Ticker

6/recent/ticker-posts

ZIJUE AINA ZA WAKE


 1. MKE MASUMBWI*

 Huyu ni mke anagombana na mumewe kwa makusudi ili tu kumpandisha hasira... huyu yuko tayari kugombana na mumewe, hasa mbele za watu ili* *watu wamuone.* 

2. MKE BOSI*

 *Huyu ni mke ambaye anapata pesa nzuri, iwe kazini au kwenye biashara zake, lakini hamheshimu mumewe na anamdunisha na kumshusha hadhi kwa sababu yuko vizuri kiuchumi kumzidi mumewe.* 

3. MKE POLISI*

 Aina hii ya wanawake ni maarufu sana. Huyu ni mke ambaye humchunguza au kumpeleleza na kumfanyia ujasusi mume wake kila mahala anapokwenda. Mume* *anapokwenda bafuni, yeye huku nyuma ananyatia fasta simu ya mumewe na kuchunguza meseji zake, mume akipiga au kupigiwa simu, yeye anasimama nyuma ya mlango* *kusikiliza maongezi yote... Mume akitoka kwenda kazini au matembezini anahakikisha anamfuatilia, ikibidi kuweka watu wa*kumchunguza* .

4. MKE KAMUSI*

 Huyu huwa hasikilizi ushauri wa mumewe, badala yake anapendelea kumsikiza mama yake, dada yake au rafiki yake... mumewe anapomwambia jambo, haraka sana anaenda kwanza kumuuliza* *mama yake, dada yake au rafiki yake kama mtu anavyokimbilia kwenye kamusi ili kujua iwapo atekeleze aliyoambiwa* *na mumewe au la.* 

5. MKE SHUGHULI*

 *Huyu anapenda kila kiatu na mkoba unaoingia sokoni ili apate kuhudhuria kila  shughuli inayojitokeza hata kama familia  yake haina ubavu wa kiuchumu wa kugharamia mambo hayo, yeye anahudhuria* *kila shughuli, hivyo kumpuuza mume, watoto na nyumba.* 

6. MTOTO WA BABA*

 *Yeye huripoti na kumshitaki mumewe kwa baba yake kila yanapotokea majibizano kidogo na mumewe.* *Matajiri ndio wenye mwenendo huu, hasa* *kama mumewe anafanya kazi kwenye ofisi ya baba* *yake* .

7. MKE JALALA*

 *Unaweza kuhisi kuwa ni jina kali kidogo, lakini wake wa aina hiyo wapo. Hawa ni aina ya wake ambao huziacha nyumba zao zikiwa chafu, na utawaona wanakimbilia kuzisafisha pale mgeni* *anapokaribia kufika nyumbani, mara nyingi mume anapotoka kazini anakuta nyumba iko ovyo-ovyo kabisa.* 

8. MKE MWENYE HOFU YA MUNGU*

 *Huyu ni mbembezi na mwenye mahaba. Hutoa mahitaji ya kihisia na kiroho, muda wake mwingi ni kwa ajili ya familia yake. Huiongoza nyumba yake kiroho, anaishi na mumewe kwa* *adabu na heshima. Ana nidhamu. Anauchunga sana ulimi wake.* 

9. MKE MTANDAO*

 *Huyu muda wote yuko mtandaoni, kwenye instagram, akiposti picha kuonesha maumbile yake, anachati kiasi cha kusahau kufanya mambo* *ya msingi, kwa sababu muda wote anataka kujua kinachotokea  mtandaoni.* 

 *Kwa dada zangu, jitazame uko kundi gani hapo... na kwa kaka zangu, tazama una mke wa aina gani hapo.* 

 JE, WEWE UPO KATIKA KUNDI LIPI? UMEMFANYA MUMEO/Mkeo  AWE MTU WA AINA GANI?* 

 UMEFAIDIKA NINI KUTOKANA NA MABAYA YAKO KAMA MKE?*

♥️♥️Dumisha_Ndoa_Yako♥️♥️

Tao Maoni 

                  Share

Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();