MONALISA
SEHEMU YA: 16
Monalisa baada ya kuingia ofisini kwa Mr Brown alimkuta akiongea na simu na baada ya Mr Brown kumuona Monalisa ameingia ofisini kwake haraka sana akakata simu ile aliyokuwa anaongea nayo na kisha akamuangalia Monalisa huku akitabasamu, Monalisa alimuangalia Mr Brown kwa hasira ya hali ya juu sana! "Vipi binti yangu mbona hivyo tena?.." Mr Brown alimuuliza Monalisa. "Mimi sio binti yako tena, kwanini lakini unakuwa mkatili kiasi hiki?.." Monalisa aliwaka kwa jazba. Mr Brown akapigwa na butwaa akijiuliza vipi siri yake imegundulika nini! "Nimekuwa mkatili kuhusu nini mwanangu, mbona sikuelewi Eti?." Mr Brown alijifanya kushangaa. "Utanielewa tuu, unafikiri sijui ulichokifanya kwa baba yangu!.." Monalisa alizidi kumpa wakati mgumu baba yake mlezi huyo. "Monalisa umechanganyikiwa, kwani wewe una baba mwingine zaidi yangu mimi..?" Mr Brown alihoji. Basi ikawa ni vurugu mle ofisini kwa Mr Brown kwani Monalisa bado aliendelea kumsumbua Mr Brown kuhusu ni wapi alipompeleka baba yake (Mzee Mussa) ikawa ni hekaheka Monalisa alichachamaa ile kisawasawa, Mr Brown kila akijitahidi kumtuliza Monalisa na kumwambia kuwa yeye ahusiki na tukio hilo na zaidi akajidai kutomtambua kabisa huyo Mzee Mussa. Lakini wapi Monalisa hakumuelewa kabisa Mr Brown! Ikabidi Mr Brown apige simu kwa mlinzi na kuomba msaada wa kuja kumuondoa Monalisa hapa ofisini ambapo mlinzi huyo alifika ndani ya muda mfupi na kuanza kumtoa Monalisa kwa nguvu, "Sawa mimi naondoka, lakini ukumbuke kuwa damu ya mtu haipotei bure!.." Monalisa alisema kwa hasira na kuondoka ofisini mle huku mlinzi akimfuatia kwa nyuma! Mr Brown huku nyuma alibaki na maswali ya kujiuliza kuwa huyu Monalisa hizi habari kama yeye sie baba yake amezipata wapi? Mr Brown alipagawa sana. "Hapa cha kufanya ni kuwauwa wote, kuanzia yule kunguni mpaka na mama Monalisa pamoja na Monalisa mwenyewe!.." Mr Brown alijisemea mwenyewe, hakutegemea kabisa kama ile siri ya kuwa yeye sie baba mzazi wa Monalisa ingeweza kuvuja kwani hata Mali zake zote alimuandikisha Monalisa akiwa ndio kama mtoto wake wa kipekee halafu Leo zinakuja habari za Monalisa kumtambua baba yake halisi. Hapa sasa Mr Brown aliona sio tena kuziba ufa ili ajenge ukuta Bali aliona dawa ni kuubomoa huo ukuta wenyewe kisha aujenge tena upya! "Inawezekana vipi mbwa nimfuge mwenyewe, halafu leo hii atake kuniuma meno!?." Mr Brown alijiuliza yeye mwenyewe huku akitabasamu kiufedhuli, akafungua droo ya ofisini kwake na kutoa bastora yake ndogo na kuitazama kisha akaibusu bastora yake hiyo. "Hii ndio njia rahisi ya kuwafikisha kuzimu hawa mbwa, pumbavuu!." alitamba Mr Brown!
Monalisa baada ya kuondoka ofisini kwa Mr Brown kwa kutolewa kwa nguvu na yule mlinzi aliyeagizwa na Mr Brown, Monalisa alienda moja kwa moja mlimani city na kuonana na rafiki yake Suzzy ambapo alimsimulia jinsi alivyoenda ofisini kwa Mr Brown na alivyomfyatukia kwa kumuambia ukweli wake alichokifanya kinajulikana! Suzzy akamshauri Monalisa na kumwambia kuwa kilichobaki sasa ni kuripoti polisi ili wamfuatilie Mr Brown nyendo zake na ikigundulika kuwa ni kweli amemteka Mzee Mussa basi na wamkamate, Monalisa alikubaliana na ushauri wa Suzzy bila kupoteza muda akaenda polisi na kutoa maelezo yake jinsi alivyopotelewa na baba yake na kumuhisi Mr Brown ambaye ni baba yake mlezi kuhusika na tukio hilo. Polisi waliandikisha maelezo ya Monalisa na baada ya hapo wakamtaka Monalisa awapeleke ilipo ofisi ya Mr Brown ili waanze kumfuatilia kwani polisi walijua kwa vyovyote vile kama ni kweli atakuwa amemteka Mzee Mussa basi ni lazima akitoka ofisini kwake ataelekea huko alikofichwa Mzee Mussa!
Askari polisi wakiwa ndani ya gari ya kiraia pamoja na mavazi pia ya kiraia Lakini silaha walikuwa nazo wakapiga kambi nje ya jengo la ilipo ofisi ya Mr Brown kwa mujibu wa maelezo aliyowapa Monalisa, askari waliendelea kusubiri mpaka majira ya mchana wakamuona Mr Brown akitoka ofisini kwake na kuingia kwenye gari yake na kuondoka zake na polisi nao pia wakaanza kumfuatilia kwa nyuma Mr Brown ambaye hakujua kama anafuatiliwa nyuma na mapolisi. Monalisa naye alikuwepo kwenye msafara huo kwani alikodi Tax na kumuambia dereva afuatilie hizo gari kwa ukaribu sana hakutaka kutumia gari yake kwa kuhofia ingeweza kujulikana pia Monalisa hakutaka kabisa kumshirikisha mama yake juu ya jambo hili kwani hakuwa anamuamini tena baada ya kukumbuka Mzee Mussa jinsi alivyomsimulia kuwa alimsaliti kwa sababu ya Mr Brown, Mr Brown akiwa yupo ndani ya gari yake safari yake hii ilikuwa ni kuelekea kinyerezi ilipo nyumba yake ya siri ambayo Mzee Mussa ndio alikuwa amefichwa na wale majambazi aliowatuma wakamteke kule hotelini na sasa ndio alikuwa anaelekea huko kwenda kum'maliza kabisa Mzee Mussa. Bahati mbaya Mr Brown hakujua kama anafuatiliwa nyuma na maaskari pamoja na Monalisa mwenyewe!,
ITAENDELEA
MONALISA
SEHEMU YA: 17
Mr Brown akiwa hajui hili wala lile yeye alikuwa anaendelea na safari yake ya kuelekea kule kwenye nyumba yake ya siri iliyokuwa maeneo ya kinyerezi kwenda kumuua Mzee Mussa ambaye tayari alikuwa ameshatekwa na wale majambazi aliowatuma waende wakamteke kule hotelini ambao walifanikiwa kumteka na sasa kilichokuwa kinasubiriwa ni boss Mr Brown kwenda huko kumaliza kazi ya kumpeleka kuzimu Mzee Mussa.
Polisi nao waliendelea kulifuatilia gari la Mr Brown kwa ukaribu sana ili kujua ni wapi hasa alipokuwa anaelekea, Monalisa naye akiwa yupo kwenye ile Tax aliyokuwa ameikodi na kumuambia dereva afuatilie msafara huo nao walikuwa nyuma kabisa wakifuatilia. Monalisa alishangaa kuona msafara ule ukielekea maeneo ya kinyerezi hapo akajua kwa vyovyote vile Mr Brown atakuwa anaenda kumuua baba yake (Mzee Mussa) roho yake iliumia sana, lakini akajipa imani na hawa askari polisi waliokuwa wakimfuatlia Mr Brown kuwa watawahi kudhibiti jambo hilo la mauaji kabla alijatokea. Wakati safari ikiwa inaendelea Monalisa akajaribu kuvuta kumbukumbu zake na kukumbuka mambo mengi mazuri aliyofanyiwa na Mr Brown wakati alipoamini kuwa ni baba yake mzazi kabla ajatokea Mzee Mussa aliyeanza kumfuatilia na mwanzo alipomchukulia kama ni mwendawazimu tu mpaka mama yake alipomthibitishia na kumwambia huyo ndie baba yake halisi kule manzese midizini kwenye lile banda la mama lishe alilokuwa akijihifadhi Mzee Mussa hapo mwanzo, ghafla wakaona ile gari ya wale askari ikipunguza mwendo na kusimama kabisa ikabidi na dereva wa Tax aliyokodi Monalisa naye asimamishe gari kwa nyuma yao.
Gari ya Mr Brown ilisimama nje ya jumba kubwa lililokuwa limezungushiwa uzio na mbele kulikuwa na geti kubwa la rangi nyeusi, Mr Brown akapiga honi Mara mbili na geti hilo likafunguliwa gari ya Mr Brown ikapata kuingia ndani na baada ya hapo geti likafungwa!
Gari ya maaskari ambayo ilikuwa imesimama kwa mbali kidogo na eneo hilo sasa askari wale wakashuka kwenye gari na kuanza kujadiliana ni namna gani wataweza kuingia ndani ya huo mjengo alioingia Mr Brown ili waende kujua nini kinaendelea humo, Monalisa naye akashuka kwenye ile Tax na kwenda mpaka kwa wale maaskari.
"Binti usiwe na wasiwasi kabisa, hapa tunajadili namna ya kuingia humo ndani kwenda kumkomboa baba yako.." askari aliyeonekana kuwa na cheo kikubwa alisema.
Jamani afande naombeni mfanye haraka asije akamuua baba yangu." Monalisa naye alisema kumwambia askari yule, basi bila kuchelewa mkuu yule wa maaskari akakipanga kikosi chake na njia rahisi waliyoiona ilikuwa ni kuruka uzio wa hilo jumba na kisha watumbukie kwa ndani yake, bahati nzuri eneo hilo halikuwa na pilikapilika za watu wengi hivyo ikawa ni nafasi nzuri kwa askari wale kuruka uzio na kuingia ndani bila kuonekana na macho ya wapita njia kwani mtaa huo ulikuwa umepoa sana!
Monalisa alirudi kwenye ile Tax na kubaki na yule dereva wa Tax ndani ya gari baada ya kuambiwa hivyo na wale askari kuwa sasa inabidi akae mbali na awaachie wao hiyo kazi ya kujaribu kumkomboa Mzee Mussa kutoka kwenye himaya ya Mr Brown alimokuwa amewekwa mateka,
Monalisa akiwa yupo ndani ya gari aliendelea kumuomba Mungu hili baba yake (Mzee Mussa) apate kuokolewa na maaskari wale alitokea ghafla kumchukia Mr Brown kwa sababu ya ukatili wake wa kutaka kumuua Mzee Mussa asiye na hatia yeyote maskini na ikiwa mke ambaye ndie mama yake yeye Monalisa pamoja na yeye mwenyewe (Monalisa) walichukuliwa na Mr Brown ili apate kuficha siri yake ya kutokuzalisha. Mara ghafla ikasikika milio ya risasi kutokea mle ndani ya ule mjengo ambao Mr Brown aliingia na wale askari pia nao wakaingia, risasi ziliendelea kusikika kuonyesha kuwa mle ndani kulikuwa na mapambano makali huku mayowe zikisikika za watu kuugulia maumivu. Monalisa akaingiwa na hofu sana baada ya kusikia milio ile ya risasi hakujua nini kinaendelea humo ndani yake zaidi alikuwa na wasiwasi kuhusu usalama wa baba yake mzazi (Mzee Mussa) kwa upande wa Mr Brown wala hakumfikiria kabisa aliona hata wale maaskari wakimuua au kumkamata ni sawa tu japo amemlea tangu akiwa mdogo lakini kwa haya mambo yake ya kikatili alishaanza kumchukia na kumuona ni muuaji.
Monalisa akawa anataka kutoka mle ndani ya gari na kwenda kule kwenye ule mjengo ambao ndio ulikuwa ukisikika risasi zikirindima ndani yake haikujulikana kama ni maaskari ndio walikuwa wanashambulia mpambano huo au ni wale majambazi wa Mr Brown, hali hiyo ilimpa sana mashaka Monalisa ikabidi dereva wa Tax apate kazi ya ziada kumtuliza Monalisa aliyekuwa bado amechanganyikiwa! Baada ya risasi zile kurindima kwa muda wa saa moja na nusu (1:30) hatimaye kukapoa na kuwa kimya kabisa, mpaka hapo bado haijafahamika nani kapigwa na nani amepona. Punde lile geti kubwa likapata kufunguliwa na watu kuonekana wanatoka nje kabisa sasa hapo sasa ikabidi Monalisa na yule dereva kukaza macho yao vizuri na kuangalia ni akina nani hao wanaotoka nje!,
ITAENDELEA
MONALISA
SEHEMU YA: 18
Monalisa akiwa yupo na yule dereva wa ile Tax aliyokodi wakati wapo ndani ya gari Mara ghafla wakaona geti kubwa la kwenye ule mjengo walioingia wale maaskari kumfuata Mr Brown ukifunguliwa na watu wakaonekana kutokea ndani yake. Monalisa na yule dereva wakakaza macho yao vizuri ili kuona ni akina nani hao wanaotoka humo ndani! Wakaweza kuwaona maaskari kama watatu hivi akiwepo na yule askari mkuu aliyekuwa akiongoza operesheni hii ya kumkomboa Mzee Mussa kutoka kwenye himaya ya Mr Brown, maaskari wale walionekana kama kuna jambo Fulani wanalijadili hapo Monalisa uvumilivu tena ukamshinda kwani alitoka kwenye gari na kwenda moja kwa moja mpaka pale waliposimama wale maaskari na kuwauliza nini kinaendelea mpaka muda huo. "Binti tunaomba uwe mtulivu, kwani kazi ya kumkomboa baba yako tumeifanikisha vizuri sana japo tumepoteza askari wetu wawili kwenye mapambano!,," alisema kwa huzuni yule mkuu wa maaskari. Monalisa naye alihuzunika sana baada ya kusikia vile kuwa kuna askari waliopoteza maisha yao kwenye mapambano Yale! "Sasa binti ni hivi, tumewasiliana na makao makuu waje hapa kutupa msaada wa kuwachuhukua hawa watuhumiwa wote pamoja na majeruhi!,," aliendelea kusema yule askari, Monalisa akaomba apewe angalau nafasi ya kumuona baba yake (Mzee Mussa) wale askari wakamwambia kwanza asubiri mpaka msaada utakapokuja.
Wakiwa wapo kwenye kusubiri Mara ghafla zikatokea gari mbili aina ya Land Cruiser (Pick up) za polisi waliokuja na silaha na moja kwa moja wakateremka kwenye zile gari na kuanza kuongea na wenzao wale waliokuwa kwenye eneo hilo na baada ya kuongea kwa muda kidogo na kupeana taharifa ya nini kilitokea hapo wakamtaka Monalisa na yule dereva Tax kusubiri hapo nje na kisha wao wakaingia ndani ya ule mjengo. Monalisa akasubiri nje!
Baada ya muda wakaonekana askari wakiwa wamebeba kwenye machela maalumu zile maiti mbili za wale maaskari wawili waliouwa kwenye mapambano Yale na wakazipakia maiti hizo kwenye gari halafu baadae wakatolewa wale majambazi watatu waliomteka Mzee Mussa huku wakiwa na boss wao Mr Brown wote wakiwa wamefungwa pingu kwenye mikono yao na kisha na wao wakapakiwa kwenye gari ya polisi, mwisho kabisa akatolewa Mzee Mussa huku akiwa na majeraha kidogo kwenye mwili wake ilikuwa inaonyesha kabla ya kufika maaskari majambazi wale walianza kumpa kibano. Monalisa alipomuona alimkimbilia na kwenda kumkumbatia baba yake (Mzee Mussa) huku akilia machozi kuonyesha aamini Kama amenusurika kuuawa na Mr Brown!
Basi baada ya hapo wote wakaingia kwenye magari na kuanza safari ya kuondoka kwenye eneo hilo zile maiti mbili za wale maaskari zikipelekwa kwenye hospitali ya taifa kwenda kuhifadhiwa na wale watuhumiwa wote wakipelekwa kwenye kituo cha polisi kwenda kufunguliwa mashtaka ya kesi iliyokuwa inawakabili wakati huo, Mzee Mussa naye alipanda gari moja na Monalisa kwenye ile Tax aliyokodi Monalisa na wakawa wanaelekea hospitali kwanza ili kwenda kupata matibabu ya Yale majeraha aliyoyapata Mzee Mussa pale kwenye ule mjengo wa Mr Brown walibakishwa askari watatu ili kulinda usalama wa eneo hilo! Mzee Mussa aliweza kupatiwa matibabu ya Yale majeraha yake yaliyokuwa kwenye mwili wake na aliweza kuruhusiwa kutoka hospitali siku hiyo hiyo Monalisa alifurahi sana kumuona baba yake akiwa mzima japo majeraha alikuwa nayo lakini furaha ya Monalisa ilikuwa ni kumuona baba yake akiwa mzima, yule mkuu wa maaskari aliyoongoza ile operesheni ya kumkomboa Mzee Mussa alimwita Monalisa pamoja na Mzee Mussa kituoni na kuwaomba kuwa wawe mashahidi kwenye kesi ile kwani muda wowote Mr Brown pamoja na wale majambazi wake watafikishwa mahakamani kwenda kujibu mashtaka yao yanayowakabili. Monalisa na Mzee Mussa walikubali kuwa mashahidi, basi ikabidi waruhusiwe kurudi nyumbani!
Monalisa akiwa na baba yake akaenda mpaka sehemu alipoiacha gari yake na kisha wakapanda na kuelekea mlimani city kwenda kumfuata Suzzy kwani jioni tayari ilikuwa imeshafika na baada ya kumfuata Suzzy wakaenda kwanza kule Sinza hotelini alipokuwa anaishi Mzee Mussa mwanzoni kabla ya kutekwa na wale majambazi waliotumwa na Mr Brown baada ya kufika hotelini hapo wakachukua vitu vyote vya Mzee Mussa na Monalisa akamuomba waende wakaishi wote kule nyumbani kwake mbezi beach na Mzee Mussa akaweza kukubali bila hata ya kuwa na kipingamizi. Basi wakaondoka hotelini pale na kuingia kwenye gari ya Monalisa na safari ya kuelekea mbezi beach nyumbani kwa Monalisa ikaanza wakiwa wapo ndani ya gari sasa Monalisa akaona ngoja amjulishe mama yake (Bi Sophia) Yale yote yaliyotokea akachukua simu yake na kumpigia mama yake baada ya Bi Sophia kuipokea simu ya Monalisa akaelezwa kila kitu kilichotokea na Bi Sophia akamtaka mwanae Monalisa wampitie kule nyumbani kwa Mr Brown mikocheni ili waongee vizuri kuhusu suala hilo, Monalisa akamwambia baba yake (Mzee Mussa) jinsi alivyoongea na mama yake Mzee Mussa akaweza kukubali wampitie tu Bi Sophia huko mikocheni!, ITAENDELEA
MONALISA
SEHEMU YA: 19
Monalisa akiwa yupo na baba yake Mzee Mussa pamoja na rafiki yake Suzzy wakawa wanaelekea mikocheni nyumbani kwa Mr Brown kwenda kumuona bi Sophia ambaye alimuoomba Monalisa wampitie, baada ya muda waliweza kufika mikocheni na kumkuta Bi Sophia ambaye aliwakaribisha vizuri sana.
Bi Sophia alishangaa kumuona Mzee Mussa akiwa na muonekano mwingine wa kupendeza tofauti na alivyokuwa amemuona kwa Mara ya mwisho wakati wanamchukua kule manzese midizini na Monalisa akaenda kumpangia kwenye ile hoteli ya kule Sinza! Monalisa alimsimulia mama yake (Bi Sophia) Yale mambo yote yaliyotokea mpaka Mzee Mussa akatekwa na wale majambazi waliotumwa na Mr Brown kule hotelini na pia akamsimulia jinsi alivyoenda kuripoti polisi hilo tukio na polisi walivyofanikiwa kumkomboa Mzee Mussa na kuwakamata majambazi wale wote pamoja na Mr Brown, Bi Sophia alishangaa sana kusikia hivyo! "Kwahiyo mama ndio hivyo,nimeamua kumchukua baba yangu na naenda kuishi naye..!" Monalisa alimwambia mama yake.
Bi Sophia alimuomba tena msamaha Mzee Mussa na kumuomba amsamehe kwa yote aliyomfanyia kipindi cha nyuma mpaka akamsaliti na kwenda kuishi na Mr Brown pamoja na mtoto wao ambaye ndio Monalisa kipindi hicho alipokuwa bado mdogo sana! Mzee Mussa akamwambia Bi Sophia kuwa alishamsamehe tangu zamani na pia hana kinyongo naye kabisa hivyo ajisikie tu kuwa na amani,
"Kwahiyo mama habari ndio hiyo, kesho jiandae kumpelekea chai asubuhi mumeo kituoni!.." Monalisa alimwambia mama yake. Baada ya hapo wakamuaga Bi Sophia na kuondoka kuelekea nyumbani kwa Monalisa mbezi beach!
Baada ya wiki moja kupita Mzee Mussa sasa Yale majeraha aliyokuwa nayo baada ya kuyapata wakati alipotekwa na watu wa Mr Brown ambao walianza kumpa kipigo kwanza kabla ya kuja kuokolewa na askari polisi, Mzee Mussa kwa sasa aliendelea vizuri sana na aliyafurahia maisha kwa kuwa karibu na binti yake Monalisa.
Siku moja Monalisa alimwambia hivi Mzee Mussa: "Baba unaonaje kama ukirudiana na mama ili muishi pamoja tena?.." Monalisa alisema.
Mzee Mussa akafikiria kwa muda halafu akamuuliza Monalisa: "Unapenda nirudiane na mama yako mwanangu?.." Mzee Mussa aliuliza.
"Ndio baba yaani nitafurahi sana, kama wazazi wangu mtakuwa pamoja,," Monalisa alisema. Mzee Mussa akashusha pumzi halafu akasema: "Sawa mwanangu nimekusikia, ngoja iishe kwanza hii kesi ya huyo baba yako mlezi Mr Brown!.." alisema Mzee Mussa.
Kesi iliyokuwa inamkabili Mr Brown pamoja na wale majambazi wake ya kumteka Mzee Mussa na kutaka kumuua pamoja na kesi ya kusababisha vifo vya wale askari polisi waliouwawa wakati wa mapambano Yale, sasa iliweza kufikishwa mahakamani Mara baada ya uchunguzi wake kukamilika na Monalisa pamoja na Mzee Mussa walitakiwa kwenda kutoa ushahidi wao ili mahakama iweze kutoa hukumu kwa watuhumiwa wote wa kesi ile. Mpaka kwa wakati huu Mali zote za Mr Brown Zilikuwa zipo chini ya Monalisa kama ambavyo Mr Brown mwenyewe alivyomuandikisha wakati huo mambo yalivyokuwa kabla hayajaharibika na Mr Brown kuamini kuwa Monalisa ataendelea kuwa ni mwanae! Siku ya hukumu ilifika na Monalisa pamoja na baba yake halisi (Mzee Mussa) pamoja na Bi Sophia na Suzzy walifika mahakamani na baada ya muda karandinga la mahabusu lilifika kutokea magereza na Mr Brown pamoja na wale majambazi wake walishushwa na kupandishwa kizimbani mahakamani hapo ili kusomewa mashtaka yao na baada ya hapo hukumu ipate kutolewa!!,
ITAENDELEA SEHEMU YA MWISHO KABISA.
MONALISA
SEHEMU YA: 20 (MWISHO)
Mr Brown pamoja na wale majambazi wake aliowaagiza kumteka Mzee Mussa kwa lengo la kumuua sasa wote walifikishwa mahakamani kwenda kujibu mashtaka ya kesi iliyokuwa inawakabili ya kumteka na kutaka kumuua Mzee Mussa pamoja na kusababisha mauaji kwa wale askari polisi wawili waliouwa kwenye mapambano Yale ya kumkomboa Mzee Mussa kwenye ule mjengo wake wa kinyerezi.
Siku ys hukumu ilifika na Monalisa pamoja na baba yake Mzee Mussa walitakiwa kufika pale mahakamani ili kutoa ushahidi wao kwa kuwa muhusika mwenyewe wa kutekwa alikuwa ni Mzee Mussa, basi Monalisa pamoja na Mzee Mussa walifika pamoja na Bi Sophia mama yake Monalisa na rafiki wa Monalisa Suzzy nao walikuwepo! Muda wa kusomwa kesi ulipoanza hakimu alisoma mashtaka kwa watuhumiwa wote na hawakutakiwa kujibu kitu chochote kwa vile ushahidi wote ulikuwa upo hadharani, Mzee Mussa akiwa kama ndio shahidi namba moja aliweza kutoa ushahidi wake pale mahakamani kuanzia jinsi alivyotekwa na wale majambazi mpaka walipomfikisha kule kwenye lile jumba kinyerezi kwa lengo la kumuua na polisi baadae walivyokuja kumuokoa, Monalisa naye akiwa kama ni shahidi namba mbili naye pia akatoa ushahidi wake wa kuanzia alipoanza kumtilia mashaka baba yake huyo mlezi kuhusika na tukio la kutekwa baba yake halisi Mzee Mussa kule hotelini na mpaka walipomfuatilia pamoja na askari polisi na kumkuta kinyerezi ambapo ndio Mr Brown alikusudia kumuua Mzee Mussa. Mwisho kabisa shahidi namba tatu alikuwa ni yule askari polisi aliyeongoza operesheni makini ya kumkomboa Mzee Mussa naye Afande yule akatoa ushahidi wake jinsi walivyofanikiwa kuwakamata watuhumiwa wote hao tena wakiwa na silaha ambazo Zilikuwa zinamilikiwa kinyume na sheria zilizosababisha vifo kwa askari polisi wao wawili! Basi hakimu alilidhishwa na ushahidi wote uliopatikana na aliweza kutoa hukumu yake dhidi ya washtakiwa wale kwa kuanzia na kesi ya kumteka na kutaka kujaribu kumuua Mzee Mussa hakimu aliwahukumu kila mmoja kati ya washtakiwa wale wanne ambaye ni Mr Brown pamoja na wale majambazi wake watatu kila mmoja kutumikikia kifungo cha miaka thelathini (30) jela, na katika kesi ya Pili iliyokuwa ikiwakabili ya kusababisha mauaji kwa askari polisi wale wawili hapo hakimu hakuwaonea huruma hata kidogo watuhumiwa wale kwani akawahukumu wote kifungo cha maisha jela. Baada ya kutoka hukumu ile Monalisa kwa upande wake alifurahi sana kuona sheria imefuata mkondo wake na pia upande mwingine alihudhunika kwa kuona Mr Brown aliyeamini kuwa ni baba yake mzazi kwa kumlea na kumuhudimia kama mwanae pamoja na kumsomesha na mpaka hapo alipofikia kuwa na maisha mazuri aliyonayo hivi sasa, hapo Monalisa alishindwa kujizuia akajikuta analia machozi kumlilia baba yake mlezi huyo Mr Brown! Kabla Mr Brown ajapandishwa kwenye karandinga la magereza ili kwenda kuyaanza maisha mapya ya gerezani kwanza aliomba nafasi ya kuongea kidogo na Monalisa na alipopewa nafasi hiyo alimwambia hivi: "Nisamehe sana mwanangu kwa yote niliyoyafanya, nilifanya hivi kwa ajili yako mwanangu sikutaka umjue baba yako halisi!,," Mr Brown alisema huku akilia machozi. "Mwisho kabisa mwanangu kuanzia sasa Mali zangu zote zitakuwa chini yako naomba uzitunze na zitawasaidia sana,," alisema Mr Brown na kisha akaja askari magereza na kuanza kumswaga Mr Brown kama ng'ombe kumuingiza kwenye karandinga na safari ya kuelekea gerezani ikaanza kwenda kutumikia vifungo vyao, huku nyuma Monalisa alibaki anamlilia lakini ndio hivyo tena hukumu tayari ilishatoka. Basi hakukuwa na la ziada tena mahakamani pale Monalisa pamoja na wazazi wake na rafiki yake Suzzy wakaingia kwenye gari na safari ya kurudi nyumbani na wao ikaanza!
Baada ya mwezi mmoja kupita maisha ya Monalisa na wazazi wake yaliendelea vizuri sana kwani Monalisa aliweza kuwaunganisha tena wazazi wake hivyo kuanzia hapo Mzee Mussa pamoja na Bi Sophia wakawa ni kitu kimoja mapenzi yao moto moto yakaibuka na kuzaliwa tena upya kwa msaada wa mtoto wao Monalisa mambo yao sasa yakawa ni Bam bam wakafanya yaliyopita si ndwele na kuganga yajayo, Monalisa na wazazi wake wote wakawa wanaishi pamoja kule kwenye lile jumba lake mbezi beach na kule mikocheni nyumbani kwa Mr Brown Monalisa aliwapangisha wazungu pia Monalisa aliweza kuzisimamia vyema Mali zote zilizoachwa na Mr Brown kwa msaada wa ushauri wa wazazi wake yaani Mzee Mussa pamoja na Bi Sophia. Pia Monalisa bado aliendelea kuwa karibu na yule rafiki yake Suzzy ambaye alikuwa ni yatima hivyo wakawa wote wanaishi pamoja na maisha yakawa yanaendelea kihivyo. Siku moja wakati wanakula chakula cha usiku Monalisa aliwaambia wazazi wake hivi: "Baba na mama kesho mchumba wangu anakuja kutoka marekani alikokuwa masomoni akisomea udaktari, kwahiyo nawaombeni wote kwa pamoja twende uwanja wa ndege kumpokea!,," Monalisa aliposema hivyo Bi Sophia pamoja na Mzee Mussa walifurahi sana na wakaahidi wataenda kumpokea na kumuona huyo mkwe wao kutoka marekani!,
MWISHO KABISA NIMEMALIZA.
Mwisho wa hadithi karibu kwa maoni kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇
Bonyeza hapa Download App ya MAHABA
Makala nyingine
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Video Jifunze haya mwanaume Hawezi kuchomoka
Sababu kubwa inayo sababisha mwanaume Kupunguza mapenzi kwako
Fursa ya kujiajiri kupitia blog
Tambua sababu zinazo sababisha wanawake wengi kuachwa na waume zao
0 Maoni