katika mahusiano yako hayo ikiwa kila siku ni majuto na maumivu. Kwanini usitake kujipanga na kuangalia mustakabali mwingine wa maisha yako kimahusiano? Wengi katika hili mnashindwa. Japo mnaona mnateseka katika mahusiano yenu mnajitahidi kadiri muwezavyo kuonesha eti mko katika furaha. Mbali na hilo, mnatumia kila mbinu na jitihada kuhakikisha hamuwapotezi hao wapenzi wenu, ingawa wao wanaonesha dhahiri kutotamani kuendelea kuwa katika mahusiano na nyinyi.
Yote hii ni kutoakana na ile dhana kuwa na nipatampa wapi kama huyu? Cheki alivyokuwa mzuri, angalia mali zake kila mtu anamsifia. Hayo siyo maisha, jiongeze.
kama Umeipenda share na kwa wengine
0 Maoni