Bonyeza hapa Download App ya MAHABA |
MONALISA
SEHEMU YA: 01
"Happy birthday to you!" Happy birthday birthday to you! " hizo Zilikuwa ni sauti zilizokuwa zikimtakia maisha marefu binti mmoja mrembo sana aitwae Monalisa ambaye kwa siku hii ya Leo ilikuwa ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa! Monalisa alikuwa akisheherekea kutimiza miaka 23 ya kuwepo kwake duniani, hivyo wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali waliweza kufika kwa usiku huu wa saa 4:36 katika jumba LA kifahari LA Mr Brown ambaye ndie baba yake na Monalisa! Wageni waalikwa waliendelea kuburudika kwa vinywaji pamoja na vyakula vya kusaza (Kubakisha) huku muziki laini ukiwapa raha! Kwa sasa lilikuwa linasubiriwa tukio muhimu ambalo sio lingine ni ukataji wa keki ambayo Monalisa atakata keki hiyo na kuwalisha
wazazi wake pamoja na ndugu jamaa wa karibu! Monalisa alikuwa ni mtoto wa pekee katika familia ya Mr Brown na mkewe Bi Sophia ambaye ndie mama yake mzazi na Monalisa hawakuwa na mtoto mwingine tena, hivyo walimpenda sana binti yao hiyo! Pamoja na kupendwa sana na wazazi wake lakini Monalisa alikuwa haishi nao alikuwa akiishi katika jumba lingine la kifahari lililokuwa maeneo ya mbezi beach alilopewa na baba yake Mr Brown ambapo aliwekewa na mlinzi wa kumlinda nyumbani hapo pamoja na wafanya kazi wa ndani pia wawili wa kumtunzia mazingira katika jumba hilo! Pia Monalisa alikuwa anaishi na rafiki yake wa karibu sana aitwae Suzzy aliyekuwa akimpa kampani ili asijisikie unyonge, kwa usiku huu pia alikuwa yupo na best yake Suzzy katika sherehe hii hapa nyumbani kwao mikocheni kwa Mr Brown! Sherehe ya birthday ya Monalisa ikawa inaendelea!
Katika usiku huohuo maeneo ya manzese midizini katika banda moja moja LA mama lishe anaonekana mwanaume mmoja aliyekuwa na muonekano wa kifukara akiwa amejilaza kwenye mabenchi yaliyokuwa ndani ya banda hilo LA mama lishe huku akionekana ni mwingi wa mawazo na wakati mwingine pia alikuwa akilia machozi, "Nasema haiwezekani ni lazima niipate haki yangu, sikubali haki yangu ipotee hivihivi!" alisema mwanaume yule fukara kwa sauti iliyojaa uchungu mwingi ndani yake huku akijifuta machozi yaliyokuwa yanamtoka! Kwa usiku huu ndani ya banda hili LA mama lishe hakukuwa na pilikapilika za wateja licha ya asubuhi na mchana kuwa banda hili linafanya huduma ya kuuza chakula, lakini kwa wakati huu wa usiku lilimfaa fukara huyu aliyekuwa amekosa sehemu ya kulala na kuja kujihifadhi kwenye banda hili huku sauti za mbu zikimliwaza na wakati mwingine wakimuuma mwilini mwake na kupelekea kila wakati kujipiga katika mwili wake ili
kuwafukuza mbu hao waliokuwa na hasira na damu yake! Mwanaume huyo fukara akaingiza mkono wake kwenye mfuko wa koti lake ambalo lilikuwa ni kuukuu pamoja na chafu kupindukia kisha akatoa picha tatu zilizokuwa kwenye bahasha ndogo na kuziangalia picha hizo, machozi yalizidi kumtoka fukara huyu Mara baada ya kuziangalia picha hizo! "Nasema sikubali, lazima nipate haki yangu!" alisema fukara yule kwa uchungu na kisha kuzirudisha picha zile kwenye lile koti lake lililokuwa pia limechanika, sasa akawa anajaribu kutafuta usingizi ambao nao ulionekana kumkwepa kwa sababu ya mawazo aliyokuwa nayo akajikunyata kwenye Yale mabenchi bandani pale huku kundi kubwa LA mbu likimuandama na kumchachafya fukara huyu!
Tunarudi kule kwa akina Monalisa sasa! Ile sherehe yao sasa hatimaye ilikuwa imefika ukingoni kwenye majira ya 6:30 usiku Mara baada ya Monalisa kukata keki na kuwalisha wazazi wake pamoja na wageni waliohudhuria birthday yake, kwa sasa wageni waalikwa walionekana wakiingia kwenye magari yao na kuanza kurudi majumbani kwao! Monalisa na rafiki yake Suzzy nao wakawa wanapakia zawadi alizopewa Monalisa na wageni kwenye gari ili apate kurudi kule nyumbani kwake mbezi beach, baada ya hapo Monalisa na best yake Suzzy wakaingia kwenye gari na safari ya kwenda nyumbani kwake ikaanza wazazi wake wakamtaka kuwa makini barabarani wakati wa kuendesha gari! Basi wakaagana pale na kutakiana usiku mwema kisha Monalisa na Suzzy wakaondoka! Baada ya mwendo wa nusu saa hatimaye Monalisa alisimamisha gari yake nje ya geti kubwa LA pale nyumbani kwake ambapo mlinzi wake akamfungulia geti na Monalisa akaiingiza gari yake ndani ya (fensi) uzio baada ya hapo Monalisa na Suzzy wakashuka kwenye gari na zile zawadi na moja kwa moja wakaingia ndani kwenda kulala, kwa kuwa walikuwa na uchovu wa ile sherehe awakuchelewa kupata usingizi! Asubuhi ya siku ya Pili ikafika! Monalisa na Suzzy wakaamka na kujiandaa ili kwenda kwenye biashara zao maeneo ya mlimani city ambapo Monalisa alikuwa na maduka mawili makubwa aliyokuwa amefunguliwa na baba yake Mr Brown waliyokuwa wanauza nguo za kike na za kiume pamoja na viatu, baada ya kumaliza kujiandaa Monalisa na Suzzy wakaingia kwenye gari na mlinzi akafungua geti kubwa Monalisa akatoa gari yake nje! Baada ya Monalisa kuitoa gari yake nje aliweza kumuona mwanaume mmoja fukara akiwa amesimama kando ya geti LA pale nyumbani kwake,
Monalisa akampuuza kwa kudhani labda anaweza kuwa ni mwendawazimu MTU yule hivyo akaiondoa gari yake kwa mwendo wa kasi sana! Yule MTU fukara akaiangalia ile gari ya Monalisa iliyokuwa ikiyoyoma machoni kwake, kisha na yeye kwa mwendo wa kujikongoja akafuata muelekeo wa barabara kule ilipoelekea gari ya Monalisa! Kumbe huyu MTU fukara ndie yule aliyekuwa amelala kule kwenye lile banda LA mama lishe!! Sijui kafuata nini nyumbani kwa Monalisa?? Tufuatilie story hii tutajua tu!,, ITAENDELEA SEHEMU YA 02 AHSANTE KWA KUISOMA
👯MONALISA👯
SEHEMU YA: 👉02👈
Baada ya Monalisa kumpuuza yule MTU fukara aliyekuwa amesimama pale nje ya geti la nyumbani kwake Monalisa akiwa na rafiki yake Suzzy ndani ya gari aliiondoa ile gari yake kwa kasi sana na kumuacha yule MTU fukara akiishuhudia kwa macho ile gari ya Monalisa ikiyoyoma machoni kwake! Yule MTU fukara naye kwa mwendo wake wa kujikongoja akawa anafuata uelekeo wa barabara kule ilipoelekea gari ya Monalisa? Baada ya muda hatimaye Monalisa na rafiki yake Suzzy wakawa wamefika kwenye biashara yao maeneo Yale ya mlimani city na kufungua maduka yao na kuanza kuonyeshana baadhi ya picha zilizokuwa kwenye simu zao za ile birthday ya Monalisa iliyokuwa imefanyika usiku wa Jana yake, Monalisa alisahau kabisa kama asubuhi hii ya Leo alimuona yule MTU fukara amesimama kule getini kwake na kumdharau kwa kudhani labda ni mwendawazimu! Kwa muda huu Monalisa na Suzzy walionekana kufurahi hapa kwenye biashara yao na zile picha zilizokuwa kwenye simu zao!
Upande wa Pili anaonekana Mr Brown ambaye ndie baba yake na Monalisa akiwa yupo ofisini kwake akiendelea na majukumu ya kazi, Mara simu yake ya mkononi ikawa inaita! Mr Brown akaiangalia hiyo namba inayompigia kwenye simu yake akagundua kuwa ni ngeni kabisa "Nani huyu anaenipigia simu?" Mr Brown alijiuliza yeye mwenyewe na kuamua kuipokea ile simu! "Aloo Mr Brown naongea hapa, sijui wewe nani mwenzangu?" hivyo ndio alivyoanza Mr Brown Mara baada ya kuipokea ile simu! "Najua kama Mimi hapo naongea na Mr Brown, kuhusu Mimi usihofu utanijua!" Ilijibu sauti kavu na nzito kutoka upande wa Pili wa simu! "Ni vizuri kwanza ukajitambulisha ili
nikufahamu" Mr Brown alisema kwa wasiwasi! Kikasikika kicheko kikubwa cha dharau kutoka kwa yule MTU aliyekuwa anaongea na simu upande wa Pili kisha Baada ya kucheka yule MTU akasema: "Najua unanifahamu vizuri sana, lakini unajitoa ufahamu na kujifanya haunijui!" alisema yule MTU! "Mpumbavu wewe, hebu sema shida yako sina muda wa kusikiliza hizo ngonjera zako eboo!" Mr Brown alifoka akionekana kuchukia sana! "Sawa niite Mimi mpumbavu, lakini kumbuka kuwa haki yangu ipo kwako na sasa ndio muda wangu wa kuidai umefika!" alisema yule MTU na yeye kwa hasira! "Haki gani unayoidai kutoka kwangu mbwa wewe?" Mr Brown aliuliza kwa jazba!
"Niite mbwa niite mpumbavu, lakini muda wa kuipata haki yangu ndio umefika na ni lazima utanipa tu!" Alisema yule MTU kwa hasira na kisha akakata simu yake, na kumuacha Mr Brown akiwa ameduwaa! "Ni mshenzi gani huyu anaetaka kuichezea akili yangu?" Mr Brown alijiuliza yeye mwenyewe huku kijasho chembamba kikimtiririka kwenye paji lake la uso licha ya ofisini kwake kuwepo na A/C (Kiyoyozi) akajaribu kupiga tena ile namba lakini simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa mwishowe ikakatika, Mr Brown akuchoka akapiga tena simu safari hii akakuta ndio haipatikani kabisa! Mr Brown alichanganyikiwa sana hakumjua yule MTU ni nani na hiyo anayodaiwa na huyo MTU pia akuijua! Mr Brown alizama kwenye dimbwi LA mawazo pale ofisini kwake akimfikiria yule MTU!
Kwa upande wa akina Monalisa na Suzzy jioni ilipofika waliweza kufunga maduka yao na Baada ya kumaliza kufunga sasa wakawa wanaelekea sehemu ya parking (Maegesho) pale ambapo Monalisa aliipaki gari yake muda wa asubuhi walipokuja hapa mlimani city, wakiwa wamebakisha hatua chache kufika pale ilipokuwa hiyo gari Monalisa alishtuka Mara baada ya kumuona yule MTU fukara ambaye asubuhi hii ya Leo alimuona akiwa amesimama nje ya geti kule nyumbani kwake na sasa alipatwa na mshtuko na kushangaa kumuona tena huyu MTU maeneo ya hapa tena akiwa ameigemea ile gari ya Monalisa kwa sehemu ya mbele! Monalisa kwanza akasita kwenda na kumuonyesha rafiki yake Suzzy ambaye alikuwa bize na simu yake ya mkononi akiperuzi mtandao wa WhatsAp "Suzzy hebu angalia kwanza pale kwenye gari" Monalisa alimuonyesha Suzzy yule MTU! Ikabidi Suzzy sasa aache kufanya kile alichokuwa anafanya kwenye simu yake na kuangalia kule aliopoelekezwa na Monalisa, Suzzy baada ya kuangalia na yeye akaweza kumuona Yule MTU fukara akiwa yupo pale kwenye gari kama vile anamsubiri mtu! "Si ni kichaa yule, sasa Monalisa unashangaa nini?" Suzzy aliuliza kwa mshangao "Hapana Suzzy kinachonishangaza yule MTU asubuhi nilimuona kule nyumbani
akiwa nje ya geti, na sasa nashangaa kumuona tena hapa ameegemea gari yangu!" alisema Monalisa! Sasa ikabidi wasimame na kuanza kufikiria namna ya kwenda pale ilipopaki ile gari maana yule MTU tayari aliwapa hofu! Bahati nzuri ni wao ndio walikuwa wa kwanza kumuona Yule MTU! Mara ghafla yule MTU fukara akageuka na kuwaona Monalisa na Suzzy pale walipokuwa wamesimama, yule MTU akawakakazia macho! Monalisa na Suzzy walibaki wanatetemeka! Sasa yule MTU akatoka pale kwenye gari na kuanza kuwafuata mabinti hawa waliokuwa wanatetemeka kwa hofu!!,, ITAENDELEA SEHEMU YA 03
👯MONALISA👯
SEHEMU YA: 👉03👈
Baada ya yule MTU fukara aliyekuwa ameigemea ile gari ya Monalisa kuwaona wakina Monalisa na rafiki yake Suzzy pale walipokuwa wamesimama, sasa yule MTU akawa anatoka pale kwenye gari na kuwafuata mabinti hawa waliokuwa wanatetemeka kwa hofu! Monalisa na Suzzy walitamani kukimbia mbio Mara baada ya kumuona Yule MTU waliyekuwa wanamuhofia kuwa anawasogelea, lakini kabla hawajatimua mbio Mara ghafla akatokea mlinzi nyuma yao! Kumbe alikuwa ni mlinzi wa hapa kwenye eneo LA parking (Maegesho) ya magari ndie aliyekuwa amekuja! "Vipi Madame kuna tatizo hapa?" yule mlinzi alimuuliza Monalisa! Monalisa alibaki kimya akawa anaangaliana na Suzzy kama vile wanategeana nani aseme hicho
wanachokiogopa! "Kwa sababu nimewaona muda mrefu mmesimama hapa, nikaona ngoja nije pengine kuna tatizo labda!" bado yule mlinzi aliendelea kuongea! Wakati yule mlinzi akiendelea kuwasemesha Monalisa na Suzzy pale, sasa yule MTU fukara akawa amefika karibu kabisa na pale waliposimama! Yule MTU bila hata ya kusema kitu chochote akawapita na kuendelea na safari yake huku nyuma akiwaachia harufu mbaya ya uvundo iliotokana na nguo zake kuwa chafu sana, lakini wakati alipokuwa anawapita yule MTU alimuangalia Monalisa kwa macho makali sana mpaka Monalisa akaogopa! Baada ya yule MTU kuwa tayari amewapita, yule mlinzi akaanza kucheka! "Aaahaaah kumbe mlikuwa mnamuogopa yule kichaa?" Mlinzi aliuliza! Monalisa na Suzzy haraka wakamuuliza mlinzi! "Kwani unamjua yule MTU?" Mlinzi
akatabasamu kisha akajibu! "Hapana simjui kabisa, lakini kwa ule muonekano wake jinsi alivyo ni lazima tu atakuwa ni kichaa!" Monalisa na Suzzy wakashusha pumzi ndefu Baada ya kusikia hivyo, Monalisa akageuka nyuma na kumuangalia yule MTU fukara ambaye kwa wakati huu alikuwa anatpkomea kabisa kwenye eneo lile! "Huyu MTU Mimi nahisi atakuwa sio chizi, lazima kuna kitu kitakuwa kinamsumbua" Monalisa alijisemea yeye mwenyewe moyoni huku akimuangalia fukara akiingia mitini! "Hey Monalisa hebu tuondoke zetu" Suzzy alimshtua Monalisa, "Ok poa twende zetu" alisema Monalisa na kuanza kuelekea pale kwenye gari yake! "Samahani Madame kabla aujaondoka nilikuwa na shida kidogo!" yule mlinzi alimsimamisha Monalisa! Monalisa akasimama na kumuuliza yule mlinzi, "Bila samahani ulikuwa na shida gani?" Mlinzi kwanza akachekacheka kwa aibu halafu akasema: "Madame nilikuwa na shida, tangu asubuhi sijakula msosi kwahiyo kama una chochote naomba unisaidie!" Mlinzi alimpiga mzinga Monalisa! Monalisa akafungua pochi yake na kutoa noti ya shilingi elfu kumi (10000) na kumpa yule mlinzi, ambaye alimshukuru sana Monalisa! Baada ya hapo Monalisa akaingia kwenye gari yake akiwa na Suzzy akawasha gari na kuiondoa huku mawazo kuhusu yule yakimsumbua, na kujiuliza kuwa yule MTU ni nani na kwanini alikuwa amekaa pale kwenye gari yake tu? Na pia muda ule aliokuwa amewapita pale kwanini alimkazia sana macho yeye? Monalisa hakupata jibu! Safari ya kurudi nyumbani kwake mbezi beach ikaendelea!
Kwenye majira ya usiku mikocheni nyumbani kwa Mr Brown ambaye ndie baba yake na Monalisa, Mr Brown alijawa sana na mawazo kichwani mwake alikuwa akimfikiria yule MTU asiejulikana ambaye alimpigia simu na kumuambia kuwa anadai haki yake! Mr Brown hakujua MTU huyo ni haki gani aliyokuwa anaidai, akajaribu kuvuta kumbukumbu kama anadaiwa na MTU jibu ni hapana! Zaidi ni yeye ndie aliyekuwa anawadai watu, sasa huyu MTU anamdai nini? Hilo ndio swali lililokuwa likimtesa Mr Brown baba yake na Monalisa! Hata mkewe Bi Sophia mama yake mzazi Monalisa aligundua kuwa mume wake yupo kwenye mawazo! "Vipi Mme wangu, Leo mbona kama Nakuona haupo Sawa kulikoni?" Bi Sophia alimuuliza mumewe! Mr Brown akashusha pumzi ndefu halafu akamsimulia mkewe nini kinachosababisha yeye awe na mawazo, Bi Sophia naye alichoka kabisa kusikia hivyo! "Mmh kwahiyo mme wangu, wewe aumfahamu kabisa huyo MTU?" Bi Sophia aliuliza! "Ni kweli kabisa mke wangu Mimi simjui huyo MTU" Mr Brown alijibu! Wakati wakiendelea kutafakari Mara ujumbe mfupi (SMS) ukaingia kwenye simu ya Mr Brown akachukua simu yake na kuusoma ujumbe huo uliandikwa hivi: "NAKUTAKIA USIKU MWEMA LAKINI USISAHAU HAKI YANGU BADO NAIDAI KUTOKA KWAKO!" Mr Brown alichoka kabisa Mara baada ya kuisoma SMS ile, akampa simu na mkewe naye apate kuusoma ujumbe huo Bi Sophia na yeye pia akausoma "Mmh mume wangu hili jambo sio la mchezomchezo kabisa" Bi Sophia alisema! Mr Brown akajaribu kupiga ile namba akakuta haipatikani kabisa, basi yeye na mkewe wakabaki wanajiuliza maswali yasiyo na majibu kuhusu huyo MTU!
Ni asubuhi na mapema Monalisa na rafiki yake Suzzy wanapata kuamka kama kawaida na kujiandaa kwa ajili ya kuelekea kule kwenye biashara yao mlimani city baada ya Kumaliza kujiandaa wakaingia kwenye gari, mlinzi akafungua geti na Monalisa akapata kuitoa gari yake nje! Monalisa akapatwa na mshtuko Mara baada ya kumuona tena Yule MTU fukara akiwa amesimama palepale nje kando ya geti, Monalisa akaona Leo kama ni noma acha na iwe noma ni lazima amuulize huyu MTU kwanini anamfuatilia hivi anataka nini kwake! Monalisa akasimamisha gari na kushuka chini huku akimuacha rafiki yake Suzzy mle ndani ya gari, Monalisa huku mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio akapiga hatua kumfuata yule MTU fukara pale alipokuwa amesimama nje ya geti! Monalisa alijivika tu ujasiri kumfuata MTU yule lakini kiukweli alikuwa anamuogopa sana, hatimaye Monalisa akamfikia yule MTU!,, ITAENDELEA SEHEMU YA 04
👯MONALISA👯
SEHEMU YA: 👉04👈
Monalisa baada ya kumuona tena yule MTU fukara akiwa yupo pale nje ya geti hapa nyumbani kwake Monalisa aliamua kushuka kwenye gari na kuamua kumfuata ili amuulize kwanini anamfuatilia, na sasa ndio alikuwa anamfuata na hatimaye akamfikia yule MTU! "Habari yako?" Ndivyo Monalisa alivyoanza kwa kumsalimia huyu MTU fukara ili kumpima uwezo wake kiakili! "Habari yangu nzuri, sijui wewe!" Yule MTU alijibu salamu ya Monalisa! Hapo sasa Monalisa akashusha pumzi na kuona kumbe hapa wanaweza kuelewana, halafu sasa akamuuliza "Samahani tangu Jana nakuona umekuwa ukinifuatilia, una shida gani na Mimi?" Monalisa aliuliza! Yule MTU akajaribu kulazimisha tabasamu usoni kwake halafu akamjibu Monalisa! "Ni kweli kabisa Monalisa, ndio nakufuatilia" alijibu MTU yule, Monalisa alishtuka kusikia kuwa ametajwa jina lake na huyu MTU akajiuliza amemjuaje! "Nani kakutajia jina langu, na pia unanifuatilia unataka nini kwangu?" Hayo ni maswali ambayo Monalisa yalimtoka mfululizo! Yule MTU fukara akacheka Sana halafu akasema: "Sikiliza Monalisa nikuambie kitu, Mimi sio kichaa kama unavyofikiria nimeacha nyumba ngapi mpaka nimekuja kusimama hapa kwako?" yule MTU alisema! "Sawa
nimekuelewa, haya basi jitambulishe wewe ni nani na pia una shida gani?" Monalisa aliuliza "Mimi kujitambulisha kwako ni bado mapema sana, lakini ukitaka kunijua Mimi ni nani subiri kwanza" alisema MTU Yule huku akiingiza mkono kwenye mfuko wa koti lake ambalo lilikuwa limechakaa na kuchanika kisha akatoa bahasha ndogo na kumkabidhi Monalisa! Monalisa akasita kuipokea ile bahasha! "Binti naomba upokee hii bahasha na uende ukampe mama yako, halafu yeye atakuambia Mimi ni nani!" alisema MTU yule huku akimkazia macho Monalisa! Monalisa akajikuta
anaipokea bahasha ile huku mikono yake ikitetemeka! "Vizuri sana binti, sasa hiyo bahasha unatakiwa kumpa mama yako na asiione mtu yeyote umenielewa?" alisema MTU yule kwa msisitizo! Monalisa aliitikia kwa kutingisha kichwa! "Sasa Mimi naondoka kwaheri tutaonana tena siku nyingine" alisema MTU yule na kisha taratibu akaondoka zake na kumuacha Monalisa akiwa ameduwaa huku ile bahasha akiwa ameishika mikononi mwake! Monalisa akamshuhudia yule MTU fukara akipotea machoni kwake halafu akaiangalia ile bahasha iliyokuwa imechoka aliyopewa na yule MTU halafu Monalisa akarudi tena kwenye gari yake na kumkuta Suzzy "Vipi yule kichaa anasemaje?" Suzzy alimuuliza Monalisa "Mwenzangu yule mtu kumbe sio kichaa" Monalisa alijibu "Eti unasemaje, wewe umejuaje kama yule mtu sio kichaa?" Suzzy akauliza kwa mshangao! Ikabidi Monalisa amsimulie yote yale waliyoyaongea na kumuonyesha ile bahasha aliyompa! "Mmh kwahiyo ndani ya hiyo bahasha kuna nini sasa?" Suzzy aliuliza "Mimi sijui yeye kaniambia nikampe tu mama kama nikitaka kumjua yeye nani" Monalisa alijibu! Suzzy alichoka kabisa kusikia hivyo! Basi baada ya hapo Monalisa akaiingiza ile bahasha kwenye mkoba wake na kisha akaiondoa gari yake eneo lile huku bado akimtafakari yule MTU!
Hatimaye wakafika maeneo Yale ya mlimani city na kufungua maduka yao na kuanza kufanya biashara, lakini Monalisa akawa na shauku ya kutaka kujua nini kipo ndani bahasha ile ambayo alipewa na yule MTU, baada ya kufikiria sana akaona ngoja tu
aifungue ili aone hicho kilichokuwepo ndani ya bahasha ni nini japo alikatazwa na Yule MTU kuwa hiyo bahasha asiione MTU yeyote zaidi ya kuifikisha kwa mama yake lakini Monalisa pamoja na rafiki yake Suzzy wakaifungua bahasha ile na ndani wakakuta kuna picha tatu! Wakaanza kuziangalia picha zile ambayo moja ilikuwa ikimuonyesha yule MTU fukara akiwa yupo pamoja na mama yake Monalisa huku wakiwa wamem'beba mtoto mdogo wa kike ambaye sio mwingine bali ni Monalisa wakati alipokuwa mdogo, picha ya Pili ilikuwa ikimuonyesha yule MTU fukara akiwa sasa amem'beba yule mtoto (Monalisa) lakini mama yake Monalisa kwenye picha hii hakuwepo, na picha ya tatu iliwaonyesha yule MTU fukara akiwa yupo pamoja na mama yake Monalisa (Bi Sophia) wakiwa wamekumbatiana kwa upendo wa hali ya juu sana huku wakiwa wanatabasamu lakini mtoto Monalisa kwenye picha hii na yeye hakuwepo! Monalisa na Suzzy walichoka kabisa Mara baada ya kuziona picha zile! "Mmh Monalisa ni nani huyu mtu?" Suzzy alimuuliza Monalisa ambaye kwa wakati huu Monalisa mawazo yake yalikuwa mbali
akikiwazia kile alichokiona kwenye picha hizi! Monalisa akabaki anajiuliza huyu MTU fukara ni nani, na pia ana uhusiano gani na mama yake mpaka wapige wote picha? na kilichomchanganya zaidi ni yeye kuonekana wakati akiwa mdogo kwenye picha hizi Monalisa akabaki na maswali yasiyo na majibu! Upande Fulani akawa anahisi yule anaweza kuwa ni baba yake lakini wazo hilo hakutaka kulipa nafasi sana, kwa kuwa kama yule ni baba yake na Mr Brown ambaye ndie anaemtambua kama baba yake mzazi atakuwa ni nani sasa? Monalisa alijihisi kupagawa! Alitamani hata jioni ifike mapema wafunge duka na kwenda mikocheni nyumbani kwa wazazi wake aende akamuonyeshe mama yake zile picha, Monalisa alipanga awahi kufika kule kabla Mr Brown ajarudi nyumbani ili iwe rahisi kwa yeye kumkabidhi mama yake zile picha na kumfafanulia vizuri kuhusu yule MTU fukara!
Hatimaye jioni iliyokuwa inangojewa kwa hamu na Monalisa pamoja na Suzzy ikawa imewadia na wakafunga maduka yao mapema sana siku hii ya Leo Baada ya kumaliza kufunga maduka wakaingia kwenye gari na safari ya kuelekea mikocheni ikaanza kwenda kumuona Bi Sophia mama yake na Monalisa ili kumuonyesha picha zile na ikiwezekana awaambie yule MTU fukara ni nani!,, ITAENDELEA SEHEMU YA 05
👯MONALISA👯
SEHEMU YA: 👉05👈
Sasa Monalisa akiwa yupo ndani ya gari pamoja na rafiki yake Suzzy wakielekea mikocheni kwenda kumuona Bi Sophia mama yake Monalisa ili wakamuonyeshe zile picha na pia walitaka awaambie kuhusu yule MTU fukara ni nani, Monalisa bado mawazo yaliendelea kukisumbua kichwa chake alikuwa bado akimfikiria yule MTU fukara kuwa ni nani kwake na pia alikuwa na uhusiano gani na mama yake mpaka ifikie wamepiga picha ya pamoja na pia akawa anajiuliza yeye (Monalisa) kwenye zile picha akiwa bado yupo mdogo anahusika vipi! Safari iliendelea na hatimaye wakawasili mikocheni nyumbani kwa wazazi wa Monalisa na Monalisa akasimama gari yake nje ya geti na kupiga honi Mara mbili ambapo mlinzi wa hapa nyumbani kwao aliyekuwa amevalia uniform maalum za kazi yake ya ulinzi akapata kufungua geti na Monalisa moja kwa moja akaiingiza gari yake ndani ya uzio (Fensi) ya hapa nyumbani kwa wazazi wake, Baada ya kuingiza gari ndani
Monalisa akasimamisha gari kwenye parking ya humu ndani kisha akaizima gari yake halafu yeye pamoja na Suzzy wakateremka kwenye gari! Bahati nzuri waliwahi kufika kabla Mr Brown ajarudi hapa nyumbani na waliweza kumkuta Bi Sophia akiwa yupo kwenye eneo LA garden (Bustani) akiyamwagilia mauwa maji kwenye mpira maalum, Bi Sophia aliweza kuwaona Monalisa na Suzzy hivyo ikabidi asitishe kwanza kumwagilia Yale mauwa na kwenda kuwapokea! "Ooho karibuni sana wanangu" Bi Sophia alisema "Ahsante sana mama tumeshakaribia" Monalisa alimwambia mama yake "Vipi salama huko mtokapo?" Bi Sophia aliuliza "Huko mama ni salama kabisa, sijui hapa nyumbani" Monalisa alisema! Basi baada ya kusalimiana pale Monalisa akaona hapa ndio kwa kuanza mazungumzo kabla baba yake ajarudi "Mama sisi tumekuja tulikuwa na maongezi kidogo na wewe"
Monalisa alisema "Maongezi na Mimi, hayo maongezi vipi kwema?" Bi Sophia aliuliza Monalisa akatabasamu na kumtoa hofu mama yake: "Usishtuke mama ni maongezi tu ya kawaida" Bi Sophia akashusha pumzi halafu akasema: "Basi sawa, twende pale tukaongee" alisema Bi Sophia na kisha wakaelekea huko kwenye hiyo sehemu ya kuongea ambapo ilikuwa ni palepale uwani na kulikuwa na viti vya kukalia, Suzzy sasa ndio akabaki anamwagilia maji Yale mauwa ambayo hapo mwanzo walimkuta Bi Sophia ndie akimwagilia Suzzy akampa nafasi Monalisa ya kwenda kuongea na Mama yake! Baada ya kufika pale kwenye ile sehemu ya mazungumzo waliweza kuketi kwenye vile viti na Bi Sophia akalianzisha: "Enhe mwanangu haya niambie sasa!" Monalisa akatabasamu na kumwambia mama yake: "Usijali mama ndio ntakuambia" Bi Sophia sasa akajiweka tayari na kumsikiliza Monalisa anataka kumwambia nini! Bila hata ya kupoteza muda Monalisa akaanza kumsimulia mama yake habari yote ya yeye kufuatiliwa na yule MTU fukara kuanzia
Nyumbani kwake mpaka na kule kwenye biashara yao mlimani city na mwisho akamwambia mama yake kuhusu yeye kupewa ile bahasha na yule MTU fukara na Yale maagizo ya kuwa bahasha hiyo akampe mama yake! Bi Sophia alishusha pumzi ndefu halafu akasema: "Hebu naiomba hiyo bahasha niione" Monalisa akafungua mkoba wake na kuitoa ile bahasha na kumkabidhi mama yake, Bi Sophia akaipokea na kuifungua ambapo alizikuta zile picha na kuanza kuzitazama! Bi Sophia alipatwa na mshtuko mkubwa sana Mara baada ya kuziangalia picha zile! "Wee mtoto ina maana hizi picha ndio amekupa huyo mtu?" Bi Sophia alimuuliza Monalisa huku akiwa bado ajaamini kile alichokiona kwenye zile picha! "Ndio mama amenipa huyo mtu" Monalisa alimjibu mama yake! Bi Sophia aliigeuza nyuma picha mojawapo na kukuta maelezo yameandikwa kwa elufi kubwa: NI MIMI MUSSA BADO NI MZIMA SIJAFA! Kwa mshtuko Bi Sophia akaanguka chini na kupoteza fahamu! Monalisa alibaki amechanganyikiwa haraka akanyanyuka pale kwenye kiti alipokuwa amekaa na kwenda kumtingisha mama yake ambaye tayari alikuwa amezimia, Baada ya kuona mama yake aamki Monalisa akachukua ile bahasha pamoja na zile picha na kuzirudisha kwenye mkoba wake! Ajabu Yale maelezo yaliyokuwa yameandikwa kwenye picha wao kule mwanzo awakuyaona! Basi haraka Monalisa akamwita Suzzy na Mara baada ya Suzzy kufika akauliza: "Vipi tena Monalisa nini kimetokea hapa?" Monalisa huku machozi yakimlengalenga machoni kwake akasema: " Baada ya kumuonyesha zile picha, mama ameanguka chini na kuzimia!" Ikabidi wamuite mlinzi na Baada ya mlinzi kuja
wakamuomba awasaidie kum'beba Bi Sophia wampakie kwenye gari wamuwahishe hospital, mlinzi alipatwa na mshangao na maswali ya kujiuliza nini kimetokea lakini hakupata nafasi ya kuuliza! Haraka akamnyanyua Bi Sophia pale chini alipodondokea huku akisaidiwa na Monalisa pamoja na Suzzy wakampeleka kwenye gari ya Monalisa na Monalisa akawasha gari Suzzy naye akaingia kwenye gari, mlinzi akafungua geti na Monalisa akapata nafasi ya kuitoa gari yake nje na safari ya kumpeleka hospital mama yake ikaanza!!,, ITAENDELEA SEHEMU YA 06 Alihamisi ijayo
Kama bado hujapata App ya blog hii Download hapo chini 👇
0 Maoni