Ticker

6/recent/ticker-posts

*MAHABA*NAMNA YA KUJITUNZA WAKATI WA DAMU YA MWEZI*HOW TO TAKE CARE OF YOURSELF DURING MONTHLY BLOOD (PERIODS)


 Swahili and English 

🔴🔴🔴🔴Damu ya mwezi si ugonjwa wala haifai kuwa sababu ya wanandoa kutengana ila ni muhimu ukajua namna ya kujitunza ili usimghasi mume katika kipindi hiki.

🔴🔴🔴🔴-Kimila ni aibu kwa mumeo kuona damu yako- ila kwa dharura- kwa hivyo jaribu kuwa muangalifu unapokaa, unapolala na unapotumia choo kisafishe ili mume asikumbane na mapande ya damu.


🔴🔴🔴🔴-Vilevile hakikisha unaifunga pad yako kwa karatasi(isiyoonyesha ndani) kabla hujaitia kwenye pipa la taka. Kuna watu huwa na tabia ya kutupa pad iliyotumika ikiwa wazi. Haipendezi.
-Ni aibu kwa mwanamke aliyeolewa kurundika chupi chafu. Fua chupi pindi tu inapochafuka kwa damu.

🔴🔴🔴🔴-Kwenye upande wa kitanda unaolala, tandika leso/khanga nzito chini ya shuka ili damu ikichuruzika isipite kwenye mattress. Vilevile, weka akiba ya upande wa leso/khanga kitandani ili unapochafua shuka kwa bahati mbaya uweze kuifinika bila kulazimika kumuamsha mume kwa ajili ya kutoa shuka.
-Usiache kuoga na mumeo kwa sababu upo mwezini. Tangulia chooni ujisafi sehemu ya siri na kutupa pad kabla mume hajaingia bafu ikisha muoge kama kawaida. Hakikisha unajikamua kidogo ili damu isibaki tupuni na kuchuruzika wakati mnaoga.

🔴🔴🔴🔴-Harufu mbaya ni sababu nyengine inayotenganisha wanandoa wakati wa damu ya mwezi. Hakikisha unaoga angalau mara 2 kwa siku na unabadilisha pad kulingana na wingi wa damu yako. Usishinde na pad moja siku nzima utanuka vumba.

🔴🔴🔴🔴🔴-Unapotamba chukua muda wako kutia kidole kwenye sehemu yako ya siri ili kutoa uchafu na ujikaushe vizuri kabla hujavaa pad kwani majimaji husababisha harufu mbaya
-Mavuzi huleta ugumu katika usafi wa sehemu ya siri. Jinyoe siku kadhaa kabla hujaanza period ili iwe rahisi kujisafi.

🔴🔴🔴🔴🔴-Wakati wa damu ya mwezi ndio unapofaa kunukia vizuri zaidi kuliko nyakati zengine. Tumia manukato. Fukiza chumba, nguo, nywele na sehemu yako ya siri. Paka fitna kwenye mapaja na mitoki. Changanya mafuta ya mwili(lotion) na aloud kwenye mkono kabla hujajipaka mwilini ili harufu isiishe haraka. Vaa kikuba. Tandaza vilua na asumini kitandani.
-Usiache kujiremba na kuvaa viguo vya kumtega mume. Damu ya mwezi isiwe sababu ya wewe kutopendeza.

🔴🔴🔴🔴🔴- Kwa baadhi ya wanawake, damu ya mwezi huja na misukosuko kama maumivu ya tumbo, hasira, ukosefu wa hamu ya kula na kadhalika. Kumbuka wewe ni binadamu na hufai kujitesa. Kama hujihisi vizuri mjulishe mume wako kwa  upole na atakuelewa. Si lazima ujifanyishe kazi nyingi wakati unaumwa.

🔴🔴🔴🔴-Kilichoharamishwa wakati wa damu ya mwezi ni tendo la ndoa peke yake. Mnaweza kuchezeana mili na kufanya romance kama kawaida almurad mume asikuingilie.

English 

🔴🔴🔴🔴Blood bleeding is not a disease nor should it be a reason for couples to separate but it is important that you know how to take care of yourself so that you do not abuse your husband during this period.

🔴🔴🔴🔴-It is a shame for your husband to see your blood - except for emergency- so try to be careful when sitting, sleeping and using the toilet to clean it so that the husband does not come in contact with blood clots.

🔴🔴🔴🔴-Also make sure you wrap your pad with paper (not showing inside) before you put it in the trash can. There are people who tend to throw away a used pad if exposed. It's not fun.

-It is a shame for a married woman to pile up dirty underwear. Wash underwear only when it is contaminated with blood.

🔴🔴🔴🔴-On the side of the bed you are lying on, wrap a heavy handkerchief under the sheets so that the dripping blood does not pass through the mattress. Also, keep the handkerchief on the side of the bed so that when you accidentally stain the sheets you can cover it without having to wake the husband for the sheets.

-Don't stop bathing with your husband because you are on the moon. First go to the toilet to clean the genitals and throw the pad before the husband enters the bathroom after bathing as usual. Make sure you squeeze a little bit so that the blood does not stick to the mucus and drip when you take a shower.

🔴🔴🔴🔴-Bad smell is another factor that separates a couple during the menstrual cycle. Make sure you take a shower at least 2 times a day and change the pad according to your blood pressure. Do not overdo it with one pad all day long you will smell the aroma.

🔴🔴🔴🔴🔴-When you wash take your time to put your finger on your genitals to remove dirt and dry yourself well before putting on the pad as the fluid causes a bad smell

-Dresses make it difficult to clean the genitals. Exfoliate several days before the start of the period to make it easier to clean.

🔴🔴🔴🔴🔴-The time of the moon's blood is when it should smell better than at other times. Use perfume. Burn the room, clothes, hair and your private parts. Put on the thighs and thighs. Mix body lotion (lotion) and aloud on the hand before applying to the body so that the smell does not disappear quickly. Wear a bag. Spread the blankets and acne on the bed.

-Don't stop dressing up and wearing masks. The blood of the moon should not be the cause of your displeasure.

🔴🔴🔴🔴🔴- For some women, menstrual bleeding comes with side effects such as abdominal pain, irritability, loss of appetite and so on. Remember you are human and you should not torture yourself. If you are not feeling well let your husband know gently and he will understand you. You do not have to work hard to get sick.

🔴🔴🔴🔴-What is forbidden during the menstrual cycle is the act of marriage alone. You can flirt and have a romantic relationship with your ex-husband.



            Share


Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();