NILIKUPENDA SEHEMU YA KWANZA 01
Jua na kiza viliambatana mfululizo na kuzifanya siku ziende kwa kasi,ilianza asubuhi jioni usiku pia na hatimaye siku kukatika.Kwa upande wa Dick ilikuwa tofauti sana kwake aliona ni kama siku haziendi na wala hazisogei pia hasa pale alipomtongoza Loveness na Loveness kumuhaidi atampa jibu baada ya wiki moja kupita.
"Ooh zimebaki siku chache nimuwini huyu mwanamke,daah leo ikiisha inabaki siku moja,lakini hapana hivi jamani nakuwa kama mngojwa anayesubiri matibabu........kwani Loveness hawezi jua moyo wake unahitaji nini mpaka wiki iishe.kwangu mimi I can't wait.Siwezi kuvumilia nimeshindwa."
Dick alizungumza huku akiishika simu yake kwa lengo kwa kutafuta namba ya Loveness katika simu yake kwa lengo la kumpigia.....Alikaa muda kidogo kisha simu ikapokelewa.
"Hallow...!"
"Niambie Dick hujalala tu...!?"
"Loveness hofu ndio sababu ya haya yote,hata usingizi hauji kabisa nimeona siku ulizonipa nisubiri jibu ni kama adhabu kweli jamani...!!"
"Dick we mtoto wa kiume,umekaa kwa mama yako tumboni miezi tisa bila ya kuzungumza na mtu na wala bila ya kufanya chochote kile na ukaweza, utashindwa kunivumilia kwa wiki moja tu...!"
"Oooh Loveness sipo kwenye mzaha natumaini ungekuwa mimi usingepata hata muda kunitania.....waza fikiri amini nakupenda...!"
"Lala bwana imebaki siku ya kesho tu hofu yako ni nini,mbona siku ya leo imeisha saa tano sasa hivi,kesho hii hapo...mimi ningekuwa wewe ningekuwa mvumilivu au nikupe jibu baya sasa hivi.....Maana inaonekana una haraka sana na jibu langu."
"Loveness usinikaripie naomba unisamehe sio kusudio langu ni kusudio la moyo wangu.Kama nimekukosea naomba unisamehe na nitajitahidi kuwa mvumilivu japo itakuwa ngumu."
"Dick kuna kitu unanitafuta....umeshanikera......."
"Hallow hallow,Loveness......."
Loveness alikata simu nakumfanya Dick akose raha aonekane kama mtu mwenye matatizo lukuki,katika upande wa kusubiria jibu hasa kwa kwa wale wakina dada wanaopenda kuwaambia watu watawafikiria kwa Dick ilikuwa kama adhabu na tena adhabu hisiokuwa na hukumu.
Usiku wa Dick ulikuwa kama miaka,Dick alikuwa ni kijana ambaye ukimtazama kwa mbali unaweza kugundua ni mtu asiyekuwa na shida na kwa tafsiri ya haraka ungegundua Dick ni mtu ambaye kwake ni ngumu kuteswa na mwanamke.Na watu wengi walimtofasiri hivi kutokana na kutwa Dick alionekana kuwa na tabasamu lisiloisha utamu iwe kwenye shida alikadhalika kwenye raha lakini tabasamu kwake lilizidi kunawili.
"Daah mapenzi haya yanamaajabu sana sasa kweli kosa langu liko wapi kumpigia au nini,kanipa mawazo sasa ambayo hata sikuyatarajia..."
Dick alivuta pumzi taratibu kisha akaanza kuishusha pole pole,wakati anataka kupanda kitandani ili apate kungamana na usingizi muito wa simu yake ulisikika kwa mara nyingine,tabasamu lake lilianza kuja kwa kasi na ni baada ya kuhisi huenda mpigaji ni Loveness na si mwingine huku akiendelea kuhisi huenda Loveness anahitaji kumuomba samahani kwa alichomfanya muda si mrefu.
Baada ya Dick kuikamata siku yake na kuiweka kiganjani mwake aligundua si Loveness aliokuwa mpigaji bali ni mwanadada aliokuwa jirani yake huku akimsumbua kila siku kwa kumuhitaji kimapenzi.
"Hallow....!!!"
Dick alizungumza sauti ya uchovu iliotawaliwa na usingizi ndani yake na yote aliifanya hivyo ili mpigaji aamini aliyempigia yupo katika himaya ya usingizi lakini ilikuwa sivyo kwani bado Dick alikuwa na uadui na usingizi.
"Dick mpenzi wangu umelala,nije Dick tulale Dick....."
"Farida nielewe sikuhitaji utazeeka kila siku ukililia penzi langu,chaguo lako anahangaika mtafute ameshamkufuru mungu mara kibao kwa kuonekana hana bahati ya kupata mwanamke kumbe maskini ya mungu chaguo lake unanisumbua...."
"Dick unamaanisha nini kuse......"
Kabla ya Farida hajamaliza kuzungumza Dick alikata simu kisha kwa haraka akaizima simu yake,alijirusha kitandani huku akiendelea kumfikiria Loveness ndio muda aliokumbuka msemo wa waswahili."Mpende akupendae"
"Siwezi kutoka na Farida yani sina hisia naye kabisa hata aje niko bafuni naoga ngoma itakuwa vile vile....."
Dick alizungumza maneno hayo baada ya kuukumbuka msemo wa mpende akupendaye.Hatimaye usingizi uliweza kumpitia.
Hatimaye kulikucha Dick bila kuinuka kutoka kitandani aliiwasha simu yake na kufungua data kisha akaingia Whatsapp na kukutana na alama ya kuonyesha ya kuwa kuna status mpya,hivyo akaenda mpaka sehemu ya status akakuta alieweka status si mwingine bali ni Loveness,kidogo akaifungua...
Tabasamu la ghafla lilikuja na kupotea,pia tabasamu lake lilikuja baada ya kuona maelezo aliokuwa ameyaandika chini ya picha "Nielewe Nakupenda.."Aliitazama picha yenyewe na kugundua maelezo hayamuhusu yeye bali alikuwa amemuandikia Mama yake mzazi aliokuwa ameiweka picha yake huku akimtakia kheri ya siku yake ya kuzaliwa na Dick alithibitisha jambo hilo baada ya kusogeza picha ya mbele na kukutana na maelezo tu yaliokuwa yakisomeka vyema"Kheri ya kuzaliwa mama yangu,nakupenda sana."
Hapo hapo Dick akaliplay kwa kutoa maoni katika stastus aliokuwa ameipost loveness"Hongera kwa siku ya kuzaliwa kwa mama mkwe.."
Baada ya kutuma hivyo Loveness aliiona kisha akaanza kuandika majibu na kumtumia Dick.Alikuwa amemtumia Dick emoji inayoonesha ana hasira
toka Online
"Wanawake bwana sijui nikapendeje haka katoto kananikera,hakataki nikasifie wala nini."
Dick alitoa maneno ya kejeli,kisha akasimama na kujiandaa kisha akarudi na kuketi katika kitanda chake.Maisha aliokuwa akiishi yalikuwa ni maisha mazuri sana japo aliokuwa amepanga lakini chumba chake ungepata bahati ya kukitizama ungedhania ya kuwa ni mkurungezi katika kampuni fulani au ni mtu yoyote anayejihusisha na biashara kubwa.
Wazo lilimjia Dick kisha akachukua simu yake na kufungua data na kuingia playstore alidownload App ya kuediti picha,kisha baada ya kuwa App imemaliza kuinstall akaenda Google na kudownload picha ya ngono alijaribu kwa kuangalia picha ya mwanamke aliokuwa na umbo sawa kama Loveness kisha akaipata na kuipakua.
Baada ya hapo akachukua picha ya Loveness na kuifanyia Editing kwa kukata sura ya Loveness na kuiweka kwenye sura ya yule mwanamke aliopiga picha ya ngono,picha ikawa na muonekano tofauti ilionekana ni kama Loveness ndio kapiga picha hiyo.
Baada ya hapo Dick aliingia Whatsapp na kumkuta Loveness akiwa Online kisha akaingia Inbox na kumtumia Picha hiyo huku chini akiandika maelezo ya vitisho"Usipokubari kulala na mimi naisambaza."
Hapo hapo Loveness akajibu
"Dick husifanye hivyo,nakuja nyumbani kwako sasa hivi,ila naomba usizisambaze."
"Fanya haraka.."
"Sawa Dick nakuja....."
Je,nini kitaendelea..........Alhamisi Ijayo
Mwisho wa story asante kwa kusoma mpaka mwisho wa story yetu karibu kwa maswali maoni na ushauri ikiwa una tangazo unahitaji tukutangazie Humu pia
*BADILI MAISHA*
*Ukitaka kufahamu njia ya kutengeneza Dora 100 mtandaoni kwa mtaji wa Sh:35,000 njoo inbox nikupe huo mchongo*Whatsapp
kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇
Bonyeza hapa Download App ya MAHABA KWA HABARI ZA BISHARA NA BIDHAA MPYA TAZAMA MAUZO TV |
Makala nyingine
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Video Jifunze haya mwanaume Hawezi kuchomoka
Sababu kubwa inayo sababisha mwanaume Kupunguza mapenzi kwako
Fursa ya kujiajiri kupitia blog
Tambua sababu zinazo sababisha wanawake wengi kuachwa na waume zao
0 Maoni