Moja ya sababu kubwa ya ndoa nyingi kuvunjika siku hizi ni mali. Watu wengi wakiingia kwenye ndoa badala ya kuwaza namna ya kuishi milele kwa amani wanawaza kitu cha kufanya kama wakiachana, namna ya kugawana mali. Hii hupelekea kila kitu kuharibika kwa kila mmoja kuhangaika kuchuma chakwake badala ya kufanya pamoja.
Raha ya ndoa ni kusaidiana, kufanya kila kitu kwa pamoja, kushirikishana. Mara nyingi wanaume ndiyo huamua hivi, mara nyingi wanawake huenda kwa upepo,kwamba akiona kuwa mume anamshirikisha katika mambo yake, wanafanya mambo kwa pamoja basi naye huweka kila kitu mezani.
Lakini kuna wanawake wabinafsi, yuko kwenye dnoa nzuri, mume anamshirikisha kila kitu chake, nimuwaza, lakini utasikia kajikusanya kanunua kakiwanja kake bila kumuambia mume. Mwanaume hamkatazi kutuma pesa kwao, tena pengine wanakaa na kupanga kuwa tutume kiasi gani lakini anafanya kimya kimya na kutuma huko bila kumuambia mume.
Mwanamke unachukua mikopo, hata kama utalipa wewe lakini humuambii mume wako, mambo yakikuchachia basi ndiyo unaanza kumtafuta mume na kumuomba kukusaidia kulipa. Kuweka dhambana nyumba au kiwanja? Aina hii ya ubinafsi inavunja ndoa nyingi, mwanaume akiamua kukuamini hembu mlipe hiyo imani.
Fanyeni mambo ya maendeleo kwa pamoja, sisemi uwe wa kupelekwa tu, hapana, kama mnafanya vitu vya kudumu na wewe unachangia basi muandike majina yenu wote. Kama nyumba ya kwanza ilikua na jina lake, yapili hata iwe na majina yenu au yako. Hembu kama ndoa yako ni nzuri acha kuwaza sana kuhusu kuachana, najua kuna wakati kutokana na tabia zake unaogopa.
Lakini hakuna haja ya kujibana na kujenga kimya kimya bila kumuambia mume wako wakati yeye anakuambia kila kitu. Najua unawaza kama nayeye ananificha vingine? Sijui, inawezekana anakuficha lakini huna haja ya kumficha mpaka pale utakapoona anakuficha na hata baada ya kuongea naye akagoma kukushirikisha kabisa. Badilika usivunje ndoa yako kwa vitu ambavyo vinaepukika.
Je wewe unasemaje?
0 Maoni