Ticker

6/recent/ticker-posts

NILIKUPENDA SEHEMU YA 03

 

NILIKUPENDA SEHEMU YA 03 

ILIPOISHIA...........

Dick baada ya kumlisha mama yake Loveness keki huku mkono mmoja ukiwa umebana picha ya mama huyo,aliichomoa picha hiyo na kuwafanya watu wengi kupiga kelele za shangwe mama Loveness alimbusu Dick kwenye paji la uso huku pia mama huyo akishuka chini kwa lengo la kumpigia magoti Dick lakini Dick alimzuia kufanya hivyo.Ni zawadi dogo sana lakini ilimvutia mama huyo......Dick aliondoka huku machozi yakimlenga na kutoka nje...........

Baada ya kufika nje na kutaka kuondoka,aliichoma simu yake kwa lengo la kuangalia muda,yalikuwa majira ya saa nne na nusu usiku.Hapo hapo ujumbe uliingia katika simu yake na alipoutizama alikuwa si mwingine bali ni Loveness........

Je,nini kitaendelea.............

ENDELEA NAYO.........

"Dick nakuomba urudi ndani....."

Sms hiyo ilimfanya Dick kurudi ndani ya ukumbi na kuwafanya watu wote kupiga kelele za shangwe.Yote sababu kwa kitendo cha ghafla cha Dick kuondoka ndani ya ukumbi huo,kiliwapa upweke umati wote.

Tabasamu pia lilionekana kwa Mama yake Loveness na alikuwa hamjui Dick ni nani japo alijaribu kumuulizia mwanae na kumfanya amfahamu zaidi.Dick kama mtangazaji wa Radioni.

Waliweza kumpa Mic kwa lengo la kuzungumza machache huku jasho na machozi yakizidi kumlenga,haikuwa rahisi kuzungumza mbele ya umati mkubwa tena wa matajiri ila ni kwa sababu tayari ndio alikuwa ni mtu mwenye uzoefu wa kutumia Mic hivyo hakuona shida yoyote itakayomzuia kuzunguma.

Watu wengi walikuwa wakitarajia huenda Dick atazungumza jambo kuhusu mama Loveness lakini ilikuwa sivyo.

"Ndugu zanguni.Wakubwa zangu shikamooni,na wadogo zanguni marahaba na kwa tunaolingana habarini za usiku huu.Natumaini mu wazima wa Afya,ningependa niongee kitu mbele yenu ili kumfanya mtu fulani aamini kila kitu kutoka kwangu."

Kutokana na kauli hiyo iliwaacha watu wengi njia panda kwa kushindwa kuelewa kabisa kile alichokuwa akimaanisha,na kwa upande wa Loveness alikuwa ameshagundua alitaka kumzungumzia yeye na si mwingine.

Dick alikohoa kwa muda kisha akaendelea kuzungumza....

"Mama Loveness na  wengine wote napenda kusema ukweli wangu,utakaotoka moyoni."

Dick alimgeukia Loveness.

"Loveness nakupenda sana, tambua umuhimu wangu kwako,chozi ili si la bure najua unanichukia ila amini nakupenda.Ni ngumu mtu kuamini kama mapenzi yanaweza kunitesa kutokana na jinsi nilivyo,ila aminini nawaambieni.Mapenzi hayana komandoo wala jambazi wala steringi.Mapenzi umuumiza kila mtu.Sioni haya kukataliwa mbele zenu naomba Loveness uniambie mbele ya huu umati kama unanipenda au hunipendi....!!"
Loveness hakuweza kushika Mic tofauti na kudondosha machozi ya kumuhurumia Dick kutokana na mambo anayoyafanya juu yake,Mama yake Loveness pamoja na umati huo uliokuwepo mahali hapo.Walikuwa wakimuomba Loveness ashike Mic na kuweza kuzungumza chochote kile.Lakini Loveness alikataa kushika Mic kabisa.Kutokana na kitendo hicho kilidhihirisha hampendi Dick.Hivyo Dick akaamua kuondoka zake huku akiendelea kudondokwa na machozi,aliita Tax iliompeleka mpaka anapoishia.

Dick alikuwa akifikiria mambo mengi sana juu ya Loveness alihisi kama,mwanamke kama Loveness hayupo duniani hivyo alizidi kuonyesha juhudi juu ya kumuonyesha upendo Loveness aidha hadharani au popote pale.

Kwa tukio alilolifanya katika hafla ya kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa kwa mama yake Loveness,kidogo ilimpa muangaza wa ushindi,kwani alikuwa tayari ameshajenga undugu mzuri na ukaribu kwa mama yake Loveness jambo ambalo hakulitegemea na pia Dick anafahamu huenda Mama Loveness akawa yupo upande wake na akawa mshauri mkuu wa mwanae.

Dick aliingia ndani huku kumbukumbu ya kazi ikimuijia kichwani alikumbuka kesho yake ambayo ndio jumatatu atakuwa na kipindi Radioni,hivyo alianza kujiandaa kikamilifu japo njaa na uchovu viliendelea kumtawala,kipindi cha Dick kilikuwa ni cha aflajiri na mapema huku kikihusiana na habari pamoja na matukio mbalimbali yanayotokea ulimwenguni.Kufikia muda huo alikumbuka hajaanda habari wala tukio lolote kwa ajili ya asubuhi,kiukweli Loveness alimchanganya sana na kumfanya aanze kusahau vitu vya muhimu kuhusu kazi yake.

Japo usingizi na msongo wa mawazo vilizidi kumkumba lakini alijitahidi awezavyo ili aandae habari na matukio muhimu kwa ajili ya kesho,aliingia BBC swahili na kuchukua baadhi ya habari muhimu pia akaingia pia katika mtandano wa CNN wa ajili ya kutazama matukio ya huko nchini marekani.Alipata habari na matukio mengi kisha aka screenshoot na kuhifadhi katika simu yake.

Kisha akajirusha katika kitanda chake ili aendelee kuupata usingizi uliokuwa ukimnyemelea kila muda.

****
Yalifika majira ya asubuhi kisha Dick akaingia bafuni na kujimwagilizia maji kisha akarudi na kuandaa vitu vyake kwa ajili ya kuwahi kazini,kila kitu kilikuwa kiko sawa kisha akaondoka.

Alifika  Radioni kwa muda husika kisha akaingia kwenye kipindi na kukiendesha kama kawaida,baada ya kipindi kumalizika aliweza kurudi nyumbani.Dick huwa anakipindi kila siku asubuhi kwanzia Jumatatu mpaka Ijumaa,kwa siku za weekend ndio anapata muda wa kupumzika.
Yalikuwa yametimia majira ya saa tano kamili asubuhi kama kawaida ya Dick aliweza kwenda katika mgahawa huo aliokuwa ameshauzoea katika kupata chakula aidha cha asubuhi cha mchana vile vile cha usiku.

Siku zilizidi kwenda huku maisha ya Dick yakisonga kama kawaida,yapita wiki sasa Dick hajaona ujumbe wa Loveness au wa mtu yoyote yule.Jambo lililomkatisha tamaa na kuamua kufanya mambo yake yakimsingi bila ya kujihusisha kwenye mapenzi.

Siku zilizidi kusonga mbele mpaka ikafika weekend,Dick aliamua kwenda kwa rafiki yake aliokuwa akifanya naye kazi pamoja,rafiki yake Dick alikuwa akijulikana kwa jina la Frank ni mtu aliokuwa akipenda sana wanawake na alikuwa ni mtu wa kubadirisha kila siku.Umaarufu aliokuwa nao ndio aliokuwa akiutumia hasa katika kuwarubuni wanawake.

Frank aliweza kumuonganisha Dick kwa wanawake wengi japo Dick hakuweza kukubaliana na Frank.Yapita muda sasa Dick haitaji kushughulisha na mapenzi kabisa na kuhisi huenda ataoa uzeeni na sio ujanani kwani msichana wa ndoto zake hakuweza kumkubali na kuishia kumdharau na kumkashifu kwa kila hatua.

"Dick nasikia unajiabisha sana kwa Loveness,ndugu yangu wewe ni maarufu nani asiyekufahamu hapa tauni,unajiaribia jina mwenyewe..."

"Frank kwenye mapenzi kila mtu huonekani hafai ila siku nitakapomuoa yule atakayekuwa ananiaibisha,nitaonekana bora kuliko mwanaume yoyote yule,sema nini rafiki yangu mapenzi hayana mwenyewe.Pia Frank ukipendwa pendeka,ukipata nafasi ya kumpata anayekupenda basi hakikisha umuachi na akaenda.Jaribu kuzidisha mapenzi ya dhati ili uumfanye aliyekubali kuwa na wewe hasijute kwa maamuzi alioyafanya ya kukuchagua wewe.Pia Frank nahisi hawa wanawake ulionao hamna anayekupenda hata mmoja wote wanakupendea pesa na umaarufu ulionao nina uwezo wa kuwa kama wewe ila lengo langu nimpate ambaye hanipendi ila mwisho wa siku nifanye kitu kitakachomfanya anipende na sio umaarufu kama unavyodhani.."

"Dick unachozungumza ni sahihi sana,japo kwa wakati mwingine ni kupoteza muda tu.Ukiwa unafanya kazi kama hizi hutakiwi kuchanganya mapenzi utajikuta unaharibu kila kitu,ndio maana mi nakuwa na wasichana wengi ili huyu akizingua nashika huyu,we unadhani mi mapenzi yanaweza kuniumiza kama wewe."

"Frank! tuachane na hayo ndugu,nisikilize kwa kilichonileta hapa,."

"Sawa niambie Dick.."

"Leo usiku bata wapi..."

"Hapana Dick leo sitoki ninaapointment nyingi na wake zangu so itakuwa ngumu my friend."

"Basi sawa,ngoja niingie nyumbani sawa???"

"Sawa."

Dick aliamua kurudi mahali anapoishi huku bado taswira ya Loveness akiendelea kuutawala ubongo wake,nguvu ya mapenzi ilikuwa ikionekana kwa Dick,na mapenzi yalikuwa yakimtesa sana.

Dick alikuwa na muonekano wa kipekee,ni ngumu kwa mtu kuamini kama Dick alikuwa akiteswa na mapenzi.Wakati Dick akiwa kwenye Tax huku dereva akizidi kuongeza mwendo,simu yake iliita,alimtazama mpigaji alikuwa si mwingine bali mwanadada jirani aliokuwa akimsumbua na kuendelea kumtaka kimapenzi kisha Dick akaipokea na kuiweka sikioni.

"Dick jamani nina siku sijakuona,Dick nina habari mpya kuna mtu ananitaka mi nimekatalia na nimemwambia niko na wewe au nimekosea???"

Dick hakuweza kumjibu chochote tofauti na kukata simu.

"Dereva nishushie hapa..."

Jumbe tano ziliingia katika simu yake huku zikitoka kwa mwanadada huyo jirani yake na Dick.

"Dick kosa langu ni lipi!!"

"Kukupenda!!"

"Kukujali au pia kukupa nafasi kubwa kwenye moyo wangu."

"Sikurubuni kwa chochote,ila amini nakupenda niko tayari kujiondoa duniani hasa pale nitakapokuta una mpenzi mwingine."

"Mi najua unanipenda,usiku mwema."

Jumbe zote Dick alizipitia kwa umakini kisha akashuka kwenye Tax na kumlipa Dereva pesa yake na kisha akapiga hatua za kwenda mahali alipokuwa amepanga.

Nyumba aliokuwa amepanga ilikuwa na chumba kimoja kilichosheheni choo na bafu humo humo,pamoja na sebule.(Self container)

Ilikuwa yapita wiki Dick alikuwa hana mawasiliano na Loveness,simu yake iliita ilikuwa ni namba ya mwenye nyumba kisha Dick akaipokea simu hiyo na kuiweka sikioni.

"Hallow habari mwenye nyumba.!!"

"Nzuri Dick! nina habari mpya,nilikuhaidi ujenzi wa nyumba yangu mpya ukikamilika nitakuuzia hiyo na umekamilika hivyo kama hutojali tunaweza kufanya biashara pia."

"Aha mzee Matege,mbona mkataba wangu hujaisha au tutajumuisha pamoja na mkataba...!!??"

"Ndio mwanangu."

"Basi mzee wangu nitakupatia milioni kumi tu kijinyumba chenyewe si unakiona kilivyo kidogo."

"Basi sawa ndugu utanipatia tu milioni tisa maana wewe ni kama mwanangu wa kumzaa,na shida ikitokea huwezi kuacha kunisaidia."

"Nitumie namba zako za benki kesho nitakuamishia fedha."

"Sawa Dick,kesho si jumapili,nitahakikisha nakueleta hati ya nyumba.Kabla hujaenda kufanya malipo."

"Sawa mzee wangu."

Muda si mrefu mzee huyo alitumia namba ya Bank ya NMB aliokuwa akitumia kwa njia ya sms.

Kidogo maisha ya Dick yalianza kutawaliwa na furaha kwa kuona anasonga mbele kimaendeleo,endapo akimaliza biashara ya kuinunua nyumba hiyo,alikumbuka kila jumamosi usiku huwa anawatumia wazazi wake kiasi kidogo kwa ajili ya kujikimu kimahitaji hivyo aliweza kufanya muamala usiku huo.
Baada ya kukamilisha kila kitu simu ilipigwa kutoka kwa mama yake mzazi.

"Habari mwanangu!pesa nimeiona ahsante sana,baba yako anakusalimia.."

"Sawa mama! mwambie mwanao mi mzima wa afya mungu anasaidia."

"Sawa mwanangu nakutakia usiku mwema."
"Sawa mama.!"

Dick aliweza kuvuta shuka na kuendelea kuuchapa usingizi.

****

Ilikuwa ni saa mbili asubuhi Dick aliweza kuamka na kutoka katika kitanda chake,alichukua simu yake kwa lengo la kumtafuta mzee mwenye nyumba ili alete hati ya nyumba.Ghafla alikubana na ujumbe kutokana kwa Loveness uliosomeka vyema.

"Umeamkaje Dick....?"

Je,nini kitaendelea......Alhamisi Ijayo

Mwisho wa story  asante kwa kusoma mpaka mwisho wa story yetu karibu kwa maswali maoni na ushauri ikiwa una tangazo unahitaji tukutangazie Humu pia

*BADILI MAISHA*

*Ukitaka kufahamu njia ya kutengeneza Dora 100  mtandaoni kwa mtaji wa Sh:35,000 njoo inbox nikupe huo mchongo*Whatsapp 

kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇

Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();