TUNDA LA MKWAKWANI
Sehemu ya 2
Na Edson Tirani
___
Kweli nilijiona mwenye bahati kutokana na ujumbe alionitumia Aisha nami nikamrudishia wa kwangu, Najua unanipenda na pia naomba utambue kwamba moyo wangu ni tunda na mchumaji na mlaji ni wewe hakuna atakaeipata bahati kama hii zaidi yako wewe na pia sipo tayari kukukosa najua unanitumainia na kuniaminia, naju unashauku ya kuniona lakini usihofu najua mungu atatukutanisha mimi na wewe, upendo wako ni wa thamani zaidi ya almasi na karama yako ni zaidi ya ua la uwaridi thamani yako ni ya juu sana situmai kukukosa we ndiye ndoto yangu na pia ni hamasa yangu i love you Aisha,nikamtumia,na yeye akarudisha nyingine, Nina furaha ninapoona unanihifadhi moyoni mwako na wewe ndiye mvua yangu ya kiangazi najua mapenzi ni kupanda ngazi najua tutapanda salama na kufika huko pasipo kuyumbishwa na yeyote yule i love you too My Mrisho heart and soul front of us, (nakupenda zaidi Mrisho wangu,moyo na nafsi mbele yetu )akanitumia, kwakweli kidume nilijiona bonge ya mjanja na bahati hii sikutaka kuichezea hata kidogo mwanaume.
Najiandaa kuja huko kwenu mkwakwani na nimekuandalia zawadi nyingi sana Aisha najua hauta amini but ukweli ndiyo huo siwezi kukutajia na utajionea wewe mwenyewe,uniandalie Tunda la Mkwakwani nije nijumuike nawe kulila najua unanisubiri kwa hamu kubwa sana lakini usikate tamaa moyo wangu umekujaza wewe na nakuhakikishia nataka ufurahie penzi letu na amani kwa pamoja, yalikuwa ni maneno yangu mm Mrisho, yeye akajibu,kuhusu hilo usijali maisha ni wawili ktk nyumba na huwa ni Mke na Mume hapo utaona mafanikio ya kweli karibu sana Mrisho nakependa sana sina mwingine, tuliongea mengi sana hadi tukaagana na kukata simu,kijana mimi nilifura kwa furaha niliona mungu kanishushia dhahabu yenye thamani hata wa marekani walishindwa kuilipia, niliandaa Smartphone kwaajili ya Aisha nguo sikununua nilijua tutanunua hukohuko yani nilikuwa na pilika zisizo za kifani nilijipa misifa balaa nilinyoa nywele mnyoo wa hekima na nikajihakikishia kuwa smart sana kila mtu akiniona alikuwa akinong'ona wengine wakasema oy unampango wa kusafir nn aliniuliza jamaa mmoja ambae alikuwa mfanya biashara mwenzangu, nikamjibu yaa naenda mkwakwani Tanga, ahaa kuna shemela nin alchombeza,aha naenda matembezini tuu nilimjibu, sawa safari njema akanitakia na akaondoka,
Hallo Aisha mm ni wako Mrisho nakuarifu kama nakuja wiki ijayo huko tanga mkwakwani, ilikuwa mm nikimuambia aisha kupitia simu ya mkononi,sawa mimi nakusubiria wangu nakuandalia tunda la mkwakwani hani alijibu Aisha, tuliongea mendi siku hiyo na tukamaliza na kukata simu zetu, hatiae siku ilifika na mm nilijipanga kuenda Mkwakwani tanga, Wa mkwakwani wa mkwakwani wa mkwakwani,ilikuwa ni sauti ya mpiga debe nami nikajisogeza, karibu muheshimiwa alinikaribisha mpigadebe wa basi liitwala Mohamed Trans,aliniita bosi sababu nilivali v t_shirt nyeupe nikapiga koti la suti la blue pamoja na suruali ys blue kama koti lenyewe nikatinga miwani ya kuzuia mionzi ya jua kama anold shwazniga na brifcase mkononi huku nikipiga kiatu mkuki moyoni cha blue nacho, watu wote walikuwa wakiniangalia mm tu had wakahisi kama mm ni mpelelezi, hatimae watu walipanda wote tulisafir siku hiyo mpaka katika stendi ya mkwakwani tanga na kushuka mm nilimpigia Aisha simu aje tuonane.
Itaendelea Alhamisi ijayo
Share kwa mwingine.
Mwisho wa makala asante kwa kusoma mpaka mwisho wa somo letu karibu kwa maswali maoni na ushauri ikiwa una tangazo unahitaji tukutangazie Humu pia
*Fahamu jinsi ya kuwa milionea Kwa mtaji wa Tsh:200,000 kupitia smartphone njoo Inbox niku unganishe
KWA HABARI ZA BISHARA NA BIDHAA MPYA TAZAMA MAUZO TV |
Makala nyingine
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Video Jifunze haya mwanaume Hawezi kuchomoka
Sababu kubwa inayo sababisha mwanaume Kupunguza mapenzi kwako
Fursa ya kujiajiri kupitia blog
Tambua sababu zinazo sababisha wanawake wengi kuachwa na waume zao
0 Maoni