Ticker

6/recent/ticker-posts

JINSI TABIA YAKO INAVYOSABABISHA MIGOGORO KWENYE MAHUSIANO YAKO



 JINSI TABIA YAKO INAVYOSABABISHA MIGOGORO KWENYE MAHUSIANO YAKO

Kila mmoja anapenda kuelezea ubaya wa wengine kwenye migogoro yao ya mahusiano

Katika mazungumzo ya watu popote uendapo kwa 80% huwa lawama juu ya ubaya wa tabia za wengine na kuzungumza matokeo mabaya pamoja na kutafuta mtu wa kumpa lawama kwa kufeli mipango 

Kama huna maelewano mazuri na watu sio muda wa kuqnza kutaja ubaya wao bali ni muda wa kuangalia makosa yako ambayo yameweza kusababisha ugomvi huo 

Hili ni eneo gumu kwa sababu kila mtu hupenda zile habari za binadamu wabaya dunia ni nzuri utadhani wao sio binadamu

Kitendo cha kuwalaumu watu wengine kwa ubaya wa zao huwa kinafanya uzidi kuwachukia na kujiona huna makosa bali wao ndio wanatakiwa kubadilika tabia 

Kama kuna mtu amekaa kimya labda ni mwanamke au mwanaume wako ambaye unaishi nae au ni mtoto ameamua kukaa kimya na kila ukilazimisha aongee hataki kusema ujue tatizo lipo kwako sio kwake 

Sehemu zifuatazo utajua makosa yako ambayo husababisha ugomvi kwenye mahusiano yako na watu wengine

1.Huwa unasisitiza kwamba wewe upo sahihi na mwengine hayupo sahihi

2.Huwa unatoa lawama kwa wengine kuonyesha kwamba wao ndio chanzo cha ugomvi 

3.Unajihami kwa jazba na kukataa makosa yako ambayo yanatajwa 

4.Unajihami kwa kudai huna kosa lolote kama yakitajwa makosa yako 

5.Unatumia lugha mbaya kumshambulia mwengine kwa kutaka ajione mnyonge au aone aibu kama pakitokea mabishano

6.Unampa matusi na maneno mabaya mwenzio kwa sababu hamjaffikia muafaka kwenye mjadala 

7.Unatumia sauti ya ukali ili kuhakikisha unashinda mjadala dhidi ya mwenzio

8.Unakosolewa na wewe unamkosoa mwenzio ili kujihami makosa yako badala ya kujichunguza kuhusu tuhuma hizo

9.Unasisitiza mwenzio hajui chochote anachongea juu yako badala ya kujibu hoja 

10.Unabadilisha mada ili kukwepa ukweli ambao ametaja  mwenzio 

11.Unaongea huku ukiwa na hofu ya kukosolewa

12.Unadai umetumia njia zote na hujaona mabadiliko

13.Unadai mwenzio anatakiwa kuwa vile unavyotaka wewe sio vinginevyo

14.Unakataa kuwa hujahusika kwenye ugomvi au unasititiza kuwa hujahuzunika kwa ugomvi huo wakati kiuhalisia huna furaha juu ya ugomvi huo 

15.Unatoa msaada au kumpa ushauri  mwenzio badala ya kumsikiliza kwanza (Wanaume wengi hufanya kosa hili wengi hawajui kusikiliza malalamiko ya wanawake zao) 

16.Huonyeshi kujali hisia za mwenza badala yake Unataka kutatua matatizo ya mwenzio  haraka sana 

17.Huongei chochote zaidi unafunga mlango kwa nguvu na kuondoka eneo hilo (hiki ni kiburi na husababisha hasira sana kwa mwenzio)

18.Unataka mwenzio ajue kile ambacho unafikiria na endapo hajaonekana kujua kile unafikiria unaanza kulaumu

Hapa utakuwa umeona kwa kiwango gani umekuwa unachangia kutokea kwa migogoro kwenye mahusiano yako 

Kama unataka ugomvi shughulika kurekebisha makosa ya wengine utaona mwenzio anavyozidi kuwa jeuri 

Kila ukieleza makosa ya mwenzio na yeye huwa hakubali bali anakuja juu kueleza makosa yako ya zamani ili kubalance mjadala

Kosa kubwa ambalo wanaume wengi hufanya ni kwamba hawajui kueleza hisia zao hivyo hutumia nguvu na maneno makali kueleza hisia zao 

Ukiwa mtu mzima jirekebishe kwa kueleza hisia zako badala ya kuanza kulaumu wengine

Kama umechukizwa kwa tabia fulani sema ninasikitika au naumia sana/ninajisikia vibaya kukuona unafanya jambo fulani sio kumjia juu na matusi ya nguoni au kipigo au lawama 

Jifunze kueleza hisia zako ziwe nzuri au mbaya eleza tu sio kuweka vitu rohoni na kununa bila sababu za msingi 

Eleza tu leo nimependa uvaaji wako au Leo nimechukizwa na kitendo fulani umefanya n.k 

Jakukosolewa
ngi mwenzio ajue hisia zako kuepuka ugomvi

Mwisho wa makala asante kwa kusoma mpaka mwisho wa makala yetu karibu kwa maswali maoni na ushauri ikiwa una tangazo unahitaji tukutangazie Humu pia

*BADILI MAISHA*

*Ukitaka kufahamu njia ya kutengeneza Dora 100  mtandaoni kwa mtaji wa Sh:35,000 njoo inbox nikupe huo mchongo*Whatsapp 

kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇
Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();