Ticker

6/recent/ticker-posts

SIFA ZA MKE MWEMA

Kuwa mke mwema sio kazi rahisi ndiyo maana mume anayebahatika kupata mwanamke wa aina hiyo anapaswa kumpenda na kumuenzi* .

 Yafuatayo ni mambo 10 yanayofanywa na mke mwema:* 

 1. Mke mwema humfanya mumewe kuwa kipaumbele chake nambari moja, badala ya kazi, marafiki, ndugu au watoto.* 

 2. Mke mwema anafurahia kumuona mumewe akipiga hatua ya maendeleo na ustawi. Huyafurahia sana mafanikio ya mumewe kana kwamba ni mafanikio yake mwenyewe.* 

 3. Mke mwema sio msumbufu pindi mumewe anapokosea kwa sababu anajua kwamba usumbufu hauna faida zaidi ya kuharibu mambo.* 

 4. Mke mwema hufurahia muda wa kukaa na mumewe na anahakikisha mara kwa mara anatengeneza muda maridhawa wa kwa ajili ya mumewe.* 

5. Mke mwema huyakubali madhaifu ya mumewe na hamlazimishi kuwa mkamilifu. Kama ambavyo anapenda mumewe awe mtu bora, anaelewa kuwa atateleza na kufanya makosa.* 

 6. Mke mwema anampikia mumewe chakula anachokipenda. Anajua aina ya chakula sahihi kwa ajili ya mumewe. Hapiki tu ili kumjaza tumbo, bali hupika chakula chenye afya na kinachomsaidia kuongeza nguvu na nishati mwilini.* 

 7* *. Mke mwema hutunza siri za mumewe. Mume anapomwambia siri zake, hathubutu kumwambia yeyote, iwe mama yake au hata rafiki yake.* 

 8. Mke mwema ana moto wa mahabba, ni romantic na huyaonesha mahabba yake kwa mumewe. Haachi kumwambia mumewe kila siku:        NAKUPENDA MFALME WANGU.* 

9. Mke mwema haikatii tamaa ndoa yake pindi mambo yanapokwenda mrama. Ana utayari wa kufanya juhudi kuhakikisha ndoa yake inafanikiwa.* 

10. Mke mwema humuombea mema mumewe, pia huridhika na kile anachopewa, kiwe kidogo au kikubwa. Mke mwema hujiepusha kumlinganisha mumewe na wanaume wengine* . Je, wewe ni mke mwema??* 

*Mke mwema nikitulizo cha mume wake.*

Toa maoni hapo chini 


            Share

Reactions

Chapisha Maoni

2 Maoni

Bila jina alisema…
Asante kwa somo nzuri
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();