Ticker

6/recent/ticker-posts

FAHAMU MAMBO 10 YA KUFANYA ILI NDOA YAKO IWE BORA!!

 



FAHAMU MAMBO 10 YA KUFANYA ILI NDOA YAKO IWE BORA!!

1.Lazima Ujue Kwamba Wewe Ni MKE Na Ni Wajibu Wako KUSHUKA NA KUMTII MUMEO

“Enyi Wake Watiini Waume  Kutaniko Linavyomtii Kristo Yesu”

2.Lazima Ujue Kwamba MUMEO NI KIONGOZI WAKO, Haijalishi Uko SMART KIASI GANI, Mume Anabaki Kuwa Mume… Hata Ukiwa Rais Wa Nchi, Ukirudi Nyumbani UNAKUWA MKE WA MTU; Hapo Elimu, Nafasi, Cheo, Umaarufu Havifanyi Kazi.

“Mume Ni Kichwa Cha Mkewe… Hata Kama Kichwa Hakina Akili Bado Ni Kichwa, Na Unadhirisha Usivyo Na Akili Zaidi Kwa Kukubali Kuolewa Na Mjinga… Umeshaolewa, Umegundua Ni Mjinga, Ishi Naye Kwa Akili Na Msaidie Kujua Nafasi Yake Na Muache Akae Kwenye Nafasi Yake”

3.Usiwe Mjinga Kiasi Cha Kutoka Nje Kwenda Kueleza Mapungufu Ya Mumeo; Midomo Ya Wanawake Wengi Imevunja Ndoa Zao… Hao Mashoga, Marafiki, Ndugu Zako Watakusikiliza Ila Hawatatatua Shida Zako Bali Watachangia Kuibomoa.

“Mwanamke Mpumbavu Huibomoa Nyumba Yake Kwa Mikono Yake Mwenyewe” 

4.Simama Kidete Na Umlinde Mumeo Anaposhambuliwa… Chako Ni Chako Hata Kama Kina Mapungufu… Mtetee Mumeo Mbele Za Watu Na mkosoe Mnapokuwa WAWILI CHUMBANI.

“Naye Abigaili Akamwangukia Daudi Akamfichia Mumewe Aibu Na Kumlinda Asiuawe”

5.Mumeo Akitoka Nje Ya Ndoa Kutafuta Nyumba Ndogo, Kabla Ya Kutafuta Pepo Aliyemwingia, Tafuta Mlango Ambao Huyo Pepo Ameutumia… Inawezekana Ulipokuwa Single Ulikuwa UNAJIPENDA, Unapiga PAMBA MPAKA BASI, Umeolewa UNAJIVALIA KIVYOVYOTE [shauri Yako]; Inawezekana Ulipokuwa Hujampata LUGHA YAKO ILIKUWA SUPER, Lakini Sasa Unajibu Unavyojisikia [Shauri Yako]; Inawezekana Ulipokuwa Hujavaa Pete ULIKUWA UNAWAPENDA NA KUWATHAMINI NDUGU NA WAZAZI WAKE, Lakini Ulipoingia Tu, Ndio Umeona KARAHA YA MAWIFI NA NDUGU WA MUME [shauri yako]… INAWEZEKANA NI KITANDANI [Biblia Inasema MKE HANA UMILIKI JUU YA MWILI WAKE ISIPOKUWA MUMEWE] Usisahau Hii Ni Ya Muhimu Sana, UKISEMA ANAKUCHOSHA “KWA KUKUJIA MARA KWA MARA” [Shauri Yako]!

“Mungu amefanya jambo jipya duniani ya kwamba MWANAMKE ATAMLINDA MWANAUME”

6.Usisahau Kwamba Ni Wajibu Wa Mke KUAMKA KABLA USIKU HAUJAISHA NA KUPIGA KAZI ZOTE ZA MUHIMU NDANI… Biblia Imesema Hili, MITHALI 31 [BIBLIA HAISEMI NI KAZI YA HOUSE GIRL; UKIMPA HOUSE GIRL AZIPIGE UMEMPA NAFASI YA KUWA MKE BADALA YAKE, MAANA NI KAZI ZA MKE MWEMA HIZI]

“Mke Mwema Huamka Kabla Usiku Haujaisha Ili Kuweka Sawa Mambo Ya Nyumbani Mwake Kwa Siku Inayoanza Baada Ya Usiku Huo”

7.Ni Lazima MKE AWE NA KITU CHA KUFANYA… Ukiwa tu GOLIKIPA, Hakuna VIUNGO Wala MABEKI Kukulinda UTAFUNGWA MAGOLI.

Mke Ambaye ANA AKILI NZURI Lazima AWE NA KITU CHA KUINGIZA KIPATO…Afanye Kazi Kwa Mikono Yake Mwenyewe, Na Kutunza Watu Wa Nyumbani Kwake, MITHALI 31 IKO WAZI KAMA UNATAKA NDOA YAKO ISIMAME, UKIKWEPA IMEKULA KWAKO!

“Mke Mwema Hufanya kazi kwa mikono yake mwenyewe, na kuwapa chakula watu wa nyumbani kwake”

8.Mke Mwenye Hekima ANAULINDA UHUSIANO NA MAMA MKWE [Hii Ni Zawadi Ya Pekee Kwa Mumeo], Moyo Wa mtoto Wa Kiume Humpenda Na Kumjali Mama, Usisahau Hii Itakusaidia, NI SILAHA MUHIMU YA VITA!

SOMA KITABU CHA RUTHU Utaona Ruthu Alivyocheza Kete Zake Vizuri Na Kuuteka Moyo Wa Mama Mkwe.

“Mke Mwenye Busara Huhakikisha Anauteka Moyo Wa Mumewe Kwa Kuwa Kipenzi Cha Mama Mkwe”

9.Mke Mwenye Busara Anajua Ya Kwamba Ni Jambo Moja Kuwa Mzazi [Mwanamke Aliyezaa] Na Ni Jambo Jingine Kuwa MAMA.

Kuzaa Ni Kuporomosha Kiumbe Baada Ya Miezi 9 Aliyoweka Mungu Lakini Kuwa Mama Kunategemea MALEZI SAHIHI NA BORA Yatakayoweka Msingi Mwema Na Bora Usiofutika Kwa Mwanao.

“Mke Mwema Humlea Mtoto Wake Katika Njia Impasayo Ambayo Hataiacha Hata Atakapokuwa Mzee”

10.Mke Mwenye Hekima HUUWEKA MOYO WAKE KWA MUNGU: Huku Ndiko Anakoeleza Mapungufu Yake, Mapungufu Ya Mume Wake, Na Kukabidhi Ndoa Yao KWENYE MIKONO SALAMA NA MAKINI YA MUNGU. Mungu Anaweza Kubadili Chochote Ambacho Wazazi, Washenga Au Washauri Wa Ndoa Hawawezi Kugeuza Au Kutatua.

“Mke Mwema Hufunga Na Kuomba Kwa Ajili Ya Mumewe, Ndoa Na Familia Yake… Ni Rafiki Wa Uwepo Wa Mungu”

Mwisho wa makala  asante kwa kusoma mpaka mwisho wa makala yetu karibu kwa maswali maoni na ushauri ikiwa una tangazo unahitaji tukutangazie Humu pia

*BADILI MAISHA*

*Ukitaka kufahamu njia ya kutengeneza Dora 100  mtandaoni kwa mtaji wa Sh:35,000 njoo inbox nikupe huo mchongo*Whatsapp 

kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇
Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();