NILIKUPENDA SEHEMU YA SITA 06
ILIPOISHIA..........
Walivyofika kwa Mzee Matege kisha Dick akashuka na kuingia mpaka ndani,alikaa zaidi ya nusu sana ili tuu Annah aondoke zake.Akiwa ndani aliendelea kutazama movies ya kibongo iliokuwa ikihusiana na mapenzi na ilikuwa ikimugusa yeye kumpenda mtu hasiyekupenda.Dick baada ya kuwa amemkabidhi mke wa Mzee Matege lisiti za kuamisha fedha.Kisha akatoka nje huku huzuni ikiwa imemtawala na ni baada ya kumkumbuka Loveness.Alitoka nje huku akiamini hawezi kumkuta Annah akiwa upande wa nje.
Kwa bahati nzuri au mbaya,Dick alimkuta Annah akiwa amepaki gari lake huku akiendelea kuzidisha tabasamu na hapa ni pale alipomuona Dick.
Dick alikuwa hana jinsi hivyo aliingia ndani ya gari la Annah.Annah alipandisha vyoo vya gari hiyo vilivyokuwa tinted kisha akaanza kunyonya lips za Dick.
Je,nini kitaendelea........
ENDELEA NAYO.............
*****
Frank alikuwa akifikiria pa kuanzia kwani hukujua ni msichana gani hasiyempenda,hivyo akili yake ilikuwa ikifikiria kwa ufasaha.
Alikaa huku mawazo yakiendelea kumkumba,simu yake ilikuwa ikiita kila wakati na wapigaji walikuwa ni wasichana aliowaacha,na namba zao alikuwa ameshafuta zote na kuwataarifu kuhusu swala la kuachana nao ila kuna baadhi yao alikuwa amekariri namba zao.Kitendo kilichofanya akagundua ni wao wanaomtafuta.Wengi walilia na hata wengine kumtishia Frank katika kutoa huai wao,ila yote Frank alikubaliana nao na kuwaambia kama wanahisi kifo ni kitu muhimu kwao,wajiondoe duniani.
Frank aliweza kuwablock wote waliokuwa wakimsumbua,japo walizidi kumtafuta kwa namba ngeni lakini alikuwa akifahamu ni wao na sio wengine.
Frank wakati anafikiria atampata wapi? anayempenda,akakumbuka kuna mwanadada anaojulikana kama Joyce yuko vizuri sana kwa kila sekta ila huwa anapenda sana kugombana naye na huwa anamuonyesha dharau hasa akipita mbele yake aidha kuachia kicheko cha kinafki au kumkejeli Frank kwa namna fulani hisiofahamika au hafa kumuimbia nyimbo zinazomgusa.
*INGIZA SH:250,000 KWA MTAJI WA SH:10,000*
*Fahamu jinsi ya kuingiza mpaka Tsh:250,000 Kwa mtaji wa Tsh:10,000 kupitia smartphone njoo inbox nikupe huo mchongo*Whatsapp
Hivyo basi Frank alisimama na kutoka nje ya nyumba yake na kwenda hadi mahali anapoishi Joyce,na kumkuta yupo kibalazani huku akiendelea kula machungwa na chumvi aliokuwa ameiweka katika kisahani chake.Ujio wa Frank mahali pale ulimfanya Joyce kutema mate chini kisha akaanza kuzungumza maneno ya kejeli.
"We Frank utanifanya nisipate vitamini D."
"Aha Joyce,kweli vitamini D saa tano hii sijui saa sita."
"Hivi we umesoma shule gani kipi husichoelewa,pisha mbele yangu."
"Basi sawa,ila Joyce nina machache ya kuzungumza na wewe,naomba unisikilize japo kwa dakika tano tu ikibidi hata dakika tatu kama hutojali,unisikilize kile nachohitaji kuzungumza nawe.Nakuomba niko chini ya miguu yako."
"Dakika tatu zikiisha uchafue,simama acha kujichafua.."
"Joyce natambua unanidharau natambua sina umuhimu kwako,natambua we si kama wale wanaonipendea pesa wanaonipendea utangazaji nilionao,ni aibu sana mtu akinikuta mimi Frank nikiwa katika hali ya namna hii tena nikiendelea kunyenyekea mbele yako.Ila amini hamna mwanamke alioteka hisia zangu kama wewe.Nitafanya kila unachotaka ili tu kukupa tabasamu na furaha.Kila mwanaume ana sheria zake mimi nina sheria zangu za kukupenda wewe.Joyce nahitaji kukuonyesha ni jinsi gani nakupenda..."
Joyce bila ya kuzungumza chochote macho yake yalianza kulegea na kujikuta anashindwa kuzuia hisia zake mbele ya Frank....Joyce aliingia ndani na kumuacha Frank akiwa upande wa nje.
Frank aliamua kurudi nyumbani kwake huku moyo wake ukijaa gumzo juu ya mwanadada Joyce.Maswali mengi alikuwa akijiuliza juu ya Joyce.Je,atakuwa amemkubali....Au itakuwa amemdharau Frank.
Frank alihisi anaumiza kichwa chake kwa maswali aliokuwa akijiuliza juu ya Joyce,ilikuwa ni kawaida kwa kila Jumapiili Dick na Frank huwa wanatoka nyakati za usiku na kwenda kwenye Club maarufu kwa ajili ya kunywa vinywani pamoja na kusaka mabinti.Hasa hasa hii alikuwa anaifanya Frank maana Dick alikuwa ni kama msindikizaji na alikuwa hana tabia ya kumtongoza mtu hasiyemjua.
"Mambo Frank......".
Ujumbe uliingia katika simu ya Frank japo ulimshtua lakini baadaye aliupuzia na kungudua mtumaji atakuwa ni moja kati ya fans wake.
Kabla hajakaa vizuri ujumbe wa pili ukaingia katika simu yake huku ukiambatana na Jina la mtumaji.
"Mi,Joyce namba zako nilikuwa nazo na nilizikopi pale ulipozitaja kwenye kipindi chako,ila nachohitaji kukuambia Frank....hebu fanya kitu kitakachoonyesha unanipenda....na kama utashindwa basi....usiwe unanitumia sms kwanza mpaka pale utakapofanya kitu cha kunifurahisha mimi na cha kunifanya niamini unanipenda."
Tabasamu la Frank lilikuwa hafifu baada ya kuusoma ujumbe huo na kuumaliza.Alikuwa anataka kumjibu Joyce ila nafsi yake ilimzuia kutokana na Joyce kukataa kutumiwa ujumbe kutoka kwa Frank.
Frank alikuwa akifikiria juu ya anachotakiwa kufanya kwa Joyce lakini jibu alikosa alihisi kama atamkosa Joyce na hawezi kumpata kamwe.Kidogo alianza kupata njia za kumpata Joyce na kuhaidi kumshirikisha Dick katika swala hilo.
*****
"Siwezi kuwa na Dick kabisa siwezi japo ni chanzo cha tabasamu la mama lilipo.Japo Dick akiwa mme wangu tunaendana sana.Ila mbona mapenzi ni kawaida kumuumiza kila mtu na kuachana na mtu huwa ni matokeo ya mapenzi.Kweli Dick kwa jinsi anavyonipenda anaweza kuruhusu mwanamke yoyote kuvuka mipaka.Ingekuwa Dick anania mbaya na mimi siku alioikata picha yangu na kuwa ya kingono,mpaka mimi kwenda nyumbani kwake angeweza kufanya lolote mbaya lakini hakufanya hivyo.Ameweza kumuandalia mama yangu zawadi bora kwa ajili kumtakia kheri ya siku yake ya kuzaliwa.Katika ili nahitaji muda wa kufikiria ili niwe na Dick sitaki kufanya maamuzi yasiokuwa sahii,nahitaji kutulia kwa muda."
*INGIZA SH:250,000 KWA MTAJI WA SH:10,000*
*Fahamu jinsi ya kuingiza mpaka Tsh:250,000 Kwa mtaji wa Tsh:10,000 kupitia smartphone njoo inbox nikupe huo mchongo*Whatsapp
Loveness alianza kupatwa na mwazo juu ya Dick.Hisia kali za kimapenzi zilizidi kumuijia juu ya Dick.Alitamani sana kuwa naye japo kuna kitu hasichokifahamu kilikuwa kikimzuia,na kuna wakati mwingine alitamani hata kumpigia na kumuambia anampenda ila pia nafsi ilikuwa ikimzuia.
Alikumbuka kila alipokuwa akiomba ushauri kwa rafiki yake Rehema,Rehema alikuwa akimpa jibu ambalo lilikuwa na wasi wasi na lilikuwa ni chanzo cha kumfanya ampende Dick.."Loveness kama wewe umuhitaji Dick niachie."
Jibu la Rehemu ndio liliokuwa likimfanya Loveness ahitaji kumuambia Dick anampenda.Pia kuna wakati hisia kwa Dick zilikuwa zikitokomea kabisa na kuhisi huenda ni mawazo ya kawaida na yatakwisha.
Kwa hali halisi alikuwa hajielewi afanye lipi kwani kila alichokuwa akifikiria juu ya Dick kilikuwa kiko sahihi.
"Mama nashida ya kuzungumza na wewe....."
Loveness alizungumza na mama yake huku akionekana kutandwa na mawazo,huku muda kidogo ukiwa umepita tangu azungumze na mama yake kuhusu swala la Dick.
"Niambie mwanangu......"
"Mama unapenda sana niolewe na Dick???"
"Mwanangu nampenda sana Dick,natamani sana uje uolewe naye, mama yako kwa uzee wangu huu natamani sana kupata mjukuuu kutoka kwao tena natamani sana baba wa huyo mjuu awe Dick."
"Mama nipe muda wa kulitafakari ili.Unamkumbuka Isaya alivyoniumiza na kunidhalilisha sana...."
"Nakumbuka sana mwanangu pia naomba ukumbuke Isaya sikumuafiki kwanza alikuwa muhuni,sijui hata umlipendea nini.Mimi nina huakika asilimia zote Dick hawezi kukuamiza."
"Mama kweli baba atakubali katika ili,unakumbuka baada ya Isaya kunidhalilisha,baba alikataa nisiweze kuolewa na yoyote mpaka anitafutie yeye wa kuolewa naye.Mwanangu sasa mimi na baba yako si ni mtu yule yule.We jipange mfikirie Dick kiundani acha kwanza kumtafuta.Tuliza moyo wako jenga mambo yako naamini Dick atakuwa mume bora kwako."
"Sawa mama ngoja nikapumzike then baadaye nitamka nikupikie.baba! anarudi lini kutokana South Africa."
"Ndege aliokuwa ameikatiaTicket ipo kwenye marekebisho,nadhani ikishakuwa tayari atakuja...."
"Sawa mi ngoja nikapumzike.....mama.."
"Sawa mwanangu....."
Mwisho wa story asante kwa kusoma mpaka mwisho wa story yetu karibu kwa maswali maoni na ushauri ikiwa una tangazo unahitaji tukutangazie Humu pia
*INGIZA SH:250,000 KWA MTAJI WA SH:10,000*
*Fahamu jinsi ya kuingiza mpaka Tsh:250,000 Kwa mtaji wa Tsh:10,000 kupitia smartphone njoo inbox nikupe huo mchongo*Whatsapp
kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇
KWA HABARI ZA BISHARA NA BIDHAA MPYA TAZAMA MAUZO TV |
0 Maoni