Ticker

6/recent/ticker-posts

NILIKUPENDA SEHEMU YA 04

 


NILIKUPENDA SEHEMU YA 04 

ILIPOISHIA.......

Ilikuwa ni saa mbili asubuhi Dick aliweza kuamka na kutoka katika kitanda chake,alichukua simu yake kwa lengo la kumtafuta mzee mwenye nyumba ili alete hati ya nyumba.Ghafla alikubana na ujumbe kutokana kwa Loveness uliosomeka vyema.

"Umeamkaje Dick....?"

Je,nini kitaendelea............

ENDELEA NAYO.....

Mikono ya Dick ilianza kutetemeka furaha nayo haikuacha kuchukua nafasi,alihisi huenda Loveness atakuwa amemfikiria na kumpa nafasi katika moyo wake.

Dick alimjibu sms hiyo huku akiendelea kuachia tabasamu lililofanya meno  yote thelathini na mbili(32) kuonekana vyema.

"Nzuri Loveness za siku..."

"Nzuri tu rafiki yangu Dick...."

Nguvu zilimuishia Dick hata tabasamu kupotea,alijua huenda labda Loveness atakuwa amemfikiria kwa kiasi fulani kumbe ndio kazidi kumuumiza kwa kumpa kitengo kibaya ambacho huwa hakipendi maishani mwake na huwa hapendi mwanamke ahitaji urafiki naye kwa kuhisi ni dharau tosha.

Dick aliacha kuendelea kuwasiliana na Loveness huku Loveness naye akiendelea kukaa kimya na kutotuma tena sms yoyote kwa Dick.

Kidogo mlango ulibishwa,Dick alitoka nje na kumuangalia muhusika.Alikuwa ni Mzee Matege mzee mwenye nyumba.

"Shikamoo Mzee wangu..."

"Marahaba,mwanangu sasa mimi nina haraka kidogo sitaingia ndani.Ila hii hapa hati ya nyumbani nadhani tutakuwa tumemaliza.Unajua hapa mjini tunafanya biashara ya akili sio lazima twende mahakamani sijui kusaini madude yale,yanatupotezea muda."

"Ni kweli Mzee wangu nakuamini sana hata ukikaa na hati wewe bado ni yale yale,sema tu na mimi naweza kupata shida nikashindwa cha kumkabidhi mnunuzi."

"Sasa bwana Dickson mwanangu,ngoja niwahi japo nina hii baiskeli ila nahisi nimechelewa."

"Sawa Mzee wangu."

Dick aliingia na hati ya nyumba ndani huku akiwa ameishikilia na kuendelea kuichunguza kiasi na kuamua kuiweka chini ya godoro alilokuwa akilalia.

Kabla hajakaa mlango ulibishwa kwa upande wa nje,kisha Dick akasimama na kwenda kumfunguliwa muhusika bila ya kujua ni nani aliyekuwa akigonga mlango.

Baada ya kupiga hatua chache kisha akaufungua mlango, alikaribishwa na Mwanadada jirani huku akiwa anabubujikwa na machozi.

"Dick nakupeda tazama unavyonitesa hunishikii fimbo kunichapa na wala hutumii mkono wako kunidhuru lakini nateseka kiasi hiki naumia kiasi hiki...."

Dick hakutaka kuendelea kumsikiliza tofauti na kurudishia mlango.

"Dick fungua nitajaza watu hapa....."

Dick alifungua na kumruhusu aingie ndani kisha wakaanza kuzungumza...

"Dick unanipenda...."

Mwanadada Mariam alimuhoji Dick huku akilazimisha tabasamu lililofanya machozi yaendelee kumtiririka.

"Mariam,hapa nina mawazo sana nimefukuzwa kazi,nimegombana na wazazi wangu muda wa kodi ya nyumba umefika ni shinda tu mpaka hapa nashindwa kutoka nje kiukweli,akaunti yangu ya benki yangu imefungwa kutokana na kuwa sikukamilisha usajili.Nina zaidi ya shida."

"Heeeeh na bado,nani mwenye uwezo wa kuwa na wewe kama huna kitu,na mwaka huu utakoma."

Mariam aliendelea kuzungumza na Dick huku akiendelea kukunja vidole vitatu katika mkono wake wa kulia mithili ya mwanamke anayemchamba mwanamke mwenzie.

Mariam aliendelea kutoa maneno ya kashifu kwa Dick huku akiendelea kutikisa kiuno.

"Wewe una uwezo wa kuwa na mwanamke kama mimi huna uwezo wa kunihudumia,nahitaji matunzo,Mariam mimi nitoke na mtu hasiyekuwa na fedha,Hehehehe nicheke ninenepe mwezio."

Dick aliendelea kumtazama Mariam kwa jinsi alivyokuwa akiendelea kujisifia huku akiendelea kumkejeli Dick.

"Sasa kama huna kazi,si urudi kwenu huko,unafuata nini katika mtaa wetu.Wewe ndio unaongeza umaskini katika taifa letu hujishughulishi...Yani wewe ningekuwa na uwezo hata jiji ili ningekufukuza ukafie mbele....."

Dick bila ya kuzungumza chochote alisimama na kufungua mlango kisha akamruhusu Mariam kwa ishara ya mikono ili aweze kutoka nje,Mariam hakuacha kuendelea kuonyesha dharau alizokuwa nazo.Wakati anatoka nje aliweza kutema mate ndani ya chumba cha Dick kisha akaondoka.

Baada ya Dick kubana mlango,alifurahi sana kwa kitendo alichokifanya juu ya Mariam kwa kumdanganya mambo ya uongo ili aone kama amempenda kutoka moyoni.

Lakini pia kwa kutumia kipimo hicho hicho cha uongo kilimfanya agundue Mariam ni mwanamke aliokuwa na dharau.

Japo alikuwa na uwezo wa kumpiga kutokana na dharau alizokuwa akizifanya,ila alichokitaka ni lengo lake kutimia lengo la kuachana na Mariam.Marima alikuwa akimpendea umaarufu aliokuwa nao na si jinsi alivyokuwa.

Dick alianza kungumza kwa sauti ya chini.

"Wanawake ni hatari!,ananipendea umaarufu wangu,basi yeye ana kipi cha kumfanya nimpende.Nimetumia akili sana katika kumwambia vitu hivyo la sivyo ingeleta shida.Huyuni mwanamke hasiyenifaa kabisa! kutokana na kuigiza kwake kulinifanya nimuonee huruma.Nimempa kipimo kidogo sana cha shida zangu na kutokuwa na kitu chochote lakini ameshindwa.Tofauti na kunionyesha dharau kede hadi kunishikia kiuno hadi kunikunjia vidole.Wanawake ni watu wenye dharau sana,nimemdanganya kuhusu kazi,hana hata akili ya kuuliza ni kwa sababu gani ili anitege na kunifanya nijing'ate ng'ate ulimi lakini ameshindwa."
******

Mama Loveness alizidi kumuonea huruma Dick na hapo ni baada ya kuwa ameishikilia zawadi aliopewa na Dick huku akiendelea kuitazama.

"Kijana wangu,zawadi yako ni uthibitisho tosha unaoonyesha una upendo mkali kwa mwanangu.Napenda sana mwanangu akuelewe uje kuwa moja kati ya familia yangu."

Mama Loveness alikuwa akizungumza huku akiendelea kuruhusu huzuni iendelee kumtawala.

Wakati Mama Loveness akiwa sebuleni,aliweza kuiweka zawadi ya Dick pembeni kisha akamuita mwanae Loveness kwa lengo la kuzungumza naye.

"We Loveness mwanangu,Loveness!"

"Abeeh!! mama."

"Njoo mwanangu mpendwa."

Loveness alitoka chumbani mwake huku akiwa ameishikilia simu yake.

"Kaa hapo mwanangu."

Baada ya Loveness kuketi,alimkazia macho mama yake huku akiendelea kutandwa na hofu kutokana na unyenyekevu wa mama yake.Huenda akawa anataka kumpa taarifa mbaya kama ilivyokawaida ya mama kila akiwa na taarifa mbaya huwa anamuita mwanaye tena kwa unyenyekevu.

Lakini pia hofu ya Loveness aliondoka yote baada ya kuona zawadi ya Dick aliompatia mama yake ikiwa pembemi yake,akajua moja kwa moja.Mama yake anahitaji kumshauri juu ya Dick hivyo akawa makini katika kumsikiliza.

"Mwanangu Loveness mapenzi ni kama shule bila wanafunzi haiendi,mapenzi ni kama kufuli bila ufunguo haiendi,mapenzi ni kama kazi bila mshahara haiendi na pia mapenzi ni kama nguo iliojikunja bila pasi hainyooki."

"Mama una maana gani kusema hivyo.!!??"

"Mwanangu ni jinsi gani vitu hivyo vinavyotegemeana na hamna njia ya mkato katika kukwepa vitu hivyo visitegemeane.Mwanangu! Dick anakutegemea sana.Yule ni mfanyakazi una kwamisha kazi zake.Anakutegemea sana katika jambo fulani.Duniani kuna wanawake wengi lakini kakuona wewe umemfanyia vingapi vibaya lakini pindi tu akikuona furaha yake huja ghafla.Mwanangu jaribu kumfikiria hata kwa dakika tano tu fikiria mazuri yake japo sina huakika kama alishawahi kukufanyia baya.Mwanangu mi mama yako,yangu ni hayo."

"Mama nimekuelewa...""Ahsante sana mwanangu kwa kunielewa."

Loveness alizungumza kinafki ili kumpa furaha mama yake lakini ukweli alikuwa akiujua mwenyewe,Loveness alikuwa hampendi Dick ila kuna wakati mawazo yalikuwa yakimtawala juu ya Dick pia kuna wakati huwa hamfikiri kabisa.Loveness alikuwa  na mpenzi wake na alimuumiza sana tangu siku hiyo Loveness alijiondoa kwenye mahusiano na kwa jinsi Dick alivyo na umaarufu anaona ndio muda atakaopata maumivu makali tena yasioisha.Kutafutwa kwa Dick na kila aina ya mwanamke kitampa maumivu makali pia.Loveness anaona akimshauri Dick aachane na hiyo kazi japo Dick anaweza kukubali ila Loveness hataki kitu kama hicho.

Maana anahisi wapo wanaomtegemea Dick wapo wanaompenda kutokana na kazi anayoifanya hivyo akifanya hivyo atamuharibia maisha yake.Anaona ni bora kuzuia.nafsi yake katika kumpenda Dick.

Loveness aliondoka mbele ya mama yake huku akilazimisha tabasamu ambalo hakuwa nalo kabisa juu ya mama yake ila tu alilionyesha kama kumpa tabasamu mama yake na si vinginevyo.

Loveness aliondoka na kumuacha mama yake alioendelea kujihisi mwenye amani na furaha baada ya kuhisi kana kwamba ameshawishi mwanae katika kumkubali Dick.

*****

Frank aliendelea kusheherekea juu ya ulimwengu wa mapenzi,maendeleo ya Frank yalikuwa ni makubwa kwani alikuwa na nyumba kubwa iliokuwa na uzio pamoja na gari na hii kutokana na kuwa Frank alikuwa ameanza kazi zamani pia alikuwa na miradi mbalimbali iliokuwa ikimuingizia Fedha,Frank hakuacha kuendelea kuwashawishi wanawake wa kila aina japo kwa kila mwanamke hakuacha kutumia kinga ili kulinda afya yake.

Ilifika muda akawa anaenda hadi nje ya nchi kwa lengo la kubadirisha wanawake swala liliofanya akapata umaarufu kwa kubandikiwa jina na vijana aliokuwa akiishi nao mtaa mmoja kama"Tamu ya watoto."

Frank alikuwa akiomba likizo kazini kama mngonjwa na kuitumia likizo hiyo katika kuwasaka wanawake.

Haya yote ni mawazo yaliomkumba Frank na kumfanya akumbuke kipindi cha nyuma mambo aliokuwa akiyafanya.

Pia Frank hakuishia hapo aliendelea kukumbuka maneno ya Dick aliokuwa akimsihi.

"Frank kwenye mapenzi kila mtu huonekani hafai ila siku nitakapomuoa yule atakayekuwa ananiaibisha,nitaonekana bora kuliko mwanaume yoyote yule,sema nini rafiki yangu mapenzi hayana mwenyewe.Pia Frank ukipendwa pendeka,ukipata nafasi ya kumpata anayekupenda basi hakikisha umuachi na akaenda.Jaribu kuzidisha mapenzi ya dhati ili uumfanye aliyekubali kuwa na wewe hasijute kwa maamuzi alioyafanya ya kukuchagua wewe.Pia Frank nahisi hawa wanawake ulionao hamna anayekupenda hata mmoja wote wanakupendea pesa na umaarufu ulionao nina uwezo wa kuwa kama wewe ila lengo langu nimpate ambaye hanipendi ila mwisho wa siku nifanye kitu kitakachomfanya anipendena sio umaarufu kama unavyodhani.."

Kutokana na mazungumzo hayo alioyakumbuka kutoka kwa Dick yalimfanya aanze kutafuta mwanamke hasiyempenda,ili afanye kitu kitakachomfanya mwanamke huyo ampende huku akichana na wanawake wote aliokuwa nao.

Je,nini kitaendelea..........Alhamisi Ijayo

Mwisho wa story  asante kwa kusoma mpaka mwisho wa story yetu karibu kwa maswali maoni na ushauri ikiwa una tangazo unahitaji tukutangazie Humu pia

*BADILI MAISHA*

*Ukitaka kufahamu njia ya kutengeneza Dora 100  mtandaoni kwa mtaji wa Sh:35,000 njoo inbox nikupe huo mchongo*Whatsapp 

kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇


Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();