Bonyeza hapa Download App ya MAHABA |
(If you do not understand Swahili click on the translation section below)
MONALISA SEHEMU YA: 06
Baada ya mlinzi wa pale nyumbani kwao kumfungulia geti Monalisa akapata kuitoa gari yake nje na safari ya kumpeleka hospital mama yake ikaanza huku akiwa yupo pamoja na rafiki yake Suzzy, huku nyuma walimuacha yule mlinzi akiwa na maswali ya kujiuliza lakini hayakuwa na majibu! Monalisa aliweza kuendesha gari mpaka kwenye hospital moja binafsi iliyokuwa palepale maeneo ya mikocheni Monalisa alisimamisha gari na haraka akaomba msaada kwa wauguzi wa hospital hii na moja kwa moja kikasogezwa kitanda maalum cha kubebea wagonjwa kilichokuwa na magurudumu jirani na gari ya Monalisa bila kupoteza muda Bi Sophia akashushwa kwenye gari na kupelekwa mpaka wodini huku nyuma Monalisa na Suzzy wakifuatilia kwa ukaribu, baada ya kufika kwenye korido Daktari akawaomba Monalisa na Suzzy wabaki hapo halafu yeye pamoja na wauguzi wawili wakaingia ndani ndani ya wodi! Huku nyuma Monalisa akiwa amechanganyikiwa na kile kilichotokea akatoa simu yake kwenye mkoba wake na kumpigia baba yake (Mr Brown) na kumueleza yote yaliyokuwa yametokea kule nyumbani kuhusu kuanguka na kupoteza fahamu kwa Bi Sophia lakini akamficha kuhusu sababu iliyopelekea mama yake kupoteza fahamu pamoja na zile picha Monalisa akumwambia baba yake, Mr Brown akasema yupo njiani anakuja hapo kwenye hiyo hospital Mara baada ya kuelekezwa na Monalisa! Kweli bwana Baada ya nusu saa Mr Brown alisimamisha gari yake nje ya hospital hiyo na moja kwa moja akateremka na kuingia mpaka ndani aliweza kuwaona Monalisa na Suzzy wakiwa wamekaa kwenye viti vilivyokuwa kwenye korido ya hospitalini hapa huku wakiwa na huzuni, Baada ya kusalimiana Mr Brown akamuuliza Monalisa: "Enhe niambie nini kimetokea?" Mr Brown aliuliza! Lakini kabla Monalisa ajamjibu baba yake mlango wa kwenye ile wodi ukafunguliwa na daktari akapata kutokea wote kwa pamoja wakamzingira daktari yule na kutaka kujua hali ya mgonjwa wao inaendeleaje, daktari akawatoa hofu na kuwaambia kuwa mgonjwa anaendelea vizuri Kwani alipatwa na mshtuko tu kidogo na kwa sasa fahamu zake tayari zimeshamrudia wote pale wakamshukuru Mungu pia daktari akasema kuwa ameagizwa na mgonjwa amuitie Monalisa na Monalisa akaingia kwenye ile wodi na kuwaacha Mr Brown pamoja na Suzzy wakisubiri pale kwenye korido! Monalisa baada ya kuingia mle wodini aliweza kumkuta mama yake akiwa yupo pale kitandani akampa pole na moja kwa moja Bi Sophia akamwambia Monalisa: "Mwanangu nakuomba sana hizo picha uzitunze mpaka Mimi nikitoka hapa hospital na usimuonyeshe baba yako" Bi Sophia alisema "Sawa mama nimekusikia, lakini naomba uniambie huyo mtu ni nani kwani?" Monalisa alimuuliza mama yake! Bi Sophia akashusha pumzi ndefu halafu akasema: "Mwanangu hiyo ni historia ndefu sana, subiri kwanza tukirudi nyumbani nitakusimulia" Bi Sophia alijibu, basi kwa kuwa hali ya Bi Sophia ilikuwa ni yenye kuridhisha daktari akatoa ruhusa siku hiyo hiyo na wote wakapata kurudi nyumbani! Kwa vile usiku tayari ulikuwa umeshaingia Monalisa na Suzzy wakaamua kulala kulekule mikocheni nyumbani kwa Mr Brown ili kuangalia na hali ya Bi Sophia itakavyokuwa!
Asubuhi ya siku ya Pili hatimaye ikawa imewadia Bi Sophia sasa hali yake ikawa imetengemaa kabisa na akawaruhusu Monalisa na Suzzy waende kwenye biashara yao lakini akamwambia Monalisa kuwa jioni aweze kurudi tena ili aje amsimulie historia ya yule MTU fukara na pia amwambie ni nani kwake, basi Monalisa alifurahi kusikia hivyo na kuona sasa karibu anaweza kuujua ukweli wa yule MTU fukara ambaye amekuwa akimfuatilia kwa muda sasa! Monalisa na Suzzy wakaingia kwenye gari na kuelekea mlimani city kwenye biashara yao na Mr Brown na yeye naye akaenda ofisini kwake nyumbani akabaki bi Sophia akiwa na mawazo kuhusu zile picha na kumuwazia yule MTU fukara aliyemtambua kwa jina la Mussa kama palivyoandikwa kwa nyuma kwenye mojawapo ya zile picha! Upande wa Pili Monalisa na Suzzy waliweza kufika salama kwenye biashara yao na jioni ilipofika wakafunga biashara yao na na sasa wakawa wanajiandaa kuingia kwenye gari ili waende tena mikocheni wakamuone Bi Sophia ambaye aliwaambia kuwa jioni warudi ili awaambie ukweli kuhusu Yule MTU fukara, lakini kabla Monalisa na Suzzy awajaingia kwenye gari Mara ghafla wakaweza kumuona tena yule MTU fukara akiwa yupo maeneo ya pale huku na yeye pia akiwa amewaona wakina Monalisa! Monalisa akamfuata yule MTU fukara pale kwenye ile sehemu aliyosimama huku yule MTU akiwa amevaa Yale mavazi yake duni yaliyokuwa machafu na yamechanika, Monalisa akamfikia yule MTU fukara!!,, ITAENDELEA SEHEMU YA 07 ENDELEA
MONALISA
SEHEMU YA: 07
Monalisa sasa akiwa yupo na rafiki yake Suzzy wakati wakijiandaa kwenda kuingia kwenye gari ndipo wakamuona tena yule mtu fukara yupo maeneo Yale. Ndipo Monalisa alipoamua kumfuata mtu yule na baada ya kumfikia ilikuwa hivi: "Habari yako, naona Leo tumeonana tena! ..." Monalisa alisema. Yule mtu fukara akalazamisha tabasamu usoni kwake halafu akasema: "Habari yangu ni nzuri, ndio ni kweli tumeonana tena vipi ile bahasha ulimkabidhi mama yako? .." Monalisa akafikiria kwa muda halafu akamjibu yule mtu: "Ndiyo nilimkabidhi, lakini bado mpaka sasa ajaniambia wewe ni nani! .." Yule mtu kwanza akacheka halafu akamwambia Monalisa: "Kama umemkabidhi ile bahasha, basi utakuwa umefanya vizuri sana binti usihofu kabisa mama yako atakuambia kuhusu Mimi ..." Yule mtu alisema. "Hapana lakini pia ingekuwa ni vizuri kama na wewe ungeniambia nikakujua ..." Monalisa alimwambia yule mtu kwa sauti ya kubembeleza. "Sikiliza binti Mimi jukumu langu lilikuwa ni kukupa ile bahasha ukampe mama yako, hayo ya kutaka kunijua Mimi ni nani utaambiwa na mama yako! ..." alisema yule mtu kwa msisitizo. Monalisa akaanza kulia na kupiga magoti kwa Yule mtu kisha akamshika suruali yake iliyokuwa chafu kupindukia na kusema: "Tafadhali naomba uniambie ukweli wewe ni nani ni muda sasa unanifuatilia, nna hamu ya kukujua nipo chini ya miguu yako niambie .." Monalisa alisema huku akiwa bado amepiga magoti pale chini na kulia machozi! "Binti hebu naomba unielewe, maelezo ya wewe kunijua Mimi anayo mama yako! ..." alisema yule mtu fukara akimwambia Monalisa. Mara ghafla kundi la watu waliokuwa pale maeneo ya mlimani city wakapata kushangaa kile kitendo cha Monalisa kumpigia magoti yule mtu ambaye kwa muonekano hakuwa na utofauti na mwendawazimu. Watu wakapata kuwazunguka na kushangaa kioja kile. Iweje binti mrembo kama Monalisa ampigie magoti mtu yule tena huku akiwa analia! Yule mtu baada ya kuona Raia wamejaa pale wanashangaa akamuinua kwa upole Monalisa pale chini alipopiga magoti na kumwambia: "Sasa nisikilize binti, kama mama yako atashindwa kukuambia basi njoo manzese midizini kwenye mabanda ya mama lishe Mimi nitakuwa kwenye banda la mwisho kabisa ..." alisema mtu yule na kisha kwa haraka sana akapata kuondoka maeneo Yale huku akiwaacha watu wakiwa na maswali ya kujiuliza juu yake na pia wakimshangaa. Mwanaume ndio huyoo anatokomea zake! Sasa wale Raia wakamzunguka Monalisa na kutaka kujiua ni kipi kisa na mkasa. "Fanyeni yenu, haya hayawahusu! .." Monalisa ndivyo alivyowajibu watu wale na halafu akaingia kwenye yake ambapo ndani kulikuwa na Suzzy akaiwasha na kuondoka kwa kasi sana maeneo Yale na kuwaacha Raia wakiwa bado wamepigwa na butwaa!!
Baada ya kutoka kule mlimani city Monalisa na rafiki yake Suzzy safari yao ikawafikisha moja kwa moja mpaka mikocheni kwenda kumuona Bi Sophia ambaye ndie mama yake na Monalisa. Kwa upande wa Monalisa sasa akawa na shauku kubwa ya kutaka kumjua yule mtu fukara ni nani kwake na kwanini alikuwa anamfuatilia vile. Ndani ya mawazo yake Monalisa alihisi kuna kitu kipo nyuma ya pazia ambacho yeye bado ajakijua na sasa ndio alikuwa anataka kukijua hicho kitu. Bahati nzuri walimkuta Bi Sophia yupo vizuri kabisa kwani afya yake kwa sasa ilikuwa imetengemaa kabisa Mara baada ya pale mwanzo kuanguka na kupoteza fahamu kwa mshtuko wa kuziona zile picha alizopewa na Monalisa kutoka kwa yule mtu fukara. Bi Sophia aliwakaribisha Monalisa na Suzzy na bila kupoteza muda Monalisa akamkumbushia mama yake kuhusu ile ahadi aliuoahidi kuwa atamuambia ukweli wote kuhusu yule mtu. "Mwanangu sijui kwanza hata nianzie wapi kukueleza, vipi ujakutana naye tena huyo mtu? ..." Bi Sophia alimuuliza Monalisa. Kwanza Monalisa akajifikiria halafu akamwambia mama yake kuwa ni kweli amekutana na yule mtu tena jioni ya siku hiyo hiyo na amemuelekeza mpaka sehemu anapopatikana! Bi Sophia kwanza akashusha pumzi kwa kusikia hivyo halafu akamwambia Monalisa: "Basi kama umekutana naye, na amekuambia mpaka sehemu alipo sasa naomba twende wote nikakuambie ukweli mbele yake! ..." alisema Bi Sophia na kuwaacha Monalisa na Suzzy wakiwa wameduwaa. "Monalisa wewe si unataka kumjua huyo mtu ni nani kwako basi nipeleke nikakuambie .." Monalisa akamuuliza mama yake: "Vipi Sasa kuhusu baba akirudi? ..." Bi Sophia kwanza akacheka halafu akamjibu: "Hiyo niachie Mimi nitajua nimjibu nini! ..." Basi baada ya hapo wakaingia kwenye gari na safari ya kuelekea manzese midizini kwenye hayo mabanda ya mama lishe ikaanza kwenda kumuona yule mtu fukara kama alivyomuelekeza Monalisa pale mwanzoni. Kutoka mikocheni mpaka manzese midizini walichukua mwendo wa nusu saa tu mpaka kufika kule Monalisa akasimamisha gari mpaka kwenye mabanda na wote kwa pamoja wakapata kujionea mabanda hayo ya mama lishe yaliyokuwa yamepangana kwa mstari. Ikabidi wateremke kwenye gari na moja kwa moja Monalisa akawaongoza kuelekea kwenye banda hilo la mwisho kabisa pia waliweza kuwaona mabinti wadogo waliokuwa wakijiuza miili yao pamoja na vijana nao waliokuwa wanavuta Bange na madawa ya kulevya ilikuwa inahitaji moyo kwa mtu mstarabu kuwa hapa! Kwa mwendo wa hofu na wasiwasi hatimaye wakalifikia hilo banda lilikuwa lipo mwishoni na baada ya kuingia ndani ya banda hilo wakafanikiwa kumkuta yule mtu fukara akiwa amejilaza kwenye mabenchi bandani hapo!!,, ITAENDELEA
MONALISA
SEHEMU YA: 08
Monalisa akiwa na mama yake 7b na rafiki yake Suzzy sasa wamefanikiwa kufika Hapa manzese midizini baada ya Monalisa kuelekezwa na yule mtu fukara kuwa ndio sehemu anapopatikana na sasa wameingia ndani ya hilo banda la mama lishe analojihifadhi mtu huyo lililokuwa lipo mwishoni kabisa kati ya mabanda mengi yaliyokuwa hapa. Walifanikiwa kumkuta yule mtu akiwa amejilaza kwenye mabenchi yalikuwemo ndani ya banda hilo! Yule mtu akapata kushtuka baada ya kuona ameingiliwa na ugeni kwenye makazi yake anayojisitiri. "Samahani kwa kuja bila taharifa! .." Monalisa alimwambia mtu yule. Kwanza mtu yule akawaangalia wote kwa zamu licha ya Giza totoro lililokuwa ndani yake bandani hapo aliweza kuwaona vizuri na zaidi alishtuka alipomuona Bi Sophia (Mama yake Monalisa) kuwa naye amekuja hapa. Akamkazia macho! "Wewe mwanamke umefuata nini hapa? ..." Mtu yule alimuuliza Bi Sophia kwa ukali. "Nisamehe sana mume wangu, najua nimekukosea sana naomba msamaha! ..." alisema Bi Sophia huku akianza kulia. Monalisa na Suzzy walipigwa na butwaa Mara baada kumsikia Bi Sophia akimwita mtu yule kuwa ni mume wake walibaki na maswali ya kujiuliza vichwani mwao! Yule mtu sasa akamgeukia Monalisa. "Nilipokuambia kuwa kama mama yako atashindwa kukuambia ukweli kuhusu mimi, sijamaanisha ndio uje naye hapa! .." yule mtu fukara alimwambia Monalisa kwa hasira. "Lakini mimi sina makosa, ni yeye ndie ametaka kuja huku na ameniambia kuwa atasema ukweli huo kuhusu wewe mbele yako ..." Monalisa alijitetea. "Sasa nasema hivi, sitaki kuwaona tena hapa ondokeni haraka sana! ..." alisema mtu yule huku akionyesha kuwa amechukizwa na Bi Sophia kuja hapa! "Sasa kama tukiondoka huo ukweli Mimi nitaujua vipi? .." Monalisa alimuuliza yule mtu. Kwa wakati huu Bi Sophia alikuwa akilia kwa sauti ya kwikwi! "Hiyo utaenda kujua huko mbele ya safari wewe pamoja na mama yako! .." Bado mtu yule aliendelea kuonyesha hasira yake. "Lakini Mussa mume wangu, hebu punguza jazba basi hata kidogo mtoto anataka kukujua .." Bi Sophia alisema huku akifuta machozi! "Mama hebu niambie sasa huyu mtu ni nani? ..” Monalisa alimuuliza mama yake. Bila kukupesa macho na bila kumung'unya maneno Bi Sophia akamjibu Monalisa: " Huyo unaemuona hapo ndio baba yako mzazi kabisa! .." Monalisa na Suzzy walibaki wanaangaliana kwa mshangao! "Eti mama unasemaje? ." Monalisa alimuuliza tena mama yake akiwa kama vile aamini kile alichokisikia. "Nimesema hivi huyo ndio baba yako mzazi .." Bi Sophia alimjibu Monalisa kwa msisitizo! Monalisa huku machozi yakimtoka akamgeukia yule mtu fukara na kumuuliza: "Eti ni kweli wewe ni baba yangu, na Mimi ni mtoto wako? .." Yule mtu fukara ambaye kwa sasa tayari jina lake lishajulikana kuwa anaitwa Mussa akasema: "Ndio maana Mimi nilitaka mama yako ndio akuambie, kwa sababu ningekuambia Mimi usingeweza kuniamini kabisa ..." Monalisa akamgeukia tena mama yake na kumuuliza: "Ahsante sana mama nashukuru Leo kwa kuniambia ukweli kuhusu baba yangu, lakini pia naomba kujua je Mr Brown naye ni nani kwangu? .." Bi Sophia akafikiria kidogo halafu akamjibu: "Mr Brown sio baba yako, baba yako wa ukweli ni huyo hapo!" Monalisa na rafiki yake Suzzy sasa ndio walichoka kabisa kusikia hivyo! "Sawa mama nimekuelewa, nini sasa kimetokea mpaka baba yangu kuwa hivi analala kwenye mabanda kama haya halafu sisi tunaishi na kulala sehemu nzuri? .." Monalisa bado aliendelea kum'bana kwa maswali mama yake. Bi Sophia akuweza kumjibu kitu Monalisa akabaki tu analia! Monalisa naye huku akiwa analia akamuuliza yule mtu (Mussa) "Eti baba kwanini wewe upo na maisha hayo, tofauti na sisi? .." Yule mtu akamjibu Monalisa: "Swali hilo mwanangu, naomba umuulize mama yako yeye ndio anajua chanzo cha Mimi kuwa hivi! .." Monalisa akamgeukia mama yake na kumuuliza kwa hasira: "Mama nataka uniambie kwanini baba yangu anaishi maisha haya ya kifukara! .." Bi Sophia akafuta machozi yaliyokuwa bado yanamtoka halafu akamwambia Monalisa: "Mwanangu Monalisa, wewe na baba yako naombeni mnisamehe sana najua mimi ndie mwenye makosa ..." alisema Bi Sophia! "Ndio uyaseme sasa hayo makosa yako, sisi tunakusikiliza! .." Monalisa alimwambia mama yake kwa msisitizo. Bi Sophia sasa akajiweka tayari kusema nini kilitokea mpaka yule mtu fukara aitwae Mussa ambaye sasa ni baba mzazi wa Monalisa kuwa vile !! ,,,, ITAENDELEA
MONALISA
SEHEMU YA: 09
Monalisa sasa akawa anataka kujua nini kimemsibu baba yake ambaye ni yule mtu fukara aitwae Mussa na sasa ndio anam'bana mama yake hapa ili apate kusema. Bi Sophia akajiweka sawa na kusema: "Lakini Monalisa mwanangu, hiyo bado ni mapema sana wewe kujua kila kitu! .." Bi Sophia alisema "Bado mapema vipi mama? hiyo ni muhimu kwangu kujua nini kimemtokea baba yangu .." Monalisa naye akasema. "Ni sawa mwanangu lakini kwa leo kujua kuwa huyo ni baba yako inatosha hayo mengine utayajua taratibu nitakueleza! .." Bi Sophia aliweka mkazo wake! Monalisa akamgeukia baba yake: "Sasa baba kuanzia sasa hivi ndio mwisho wako wewe kuishi kwenye hili banda! .." Monalisa alimwambia. "Ndio mwisho wangu kuishi hapa, sasa nikaishi wapi? .." aliuliza Mzee Mussa. "Tunaenda kuishi wote nyumbani kwangu! .." Monalisa alimjibu. "Hapana siendi kuishi na mtu yeyote, kwanza nimefurahi kukuona mwanangu umekua mkubwa basi inatosha .." alisema Mzee Mussa. "Hapana baba siwezi nikakuacha uishi maisha haya na wakati Mimi nipo! .." Monalisa alimwambia baba yake. "Nimesema hivi, siendi kuishi nyumbani kwa mtu yeyote nimeridhika na maisha yangu! .." Mzee Mussa aliweka msimamo wake kwa Monalisa. "Basi kama ni hivyo baba, kuanzia sasa ña mimi nitaishi hapa pamoja na wewe! .." Monalisa alisema huku akilia machozi. Lakini hiyo aikusaidia kwa Mzee Mussa kubadilisha msimamo wake bado aliendelea kukomaa! Sana sana akatoa mfuko wake wa Rambo uliokuwa umejaa makoko ya wali na kuanza kula mbele yao makoko hayo. "Baba hebu tazama mbu waliojaa humu kwenye hili banda, tafadhali naomba ukubali tuondoke wote .." Monalisa alisema kwa kubembeleza. "Kama ni mbu mimi tayari nimeshawazoea, naombeni muondoke na mniache na maisha yangu hapa! .." Mwanaume alisema huku akiendelea kutupia zile tonge za makoko hayo ya wali kinywani mwake kama vile hana Akili nzuri! Monalisa sasa akawa analia kwa sauti baada kuona amegonga mwamba kumshawishi yule mtu fukara (Mzee Mussa) kuondoka ambaye ni baba yake naye. Suzzy rafiki yake Monalisa ambaye muda wote alikuwa yupo kimya akanyanyuka kwenye benchi ambalo alikuwa ameketi bandani hapo na kisha akaenda kupiga magoti mbele ya yule mtu na kumwambia: "Tafadhali naomba umkubalie Monalisa ombi lake la kutaka kuondoka na wewe, akiwa ni kama mwanao basi ni lazima umpe furaha yake .." Suzzy alisema. Yale maneno ya Suzzy yalionekana kumuingia sawia masikioni kwake akaacha kwanza kula Yale makoko yake ya wali na kuuweka pembeni mfuko huo na halafu akasema: "Sawa nimekuelewa binti, lakini natoa sharti moja, sitaenda kuishi nyumbani kwake moja kwa moja labda anitafutie hoteli .." Monalisa alifurahi kusikia hivyo na akasema sawa atampeleka hotelini kwenda kuishi Lakini sio aendelee kuishi kwenye banda hilo la mama lishe ambalo lilikuwa limejaa mbu utafikiri ndio kiwandani wanapozalishwa mbu hao. Basi baada ya hapo wakatoka mle ndani ya lile banda wakiwa pamoja na yule mtu fukara (Mzee Mussa) na kwenda mpaka Monalisa alipopaki gari yake na halafu wakaingia ndani ya gari! Monalisa alimuweka siti ya mbele baba yake na Bi Sophia na Suzzy walikaa siti ya nyuma. Safari ya kuelekea hotelini ikaanza ndani ya gari Monalisa bado alikuwa na mawazo ya kutaka kujua nini kilitokea hapo mwanzoni mpaka huyu mtu fukara ambaye ndie baba yake kuishi maisha haya. Na pia alitaka kujua vile vile ni kwanini mama yake anaishi na Mr Brown na ikiwa pale mwanzoni kule kwenye lile banda alimsikia mama yake akimwita huyu mtu kuwa ni mume wake. Monalisa yote haya alitamani kuyajua! "Sasa baba kile chakula ulichokuwa unakula kwenye ule mfuko wa Rambo ulikitoa wapi? .." Monalisa alijikuta akiuliza. Yule mtu kwanza akatabasamu kisha akasema: "Kile chakula mwanangu huwa ninapewa na huyo mama mwenye banda lile ninalolala, ananikusanyia mabaki ya chakula na kunipa nikiwa Mimi kama mlinzi wake pale! .." Monalisa maelezo hayo yalionekana kumchoma sana na kubaki akisikitika moyoni. Safari ikaendelea ya kwenda hotelini!
Hatimaye ile safari ya kutoka kule manzese midizini ikawafikisha mpaka kwenye hoteli moja kubwa na nzuri sana ya kuvutia yenye hadhi yake iliyokuwa maeneo ya Sinza. Monalisa akasimamisha gari yake kwenye sehemu ya Maegesho kwenye hotel hiyo ya kifahari na kisha Monalisa akamuomba mama yake na rafiki yake Suzzy wamsubiri ndani ya gari ili yeye ampeleke hotelini hapo baba yake. Basi baada ya hapo Monalisa akiwa na baba yake wakaenda mpaka sehemu ya Reception (Mapokezi) na kuanza kuongea na muhudumu wa hapo. Ilikuwa ni mshangao kwa muhudumu huyo na baadhi ya watu waliokuwa hotelini pale kumuona binti mrembo kama Monalisa amekuja na mtu fukara mwenye muonekano wa kiuwendawazimu kwa uchafu wa mwili wake pamoja na mavazi yake makuukuu yaliyokuwa yamechanika! Monalisa hakujali hilo yeye alichojali kwa wakati huu ni kuhakikisha anampatia baba yake sehemu nzuri na yenye usalama ili apumzike. Yule muhudumu mshangao wake ukazimwa na pesa aliyoitoa Monalisa wakati anaadikisha kwenye daftali LA wageni ili kupata Room (Chumba) na kujikuta akiwasindikiza mpaka kilipo chumba kizuri kilichokuwa kimepambwa kwa thamani ya hali ya juu sana. Baada ya muhudumu kuwakabidhi chumba akaondoka zake na kumuacha Monalisa na baba yake! "Sasa baba yangu haya ni makazi yako ya muda tu, nafanya mpango wa kukutafutia makazi ya kudumu .." Monalisa alisema huku akitabasamu. "Nashukuru sana mwanangu kwa kunijali baba yako ." alisema Mzee Mussa huku na yeye pia akitabasamu. Basi baada ya hapo Monalisa akamuaga na kumuahidi kuwa kesho yake Asubuhi atakuja tena hotelini hapo kumchukua na kumpeleka mjini akamfanyie shopping ya mavazi ya kisasa pamoja na kumpeleka Barber shop (Saloon) wakamnyoe minywele yake iliyosokotana kichwani pamoja na mindevu yake kama mpiganaji wa Al Shaabab. Baada ya kumuagizia chakula kizuri na vinywaji baba yake! Sasa Monalisa akarudi tena kule kwenye gari yake alipomuacha mama yake na rafiki yake Suzzy. Monalisa alijiapiza kuwa hiyo kesho ni lazima aujue ukweli wote wa nini kilitokea mpaka huyu mtu akawa hivi na awaishi pamoja na mama yake na kwanini yeye Monalisa alelewe na Mr Brown na wakati baba yake mzazi yupo. Kwa kuwa tayari Monalisa keshaandaa hapa mazingira kwa huyu mtu basi alijipa imani kuwa atamuambia ukweli wote hiyo kesho yake!!, ITAENDELEA SEHEMU YA 10 KAMA KAMA KAWAIDA ENDELEA KU_LIKE NA KU_COMMENT ILI TUSONGE MBELE! AHSANTE KWA KUISOMA.
MONALISA
SEHEMU YA: 10
Baada ya Monalisa kumuacha baba yake pale hotelini sasa akaingia kwenye gari yake na kuwakuta Bi Sophia pamoja na rafiki yake Suzzy wanamsubiri ndani ya gari. "Vipi umefanikiwa kupata chumba? .." Bi Sophia alimuuliza Monalisa. "Ndio mama nimefanikiwa, na nimemuacha anakula chakula .." Monalisa alimjibu mama yake na safari ikaendelea. Baada ya nusu saa wakafika mikocheni nyumbani kwa Mr Brown na Monalisa akasimamisha gari nje ya geti hiyo ilikuwa ni majira ya saa 3:30 usiku. "Vipi autaingia ndani kumsalimia baba yako? ." Bi Sophia aliuliza "Hapana mama kwa sasa ngoja tuwahi nyumbani, kesho nitakuja kumuona baba .." Monalisa alimjibu mama yake na Bi Sophia akashuka kwenye gari na kuwatakia safari njema na usiku mwema Monalisa na Suzzy Monalisa na Suzzy. Basi Bi Sophia akafunguliwa geti na mlinzi wa pale nyumbani na huku nyuma Monalisa akaiondoa gari yake na kuondoka kurudi nyumbani kwake mbezi beach. "Duuh hii inshu ya leo mbona kali, kumbe yule mtu ni baba yako Monalisa! ." Suzzy alianza "Yaani we acha tu, kule kunifuatilia kwake mimi nilijua tu hapa ni lazima kuna kitu .." Monalisa alisema huku akiendesha gari. "Lakini nini sasa kimemkuta mpaka kuwa vile lakini?." Suzzy alijaribu kuuliza "Mimi na wewe wote hatujui, nini kimetokea lakini nitafanya juu na chini mpaka nijue ...?" Monalisa alisema. "Mmh lakini kwa jinsi inavyoonekana, pale kuna kitu kikubwa sana kiliwahi kutokea!." Suzzy alimwambia Monalisa "Ni kweli hayo usemayo lakini hii kitu naomba iwe ni siri yetu, usimuambie mtu yeyote Suzzy! .." Monalisa alimtahadharisha Suzzy. "Ahaa Monalisa bhana, sasa kwa mfano naanzaje kumwambia mtu?." Suzzy alimuuliza Monalisa "Hamna mimi nimesema tu Suzzy .." Monalisa alisema na safari iliendelea mpaka wakafika nyumbani kwa Monalisa na baada ya kuoga na kula chakula wakaenda kulala. Monalisa bado alikuwa na hamu ya kujua nini kimetokea kwa yule mtu ambaye ndie baba yake mpaka kuwa vile na kuishi mbali na mama yake (Bi Sophia)
Hatimaye Asubuhi ikafika kama kawaida Monalisa na Suzzy wakaamka na kujiandaa ili kwenda kwenye biashara yao na baada ya kumaliza kujiandaa wakaingia kwenye gari na safari ya kuelekea mlimani city kwenye biashara yao ikaanza. Baada ya foleni za hapa na pale barabarani hatimaye wakafika na Monalisa akamwambia Suzzy: "Sasa best mimi ngoja nikukimbie kidogo, naenda kule hotelini sinza kumuona baba nilimuahidi asubuhi leo nitaenda .." Monalisa alisema. "Poa basi naomba umsalimie sana." Suzzy alisema, na baada ya hapo Monalisa akaingia kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea hotelini kumuona baba yake (Mzee Mussa) Baada ya kufika alimkuta Mzee Mussa anapata bonge la Breakfast (Kifungua kinywa) ikiwa hiyo nayo ni moja ya huduma ya bili yake hotelini hapo Baada ya kusalimiana pale moja kwa moja Monalisa akamwambia kuhusu ule mpango wake wa kumpeleka mjini kwenda kumfanyia shopping ya mavazi. Mzee Mussa alifurahi sana kusikia hivyo na baada ya hapo wakaingia kwenye gari na safari ya kuelekea mjini kwenda kumnunnulia nguo nzuri baba yake ikaanza! Japo Monalisa kule mlimani city alikuwa anamiliki maduka mawili ya nguo lakini nguo nyingi zilizokuwa kule Zilikuwa ni za kike na za kiume Zilikuwa ni kwa vijana wale wanaojiita masharobaro wa mjini, hivyo kwa mtu kama Mzee Mussa hapa ilikuwa ni lazima atafutiwe nguo zinazoendana na haiba na umri wake sio ili mradi nguo tu. Monalisa alimpeleka kwenye maduka makubwa yanayouzwa nguo za aina yake maeneo ya Posta na Mzee Mussa akapata kuchagua nguo nzuri na za kisasa ambapo kwanza akabadili palepale muonekano wake na sasa kuonekana na yeye yupo kwenye hadhi fulani , Yale manguo yake machafumachafu yaliyokuwa yamechanikachanika na kujaa viraka kila kona yakatupwa kwenye dastibani (Pipa la uchafu) Baada ya kuchukua nguo za kutosha pamoja viatu wakapakia kwenye begi na kisha kuelekea sehemu ilipo Barber shop (Saloon) na Mzee Mussa akanyolewa Yale manywele yake pamoja na ile mindevu iliyokuwa imemjaa Kama gaidi la kisomali, na sasa muonekano wake ukawa ni mpya kabisa kama sio yule aliyekuwa analala kwenye lile banda la Mama lishe lililojaa mbu kule manzese midizini. Mzee Mussa alipendeza sana! Alimshukuru sana mwanae Monalisa kwa zile huduma alizompatia, baada ya kuingia kwenye gari Monalisa akamwambia Mzee Mussa: "Sasa baba kuna kitu nataka kukijua, ni kuhusu wewe na mama nini kilitokea kati yenu! .." Monalisa alimwambia baba yake. Mzee Mussa kwanza akashusha pumzi halafu akasema: "Sawa mwanangu usijali nitakuambia kila kitu, naomba kwanza turudi kule hotelini nikakuambie hicho kitu ." Monalisa alifurahi sana kusikia hivyo haraka akaiondoa gari yake na sasa wakawa wanaelekea hotelini ambapo baba yake amemwambia kuwa ataenda kumuambia kila kitu kuhusu yeye na mke wake (Bi Sophia) mpaka kuwa hawapo pamoja, na kisha yeye ndio kama vile walivyomkuta na Yale maisha yake ya kifukara!!,
ITAENDELEA SEHEMU YA 11Alhamisi ijayo
Kama bado hujapata App ya blog hii Download hapo chini 👇
Makala nyingine
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Video Jifunze haya mwanaume Hawezi kuchomoka
Sababu kubwa inayo sababisha mwanaume Kupunguza mapenzi kwako
Fursa ya kujiajiri kupitia blog
Tambua sababu zinazo sababisha wanawake wengi kuachwa na waume zao
Mapenzi pasua kichwa fahamu zaidi
Bonyeza hapa jisajiri upate pesa kwa kupokea na kutuma SMS weka code=XDXX9
0 Maoni