Ni MUUJIZA kumpata Mwanaume anayeweza KUKUPATA NA AKALIJENGA PENZI LENU walio wengi ni kukutafuta na kukusogeza baada ya hapo wewe ndiye unawajibika kulijenga penzi, Wanaume wanaamini kwamba MWANAMKE ndiye mjenzi na wao ni wawindaji na hilo ndilo linawakanganya wana mahusiano wengi, Wanaume hawafikirii kujenga kwa mtazamo wa wewe unavyohitaji,
Ila wao husimamia penzi ambalo tayari MWENZA wake amelijenga, By nature Mwanaume ni Mtu wa kuongozwa juu ya UPENDO na ndo maana tunasema;
▪NYUMA YA MAFANIKIO YA MWANAUME YUPO MWANAMKE MAKINI
Na ukiona Mwanaume ni MPUMBAVU Basi ndani yake Kuna Mwanamke MZEMBE Yaani hajui kumfanya MUME ajitambuwe na kuendana na pendo analoliona kwa mkewe, Hakuna Mwanaume MWELEVU DUNIANI Kwani Mwalimu wa Mwanaume ni MWANAMKE.
Mwanamke usipojua kupigania PENZI lako kamwe hutajua na wala hutakuja kumuona Mwanaume wa kukupa FURAHA kwa sababu wewe huwezi kulijenga penzi lako mwenyewe.
VUTA NIKUVUTE kwenye Mahusiano na NDOA nyingi ni Mwanaume kulilia Mwanamke amuelewe na Mwanamke kulilia Mwanaume amuelewe hapo ndipo shida huja na kuharibu TASWIRA NZURI YA PENZI LA WAWILI HAO
Ni kawaida kwa Mwanaume kununua mboga na kuja nayo nyumbani, Ila Mwanaume kuipika mboga hiyo ni BAHATI
Mwanamke tambuwa wewe ni MAMA na hukomei kuitwa Mama pindi unapozaa mtoto wako bali MWANAUME ALALAYE KIFUANI KWAKO NAE NI MWANAO tena huyo ndiye anayehitaji UANGALIZI WA ZIADA kwa sababu ni mkubwa mwenzio
Sasa wewe jishaue kwamba kama hawezi kuendana na utakavyo bora YAISHE yataisha kweli na kamwe hutakaa umuone wa kukuelewa Kwani wewe mwenyewe hujui KUSIMAMA KAMA MAMA KWA MPENZI/MUMEO
Toa maoni hapo chini
Share
1 Maoni