Ticker

6/recent/ticker-posts

FAHAMU UWEZO WA AJABU ALIOPEWA MWANAMKE KWAAJILI YA KUMTEKA MWANAUMEBibili inasema *MWANAMKE NI KIUMBE DHAIFU* hapo hapo inasema *TUKAE NAO KWA AKILI.*

●Mwanamke ni mwepesi kushawishika ndio maa SHETANI alipitia kwake kumdanganya ndio maana Biblia ikasema tuishi nao kwa akili  lakini pamoja na uo udhaifu lakini wanauwezo mkubwa wa kushawishi.

Na bado inasema *MWANAMKE NI JESHI KUBWA* swali?
Walijifunza saa ngapi uwanajeshi na ili kudhibitisha kwamba ni mwanajeshi Mungu anamtuma kwa mwanamme amlinde.

Yeremia 31:22 .... *Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani;* *mwanamke atamlinda mwanamume.*

*KUMBUKA HILI MWANAUME MWENZANGU*

●MWANAMKE aliumbwa ukiwa usingizini wewe MWANAUME Mungu alimpatia uwezo mkubwa wa kumkontlo mume kumfanya mume awe na furaha na Amani wakati wote hayo yalifanyika kabla ya wewe kuzinduka.

●MWANAMKE ndiye aliyemwelewa Mungu alipoambiwa ana mimba ya Roho Mtakatifu wewe MWANAUME ulitaka kumkimbia badala ya kukabiliana na changamoto hiyo.

●MWANAMKE ndiye mtu wa kwanza kwenda kuhakikisha kama kweli Yesu amefufuka na kusambaza habari.

●MWANAMKE ndiye anayeongoza kwa ushawishi mkubwa mwanaume huna ujanja mfano.
■Eva kwa Adamu
■Delila kwa Samson
■Ester kwa Ahasuero
■Raheli kwa Labani n.k

> *Usimuudhi mke wako ana uwezo kubwa sana usione kakaa na wewe anakuvumilia pamoja na ukatili wako.*

> *Anaweza akatumia uwezo wake vibaya ndoa inaweza geuka jehanamu au akitumia uwezo wake vizuri ndoa inageuka Paradiso

Wanaume tuwathamini wanawake kwa kuwa nao ni wathamani kubwa mbele za Mungu.

               Share

Chapisha Maoni

0 Maoni