NILIKUPENDA SEHEMU YA 02
ILIPOISHIA........................
Baada ya hapo akachukua picha ya Loveness na kuifanyia Editing kwa kukata sura ya Loveness na kuiweka kwenye sura ya yule mwanamke aliopiga picha ya ngono,picha ikawa na muonekano tofauti ilionekana ni kama Loveness ndio kapiga picha hiyo.
Baada ya hapo Dick aliingia Whatsapp na kumkuta Loveness akiwa Online kisha akaingia Inbox na kumtumia Picha hiyo huku chini akiandika maelezo ya vitisho"Usipokubari kulala na mimi naisambaza."
Hapo hapo Loveness akajibu
"Dick husifanye hivyo,nakuja nyumbani kwako sasa hivi,ila naomba usizisambaze."
"Fanya haraka.."
"Sawa Dick nakuja....."
Je,nini kitaendelea.................
ENDELEA NAYO.....................
Dick aliendelea kujilaza katika kitanda chake huku akiendelea kusubiri uwepo wa Loveness mahali hapo,kwa wakati huo alikuwa akitawaliwa na msongo wa mawazo juu alichokifanya kwa lengo la kumpata Loveness.
Muda kidogo ulizidi kwenda napo ukimya ukizidi kuchukua nafasi.Kutokana na hali hiyo,ilimfanya Dick kuanza kunyemelewa na usingizi.
Sauti ilisikika ya mtu akigonga mlango huku akiwa nje.Sauti hiyo ilimfanya Dick kushtuka kisha akamuhoji mtu aliokuwa nje kwa sauti iliotawaliwa na uchovu ndani yake.
"Nani Mwenzangu.??"
"Dick ni mimi Loveness fungua...!!!"
Dick aliamka kwa pupa kisha akafungua mlango...Namuu akikaribishwa na manukato makali kutoka kwa Loveness,yaliomfanya kuzidi kuchanganyikiwa juu ya urembo aliokuwa nao Loveness.Hakika alikuwa kaumbika kwa namna yake japokuwa kwa wakati huo uso wake ulikuwa ukitawaliwa na Make up ila bado uzuri wake ulizidi kuonekana vyema.
Dimpozi zilizidi kuonekana kwa Loveness...Kutokana na muonekano aliokuwa nao Loveness ulimfanya Dick kukaa kimya huku akiendelea kumtazama kwanzia Juu mpaka chini na kuzidisha matamanio aliokuwa nao.
"We Dick mbona unanitazama hivyo kwani wewe umeniitia nini...."
Dick bila ya kuzungumza alinyoosha mkono wake wa kulia kwa kumruhusu Loveness aingie ndani huku akiendelea kuachia tabasamu la ushindi,baada ya Loveness kuvua viatu vyake aliketi kwenye moja ya sofa kubwa kuliko zote,Dick alitoka nje kwa ajili ya kuangaza usalama,alikuwa akitazamana na kundi kubwa la watoto waliokuwa wakiendelea kucheza michezo yao ya kitoto hukuwengine wakiyaelekezea macho yao mahali Dick alipokuwa.
"Nyie wajinga tokeni hapo...."
Dick alizungumza kwa hasira ya kuwafanya watoto hao wakimbie huku wakiendelea kucheka na mtoto mmoja aliokuwa akijiamini,alizungumza kwa sauti kubwa na iliomfanya Dick kuachia tabasamu.
"Kisa umepata mtoto mkali kutoka kenya Hahahahahaha"
Kisha Dick akaingia ndani,ghafla tabasamu lilikata papo hapo baada ya kuona Loveness ameshika simu yake na kufuta Picha zote alizokuwa nazo,kisha tena papo hapo tabasamu la Dick likarudi.
"Loveness! haitasaidia kitu,hizo picha nilishazikopi katika memory yangu na nimeshaitunza haipo mahali hapa,hivyo bado tu zipo mikononi mwangu,na nimekuita hapa na sio kufanya mapenzi na wewe bali elewa hisia zangu nami ni mwanaume kama wengine.Mi huwa nashangaa sana hivi wanawake hao wanaonihitaji na mimi siwahitaji hivi wao huwaga wananini au huwa wanasumbuliwa na nini au unahisi mi sitatimiza haja zako."
"Dick! huna akili na wewe sio mstaarabu kabisa!.Nimeondoka nyumbani kwa ajili yako,najua unafahamu ni siku ya kuzaliwa kwa mama yangu nahitajika niwepo mahali pale kwanini unalazimisha kila kitu,umeshindwa kuivumilia siku ya leo ikaisha najuta hata kukupa namba zangu."
Loveness alisimama kwa kuanza kuondoka.Dick alipiga magoti huku akiendelea kumuomba Loveness na kumsihi asiwezi kuondoka....Wakati mambo hayo yote yakiendelea kutokea.Sauti ya mtoto mmoja aliokuwa akizungumza kwa kumkashifu Dick,alisikika kwa mara ya pili.
"Nyie njooni muone demu wa kikenya anamzingua jamaa."
Hasira zilimuijia Dick kisha akatoka nje na kuzunguka hadi dirishani mwake na kumkuta mtoto huyo huku akiwa amepanga matofari ya block yaliomuwezesha kulifikia dirisha la Dick na hii ni kutokana na kuwa lilikuwa mbali na yeye alikuwa mfupi sana.
Dick alimshusha mtoto huyo wakati anataka kumpiga,mtoto huyo alizungumza maneno yaliomfanya Dick kupunguza hasira na kumuacha aende zake bila kumpiga.
"Bro,hamna cha ajabu kama demu hakupendi achana naye naona anavyokuzingua."
Dick alirudi chumbani mwake huku akiwa ni mwenye hasira lakini kwa bahati mbaya hakumkuta Loveness alikuwa kaisha ondoka,mawazo yalimuandama Dick.Kichwa kilizidi kumuua kisha akapata wazo la kumpigia simu Loveness.Kila alipokuwa akijaribu kupiga Loveness alikuwa akikata simu na alijaribu zaidi ya mara sita mara ya saba ndio kapokea hukuakitanguliza kashifu na kejeli.
"Dick sikupendi nielewe mbona tunasumbuana tafuta mwingine,sijui kipi kinachokuvutia kwangu kazi tu kunisumbua mshenzi wewe......Na nimeshajua huuni wako, wakati nimeishika simu yako nimeiona picha yangu ulioikata pamoja na faili uliotumia kwaiyo hainitishi kama utahitaji kusambaza picha yangu nami nitasambaza yako tena afadhali mimi baba yangu hafahamiki japo ni tajiri sasa wewe Radio presenter kila mtu anakufahamu sasa kazi kwako ukitumia ubabe nami nauweza pia."
"Lakini Loveness sio kusudio langu kufanya hivyo yote sababu natetea penzi langu kwanini usikubari kuwa muelewa,naishi kila siku kukuwaza wewe ni mara ngapi nimetaja jina lako katika kipindi changu Radioni,ni kitu gani ambacho sijakifanya cha kukuonyesha nakupenda ni kipi!! au sina haki yakuwa mpenzi wako......"
"Umemaliza kuzungumza....sasa naomba unisikilize kwa makini.Sijawahi kukufikiria hata siku moja na wala sikupendi,unashindwa hata kufikiria ni kwanini nilikupa muda mrefu wa kukufikiria yote sababu kukukatisha tamaa na kukufanya uachane na mimi lakini bado humo tu humo tu...."
"Loveness nakupenda,nakupenda na ndio maana naonekana sifai basi sawa."
"Kwaheri Dick siku njema."
Dick alikaa chini na kuanza kulia kama mtoto.Machozi yalianza kumtiririka,alilia kwa sauti ya chini ili kwa mtu yoyote aliokuwa nje asipate kufahamu kwa kila kilichokuwa kikiendelea ndani mwake.
Alisimama kishujaa kisha akainua kitanda chake na kuchomoa waleti yake aliokuwa akiitumia katika kutunzia fedha kwa ajili ya mahitaji madogo madogo huku pia waleti hiyo ikiwa na kadi ya benki.
Aliipachika katika mfuko wa jeans aliokuwa ameivaa kisha akachukua t-shirt pamoja na viatu vyake akavivaa pia.Wakati anataka kutoka ndani ya chumba hicho alikumbuka hajapiga mswaki hivyo akarudi ndani na kuingia hadi bafuni kwa lengo la kupiga mswaki kisha alipomaliza akatoka nje na kuibana kufuli yake.
Safari yake ilikuwa ikianza katika mgahawa aliouzoea katika kupata chakula pindi tu alipokuwa akihisi njaa,alifika na kisha akapata chakula kiukweli alikuwa hana raha kama alivyozeelewa.Kwa watu waliokuwa wakimfahamu wengi walimuhoji huku wengine wakiendelea kujiuliza maswali juu yake.Lakini kila aliomuhoji hakuweza kumjibu chochote.Tofauti na kumtazama kwa jicho la unyonge.
Japo kwa siku hiyo alinunua chakula kidogo lakini alishindwa kukimaliza,alianza safari ya kuelekea mahali hususi kwa ajili ya uchoraji kisha akazungumza na mchoraji kwa maelewano amchoree picha aliokuwa akihiitaji,walikubaliana malipo kisha Dick akaingia katika simu yake na kwenda hadi kwenye status aliokuwa ameiweka Loveness na kudownload picha ya mama yake Loveness,kisha akamkabidhi mchoraji na kumsihi amchoree picha hiyo kwa ukumbwa sana kisha baada ya kumaliza kuchora aandike"Kheri ya siku ya kuzaliwa."Dick alichomoa shilingi Elfu hamsini kwani ndio waliokuwa wamekubaliana na kumpatia mchoraji huyo.
Baada ya nusu sana picha ilikuwa imeshakamilika,Dick aliomba picha hiyo, ifunikwe na hisionekane.Lengo lake lilikuwa,ni kumkabidhi mama yake Loveness kama zawadi.
Muda huo Dick alirudi nyumbani kwa lengo la kujiandaa kikamilifu kwani maelezo yote juu ya hafla hiyo ya siku ya kuzaliwa kwa mama yake Loveness,Loveness alikuwa ameshaandika maelezo yaliojitosheleza juu ya mahali inapofanyika na muda kila kitu kwenye status aliokuwa ameiweka Whatsapp.Dick alikuwa akifahamu japo hakujua ataingieje katika ukumbi huo kwani hata kadi alikuwa hana.Kisha akapata Jibu na kugundua kila kitu ni pesa.
Yalivyofika majira ya saa tatu Dick aliondoka nyumbani kwake na kwenda mahali hafla ilipo,japo walinzi walimzuia Dick katika kuingia ila Dick alitoa hongo na kuruhusiwa.
Watu walikuwa wengi sana na nikutokana na umaarufu aliokuwa nao mama yake Loveness,taratibu zote ziliendelea huku Dick akiwa ameificha zawadi katika mkoti wake wa suti,na kuketi mahali palipojificha sana.
Taratibu ziliendelea huku akiendelea kumtazama Loveness alionekana kuwa na furaha sana,muda wa chakula ulifika Dick hakuweza kwenda kuchukua chakula kwa kuepuka kuto kuonekana kwa Loveness japo alikuwa na njaa sana.......
Ulifika muda wa keki,kisha Dick akasimama na kuwashangaza wengi kwani ujio wake ulikuwa haufahamiki kabisa,alifika mbele hapo na kumlisha mama yake Loveness keki huku Loveness akionekana kukunja uso na nafasi hiyo ilitolewa kwa mtu yoyote atakaohitaji kumlisha keki mama Loveness ndio maana Dick alisimama.
Dick baada ya kumlisha mama yake Loveness keki huku mkono mmoja ukiwa umebana picha ya mama huyo,aliichomoa picha hiyo na kuwafanya watu wengi kupiga kelele za shangwe mama Loveness alimbusu Dick kwenye paji la uso huku pia mama huyo akishuka chini kwa lengo la kumpigia magoti Dick lakini Dick alimzuia kufanya hivyo.Ni zawadi dogo sana lakini ilimvutia mama huyo......Dick aliondoka huku machozi yakimlenga na kutoka nje............
Baada ya kufika nje na kutaka kuondoka,aliichoma simu yake kwa lengo la kuangalia muda,yalikuwa majira ya saa nne na nusu usiku.Hapo hapo ujumbe uliingia katika simu yake na alipoutizama alikuwa si mwingine bali ni Loveness........
Mwisho wa story asante kwa kusoma mpaka mwisho wa story yetu karibu kwa maswali maoni na ushauri ikiwa una tangazo unahitaji tukutangazie Humu pia
*BADILI MAISHA*
*Ukitaka kufahamu njia ya kutengeneza Dora 100 mtandaoni kwa mtaji wa Sh:35,000 njoo inbox nikupe huo mchongo*Whatsapp
kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇
0 Maoni