Baada ya mumeo kutoka kuoga ,kama mwanamke leo famasia yako ya Furaha ya Ndoa tunakuletea mambo matano muhimu ambayo ukimfanyia mwenza wako ni vigumu kuachana nawe.
1⃣ *MFUTE MAJI KWA*
*TAULO SAFI* ◀
Mumeo anapotoka kuoga cha kwanza kumfanyia ni kumfuta maji yote mwilini mwake kwa taulo au kitambaa kisafi huku ukimshika nywele zake katika hali ya tabassamu la usoni mwako, hili linamharibu akili sana mwanaume na kudumu kukuwaza wewe.
2⃣ *MVISHE VAZI ZURI ULILOMUANDALIA* ◀
Baada ya kumfuta maji basi hatua ya pili ni kumvisha nguo nzuri ulizomiandalia ,iwe za kazini au za kulalia, kwa hili wanawake wengi wanafeli ila mjue kuwa mume anavishwa,havai mwenyewe, mchagulie nguo nzuri na umvishe ,atakuganda sana.
3⃣ *MPE MANENO MATAMU YA KUMSIFIA* ◀
Baada ya kumvisha vazi zuri ulilolichagua wewe hatua inayofuata ni kumsifu kwa alivyopendeleza na umaridadi wake, mwanamke usisubiri mumeo asifiwe na wengine nje wewe ndiye mwenyewe wa kumsifu.
4⃣ *KUMTENGEA NA KUMKARIBISHA CHAKULA* ◀
Kilicho bora kwa mwanamke ni kumtengea mumewe chakula ,mwaume haandai mwenyewe chakula anaandaliwa, kuna chakula labda mchana au usiku kabla ya kulala ,na pia kilichobora ni kumpa kifungua kinywa asubuhi kabla ya kwenda kazini mfano chai au maji ya uvuguvugu yaliyochanganywa na ndimu au limao ni mazuri kiafya , baada ya hapa muite kwa jina tamu analolipenda mfano "honey, sweat, nk " ukifanya haya atakuganda.
5⃣ *MUANDAE KWA KINACHOFUATA* ◀
Kama kasharudi kazini basi muandae aidha kupunzika katika nyakati za mchana au muandae kwa tendo la ndoa au kama ni kwenda kazini muandae kwa uzuri aidha maneno au tabassam lako kiasi cha kumfanya kukuwaza wewe siku nzima.
Haya ndio mambo matano niliyokuletea leo kupitia famasia yako ya Furaha ya Ndoa ,siku zote tunasema mwanaume ni mpambanaji kwenye majukumu ya nje ya nyumba yake lakini ndani ya ndoa yake anatakiwa kutulizwa kama mtoto na kupewa mawadda kayaya, ukimfanyia haya mwanaume baada ya kutoka kuoga utauteka moyo wake kwa asilimia 100%, fanya kuanzia leo mpendwaa.
Toa maoni
Share
0 Maoni