Ticker

6/recent/ticker-posts

NAOMBA USHAURI JAMANI

 

Mimi ni binti wa miaka 30, sijaolewa lakini naishi na mwanaume, kabla ya huyu mwanaume kuja kwangu alikua na mke wake, nilikua anachepuka naye lakini aliniambia kuwa mke wake ni mtu wa kulalamika, hamheshimu na ana matatizo mengi hivyo anachepuka na mimi ili kupata amani. Katika kuishi naye kweli niliamini kuwa mke wake ana matatizo kwani ni mtu wa kilalamika, kila mara kupiga simu na alikua mchafu, hajali watoto, ana watoto wawili ana pesa lakini watoto walikua wanavaa hovyohovyo na mwanamke mwenyewe ni msomi lakini anakua kama wa kijijini.


Hajijali, havai vizuri mapaka ukiona huwezi kujua kama mume wake ana pesa hivyo. Alikuja kwangu nikampokea na tukawa tunafurahia maisha,a liniahidi kumuacha mke wake ili kunioa mimi, alikua ananipenda anakuja na watoto wake kwangu kwani ni wakubwa tu mmoja miaka saba na mwingine minne, watoto walikua wananipenda kwani wakija kwangu huwanawanunulia vitu vingi mpaka wanafurahi. Mwaka jana mwishoni aliachana na mke wake, haikua talaka lakini walikorofishana mwanamke akaondoka.

Mimi aliniambia kuwa mke wake kaondoka na kutelekeza watoto, kwakua nilikua nampenda na watoto walishaanza kunipenda niliwachukua na kuhamia kwake, tulianza kuishi kama mke na mume. Mkewe alipojua alisumbua na kutaka wanae lakini hatukuruhusu. Sababu ya kuja hapa nikuwa, mume wangu kabadilika, hanihudumii tena, hatoi matumizi anataka tu kuja kula, hajali hata kama ninaishi na wanae, anaweza kwenda kulala nnje hata wiki nzima ana akirudi hajali, hajui watoto wanakula nini wanavaa nini wala chochote kile.

Nikimuuliza ananiambia namimi nimeshaanza kelele, kibaya zaidi nikuwa aliniachisha kazi ili kufungua biashara lakini hajanipa mtaji, nilimpa pesa yangu milioni kumi ili akaninunulie mzigo lakini mpaka sasa hivi sioni hata sumuni. Nashindwa kujua ni kwanini kabadilika, natamani kuondoka lakini sijui nitaenda wapi, hapa ninapoandika kaondoka wiki nzima hajarudi, sina hata senti ya kula, Mama wa watoto naye hata hajali hapigi hata simu kuuliza kama wanaendeleaje, nimemtafuta ananijibu mbovu kuwa niendelee kulea wakikua watamfuata tu kwani ni wanae? Najua nilikosea kutembea na mume wa mtu lakini nifanye nini na siwezi kuondoka kwani nina mimba ya miezi sita na sina kazi

Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();