Ticker

6/recent/ticker-posts

NINI CHANZO CHA MIGOGORO YA NDOA NYINGI LEO?


Ndoa nyingi sana leo zina migogoro utafiti unaonyesha %90 ya ndoa zote duniani zina migogoro ni %10 tu ndio ziko alama,migogoro ya ndoa haina dini,elimu,cheo,utajili wala umasikini unaweza kukuta mchungaji wa dini mzuri lakini ndoa yake ina mgogoro au unaweza kumkuta raisi wa nchi tajiri mkubwa,msomi mkubwa lakini ndoa yake inamgogoro mpaka imefikia mtu anafikilia uwenda ninge kuwa na pesa,cheo au elimu kubwa uwenda ndoa yangu ingekuwa na amani lakini akipata hivyo anavyo taka ndio matatizo yanazidi badala ya kupungua sasa imebaki swali la kila mtu kujiuliza kuwa nini chanzo cha mgogoro? Nazani hata wewe momaji unajiuliza swali hilo

Ilituweze kupata hilo jibu lazima tuweze kuludi kuagalia mwasisi wa ndoa yeye alivyo anzisha ndoa alikusudia wanandoa waweze kuishi kwa namna gani ili kusiwe na migogoro,

Ukisoma katika biblia

Mwanzo 2:18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Hapa tunaona Mungu ndie mwanzilishi wa ndoa na kwamba si vema mtu aishi pekeyake kwaiyo mtu yoyote lijali anae kwepa kuowa au kuolewa anakiuka mpango wa Mungu unacho takiwa kujua kuwa Mungu alianzisha swala hili akijua zipo faida hebu tuangalie faida chache

Mhubili 4:9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.

10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!

11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?

12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.

Hapo tumeona baazi ya faida za ndoa sasa tuendelee na somo

Mwanzo 2:21 Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,

22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.

23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.

24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

Hapa tumeona mwanamke anatolewa kwa mwanamume na wanaitwa mwili mmoja sasa inakuaje uchukue fimbo uanze kuchapa mwili wako mwenyewe au uanze kutukana mwili wako mwenyewe hapa lazima kuna ababu sasa twende tuangalie sababu hizo

Waefeso 5:22 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.

23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.

24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.

Hapa tunaona jukumu kubwa analo pewa mwanamke ili ndoa yake iwe na upendo na amani sasa inapo fikia mwanamke anakosa utii hii itasababisha migogoro kwenye ndoa la pili hapo tumeona manaume anapewa kuwa kichwa cha mke kwaiyo katika ndoa mwanaume ni kiongozi na mwanamke ni msaidizi sasa wapo baazi ya wanawake leo wanataka kuwa viongozi  wa ndoa zao hapo lazima utatokea mgogoro kwani hapo utakuwa unakiuka utaratibu wa Mungu,

Pia wapo baazi ya wanaume anatumia nafasi hiyo ya uongozi wa ndoa vibaya wamekuwa ni viongozi madikteta hawataki kushauliwa na wake zao hawapendi kukosolewa wala kujishusha na kuomba msamaha pale wanapo kosea wao wamekuwa wakitumia mfumo dume kwa wake zao kumbuka kuwa kiongozi haina maana wewe hukoseagi binadamu yeyote hajakamili yaani ana mapungufu japo mapungufu yanatofautiana kwa iyo katika ndoa unapo kosea unapaswa kukili kosa kujishusha kwa mwenzi wako na kuomba msamaha ili ni kwa mwanaume na manamke pia,wanaume wengi  wanazani kujishusha kwa mke wake nisawa na kujishusha hazi hapana kujishusha kwa mke wako hakukufanyi maumbile yako yabadilike na wewe mke mume anapo jishusha kwako kusikufanye umzalau heshima inapaswa kuwepo,

Pia na ninyi wanawake  mnapaswa kuwashauli waume zenu kwa busara mda mwingine wanakataa ushauri wenu hata kama ni mzuri kwasababu hamuwashauli kwa busara mume wako anapo kosea usimbeze wala kuonyesha zalau hakikisha hata kama unamkosoa tumia busara, jukumu kubwa walilo pewa wanaume kwa wake zao ni

Waefeso 2:25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;

Tumeona jukumu la wanaume kwa wake zao ni kupenda  hapo umeona jukumu la mwanaume kwaiyo mwanaume unapaswa kumpenda mke wako kama yesu anavyo lipenda mpaka akajitoa akafa kwajili ya kanisa pia mwanaume unapaswa kuwa mvumilivu sana kama yesu anavyo tuvumilia sisi wanadamu japo tunamkosea mala kwa mala lakini yuko teyali kutusamehe ata 7 mala 70 na swala la uvumilivu na kusamehe ni jukumu la wote,nazani umeona kuwa kwa sehemu kubwa mwanamke anajukumu kubwa la kufanya ndoa iwe na amani kwasabu wewe unapo mtii mume ndipo mume anakupenda siku baada ya siku

1Petro 3:6 Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.

utafiti nilio ufanya unaonyesha  asilimia kubwa ya migogoro ya ndoa inasababishwa na wanawake sio kwamba wanaume sio chanzo cha migogoro hapana hapa nazungumzia ailimia wanawake wanasababisha migogoro kwa %70 wakati wanaume ni %30 najua wapo wanawake watabeza hili endelea kunifatilia utajua ni kwanini leo usipo nilea nitaandaa somo linalo sema FAHAMU UWEZO WA AJABU ALIOPEWA MWANAMKE  KWAAJILI YA KUMTEKA MWANAUME,

Mwanamke anaouwezo mkubwa alio pewa na Mungu ambao manamke akiutambua na akiutumia hakuna mwanamume anae fulukuta haijalihi ni mkubwa kama goliati atakua mdogo kwako kama pilitoni hebu tuone biblia nayo inaliongelaje swala hili

Mithari 14:1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

Sio kambwa wanaume hawabomoi nyumba zao wanabomoa lakini idadi kubwa wanawake ndio wanaongoza kwa kiasi kikubwa ndiomaana biblia imesema

Nimetangulia  kusema kuwa binadmu wote wanamapungufu na mazaifu lakini wanawake wanamapungufu na mazaifu mengi zaidi ya wanaume ndio maana mwanaume ili uweze kuishi vizuri unapaswa kuwa mvumilivu sana  bila kuwa hivyo utashindwa  na hivyo ndivyo alivyo umbwa  nandio maana eva ndio alikuwa wa kwanza kula tunda kwaiyo wanawake ni wepesi hata kushawishika na wao wanauwezo wa wakumshawishi mwanaume na mwanaume akashawishika kwaiyo mwanaume ni mdhaifu kwa kwanamke  ndio maana nikasema wanawake wanawenza kuleta amani au kuvuluga amani katika ndoa

1petro  3: 7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

Nazani kufikia hapo umejifunza vizuri hili somo ukilifanyia kazi utaokoa ndoa yako lakini ukipuuza utabaki hivyo hivyo na ndoa yako itaendelea kuwa na migogoro mpaka unaingia kabulini au utakuwa unaowa na kuacha tu au unaolewa na kuachika tu kumbuka hakuna mwanamke wa tofauti na uyo ulie nae au mwanaume tofauti na uyo ulie nae utofauti ni kidogo ndio maana matatizo ya manaume anayajua manaume mwenzake pia matatizo ya mwanamke anayajua mwanamke mwenzake kwasababu wanaendana wanatofautiana kidogo tu

Cha msingi katika ndoa mnapaswa kuchukuliana mizigo

Mhubili 9:9 Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana huo ni sehemu yako ya maisha; na katika taabu zako ulizozitaabika chini ya jua.

Kwauwezo wako uwezi kuyafuata hayo muombe Mungu mwasisi wa ndoa atakusaidia kuyafuata na ndoa yako itapona.


                 Share


 

Chapisha Maoni

0 Maoni