Ticker

6/recent/ticker-posts

NILIKUPENDA SEHEMU YA 05

 


NILIKUPENDA SEHEMU YA 05 


ILIPOISHIA......

"Frank kwenye mapenzi kila mtu huonekani hafai ila siku nitakapomuoa yule atakayekuwa ananiaibisha,nitaonekana bora kuliko mwanaume yoyote yule,sema nini rafiki yangu mapenzi hayana mwenyewe.Pia Frank ukipendwa pendeka,ukipata nafasi ya kumpata anayekupenda basi hakikisha umuachi na akaenda.Jaribu kuzidisha mapenzi ya dhati ili uumfanye aliyekubali kuwa na wewe hasijute kwa maamuzi alioyafanya ya kukuchagua wewe.Pia Frank nahisi hawa wanawake ulionao hamna anayekupenda hata mmoja wote wanakupendea pesa na umaarufu ulionao nina uwezo wa kuwa kama wewe ila lengo langu nimpate ambaye hanipendi ila mwisho wa siku nifanye kitu kitakachomfanya anipende na sio umaarufu kama unavyodhani.."

Kutokana na mazungumzo hayo alioyakumbuka kutoka kwa Dick yalimfanya aanze kutafuta mwanamke hasiyempenda,ili afanye kitu kitakachomfanya mwanamke huyo ampende huku akichana na wanawake wote aliokuwa nao.

Je,nini kitaendelea..........

ENDELEA NAYO......

*****

"Mapenzi kichaa,mapenzi uchizi unachokikataa wewe,mwezio kinamnyima usingizi.Ni hatari hii nyimbo naikubaliga sana yani nisichokitaka mimi wengine kinawanyima usingizi,sema tatizo wanawake wengi ni wanafki na waongo.Sijui kama nitaoa mimi maana nahisi wanawake wote ni vile vile tu."

Dick alizungumza maneno hayo huku akiendelea na shughuli za kufanyia usafi katika chumba chake kwa pamoja na vyumba vingine ikiwemo,sebuleni jikoni pamoja na chooni.

Alijitahidi kufanya kazi kwa haraka kisha akaingia bafuni kuoga na kujiandaa ipasavyo.

Baada ya kumaliza kila kazi akaishika simu yake na kuikagua, hakuweza kukumbana na ujumbe wowote ule jambo lililokuwa likimchukiza na kufanya hasononeke sana.

Kama kawaida aliinua kitanda chake na kuchomoa kadi ya bank iliokuwa ndani ya wallet,alikuwa ameshazoea kutembea na wallet ila kwa siku hiyo akaona ni bora kubadiri muonekano aliokuwa nao.Hivyo akaiacha.

Wakati anataka kutoka nje alikumbuka amesahau fedha muhimu kwa ajili ya malipo ya usafiri na vinginevyo,hivyo akaamua kurudi ndani ya kuichukua wallet yake iliokuwa na kiasi cha shilingi Elfu hamsini akaona kuna umuhimu mkubwa wa kutembea na wallet na hata kama hataitumia pesa yote hiyo ila anaweza kukutana na tatizo ambalo linaweza kumgharimu pesa yote hiyo.

Aliipachika kadi ya bank ndani ya wallet kisha akaibana na kuiweka kwenye mfuko wa nyuma wa suruali yake ya kitaa aliokuwa ameivaa.Kwa muda alitoka nje na kufunga nyumba yake.Safari moja kwa moja hadi bank..Alikuwa hajazoea kupanda daladala kutokana na usumbufu aliokuwa haupendi ikiwemo na kuibiwa wallet mara kadhaa huku zikiwa zimesheheni kiasi cha shilingi laki moja na kuendelea na si chini ya kiasi hicho.Pia jambo jingine liliokuwa linamfanya achukie daladala na kutokana na kukaa karibu na watu waliokuwa wakinukia adhifari na ili ndio jambo kuu lililokuwa likimkera.

Aliita Tax kisha akapanda na kumuomba Dereva ampeleke NMB bank baada ya dakika chache alifika katika bank na kumlipa Dereva kiasi walichokubaliana, japo Dereva alimshushia mbali na bank lakini alipiga baadhi ya hatua na kufika bank.Alikuta foleni ya bank iliomchelewesha na kumfanya asubiri kwa muda kisha foleni ikaenda na kutokomea mpaka ikafika zamu yake.Aliingia ndani ya mashine ya kutoa fedha na kuamisha milioni tisa kwenda kwa Mzee matege kisha katika akaunti yake akabakiwa na shilingi  Milioni moja.

"Hallow Mzee Matege tayari kila kitu nadhani nitapita hapo kwako kukuletea lisiti ya bank..." Dick alimpigia Mzee matege baada ya kukamilisha kila kitu huku akiwa tayari yupo nje ya bank.

"Usiponikuta nyumbani unaweza kumpa hata mke wangu pia."

Tangia Dick ameanza kazi hizo ndizo fedha aliokuwa akitunza mpaka kufikia milioni kumi.Alikumbuka yapita miaka mitano sasa tangu aianze kazi hiyo ya utangazaji iliokuwa ikiimpa fedha chache sana na yote sababu alikuwa akijibana mpaka kufikia kiasi hicho.

Eneo alilokaa huwa hairuhusiwi kupaki kwa tax hata kipindi alivyokuwa anakuja mahali hapo alisimamia mbali na bank hiyo na kuanza kutembea kwa mguu mpaka bank ilipo,sehemu ya paking ilikuwa kwa magari ya watu wanaokuja katika bank hiyo ilikuwa hairuhusiwi kwa kuingia daladala au tax inayofanya biashara lakini kwa mtu binafsi aliokuwa akija katika bank hiyo kwa ajili ya lengo fulani ndio huwa anaruhusiwa.

Dick alitembea kwa mguu mpaka mahali aliposhushiwa kwa lengo la kutafuta tax nyingine akiwa pembezoni mwa barabara kabla hajafika kwenye kituo cha kupandia gari, alisikia kama mtu anamuita kwa mbali huku sauti ikijidhihirisha inatoka kwenye gari.

"We kaka???"

Dick aligeuka na kumtazama mwanadada aliokuwa akimuita huku sauti ikiwa inatoka kwenye gari..."

"Samahani kaka simamia pale kwenye kituo nikupe lift.."

Dick aliongeza mwendo na kwenda kwenye kituo cha kupandia gari kilipo huku kukiwa ni mahali aliposimamishiwa na Dereva Tax aliomleta.

Kulikuwa si mbali na alipokuwa hivyo aliongeza mwendo mpaka mahali hapo kisha akapanda gari ya huyo mwanadada aliokuwa akivutia kwa urembo wake.
"Ahsante kwa lift..."

"Bila shaka unaweza kunisaidia namba zako za simu."

"Aha Dada yangu mbona haraka hivyo,kwani we unaelekea wapi???"
"Mi nipo tu mizunguko wewe ndio unambie unaelekea wapi nikupeleke???"

"Nitakuwa nakuelekeza,but ni mbali kidogo."

"Sio mbaya mafuta yapo full tank,...."

Japo mwanadada huyo alikuwa akivutia lakini Dick alimuona kama kinyago kisiokuwa na maana kwake,hata wakati dada huyo aliokuwa akihusisha swala la namba kwa Dick,Dick alikuwa akipoteza mada na kwenda mada nyingine.

"Mi naitwa Annah.,we unaitwa nani....??"

"Naitwa Dick,mtangazaji wa Radio E .."

"Waooh kumbe ni wewe naomba basi namba zako na wewe mbona hivyo."

"Katia hapa kisha ushuke na hii barabara ya vumbi."

"Kumbe unaishi huku,nitakuwa nakuja.."

Dick alijisikia ashuke ndani ya gari hilo kwani uchangamfu wa Annah ulikuwa haumvutii hata kidogo,ila ni kwakuwa alikuwa akimsaidia katika usafiri hivyo aliendelea kwa kumsikiliza kila alichokuwa akizungumza.Kwa vichache sana alikuwa alimuunga mkono ili vingi alikuwa akikaa kimya.

Walivyofika kwa Mzee Matege kisha Dick akashuka na kuingia mpaka ndani,alikaa zaidi ya nusu sana ili tuu Annah aondoke zake.Akiwa ndani aliendelea kutazama movies ya kibongo iliokuwa ikihusiana na mapenzi na ilikuwa ikimugusa yeye kumpenda mtu hasiyekupenda.Dick baada ya kuwa amemkabidhi mke wa Mzee Matege lisiti za kuamisha fedha.Kisha akatoka nje huku huzuni ikiwa imemtawala na ni  baada ya kumkumbuka Loveness.Alitoka nje huku akiamini hawezi kumkuta Annah akiwa upande wa nje.

Kwa bahati nzuri au mbaya,Dick alimkuta Annah akiwa amepaki gari lake huku akiendelea kuzidisha tabasamu na hapa ni pale alipomuona Dick.

Dick alikuwa hana jinsi hivyo aliingia ndani ya gari la Annah.Annah alipandisha vyoo vya gari hiyo vilivyokuwa tinted kisha akaanza kunyonya lips za Dick.

Je,nini kitaendelea........Alhamisi Ijayo

Mwisho wa story  asante kwa kusoma mpaka mwisho wa story yetu karibu kwa maswali maoni na ushauri ikiwa una tangazo unahitaji tukutangazie Humu pia

*BADILI MAISHA*

*Ukitaka kufahamu njia ya kutengeneza Dora 100  mtandaoni kwa mtaji wa Sh:35,000 njoo inbox nikupe huo mchongo*Whatsapp 

kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇

Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();