JINSI YA KUKABILIANA NA MWANAUME/ MWANAMKE MWEMYE MALALAMIKO KUPITA KIASI |
Utakuwa umeishi na watu wenye tabia ya kulaumu sana na kulalamika kupita kiasi hata kwa vitu vidogo sana
Kama unaishi na mwanamke au mwanaume ambaye amekuwa kero kwa lawama zake kupita kiasi ba malalamiko ambayo hayana mwisho hii inaweza kukusaidia
Ukweli ni kuwa matatizo mengi suluhu zake zipo nyepesi ila watu wengi huteseka kwa sababu ya uvivu na kiburi
Jinsi ya kuishi na mtu ambaye analalamika kupita kiasi hata kama umefanya vitu vizuri mara ngapi bado huwa analalamika kupita kiasi ni rahisi sana
Kosa kubwa watu wengi hufanya ni kutoa ushauri,kutoa msaada,au kubishana naye kila wakati
Kama mtu analalamika sana usijaribu kumpa ushauri,usimpe msaada wa malalamiko yake,wala usianze kubishana naye kwa sababu utazuka ugomvi na mjadala mkubwa kupita kiasi na mtaweza kumwaga damu
Kwa mfano wewe ni mwanaume na unaishi na mwanamke ambaye unampa kila kitu kama chakula, nguo, matibabu,unampa msaada wa kifedha,unamnunulia zawadi kibao n.k lakini amekuwa kero kwa lawama na malalamiko kuwa humpendi,humjali, humsikilizi,humshirikishi kwenye mambo yako na anadai wewe ni mbinafsi sana
Kwa sababu ya kiburi unaweza kumpiga au kumtukana matusi ya nguoni na kuanza kujihami kuwa unampenda na kumjali na kumpa mahitaji kibao ila hana shukurani
Hilo ni kosa kwa sababu kwanza hawezi kukaa kimya bali atazidi kuwa jeuri na kuanza kujihami na kutaja makosa kibao ambayo umefanya anaweza kutaja tuhuma za kweli ukapata hasira na kumpiga sana
Unachotakiwa kujua ni kwamba mtu mwenye malalamiko sana huwa anataka kusikilizwa tu sio kupewa msaada,wala ushauri wala kujibizana nae kwa lolote
Ukifanya tofauti tu ujue mnaingia kwnye ugomvi mkubwa sana na mnaweza kumwaga damu
Njia nyepesi akitaja tuhuma zozote juu yako ziwe za kweli au uongo kwanza kubaliana na malalamiko yake ili ajue anasikiliizwa kwa sababu anachotaka ni kusikilizwa sio kuanza mabishano
Huwa wanataka uwasikilize tu sio kujieleza au kupinga tuhuma hizo
Hivyo akisema humjali , humsikilizi, humshirikishi kwenye mambo yako,humpi kipaumbele,humfanyi wa kipekee n.k hata kama huduma zote muhimu unampa usianze kubishana naye au kumpinga kwa tuhuma hizo
Kwenye kila malalamiko huwa upo ukweli ndani yake na watu wengi huwa hawataki kuambiwa ukweli na huo ndio mwanzo wa ugomvi na migogoro ambayo haina mwisho
Akiseme humjali, humsikilizi,humpi kipaumbele,humfanyi wa kipekee n.k mwambie "Ni kweli kwa uyasemayo nimekuwa busy kwa kipindi kirefu,sijaweza kukupa upendo unaostahili,sijaweza kukujali, kukusikiliza wala kukishirikisha kwa mambo muhimu na kama binadamu wengine unayo haki ya kulalamika juu ya hilo na kwa sababu nimesikia malalamiko yako nakuahidi kuyafanyia kazi nipe muda "
Kitendo cha kujishusha hata kama ni mjeuri kiasi gani huwa anakuwa mpole na mnyenyekevu kwa sababu malalamiko yake anaona yamefika sehemu sahihi na kusikilizwa
Ni sawa na waandamanaji wakifukuzwa na mabomu huwa wanaendelea kuleta vurugu lakini wakisikilizwa huacha kelele na maandamano papohapo
Kama ukiwa na ule umimi (EGO) ya kutaka kuwa juu siku zote hii njia kwako haikufai na utaendelea na migogoro kama zamani
Watu wenye tabia ya umimi huwa wanataka kuwa juu na ikiwa ambao unakwazana nao wapo na tatizo hilo hilo ujue mtakesha kwa mabishano na mnaweza kumwaga damu
Mtu mjeuri siku zote huwa anataka kuwa sahihi tu sio vinginevyo
Anasimulia Dr.David Burns kutoka chuo kikuu cha Stanford kwamba siku moja alikutana na mwanasaikolojia mbishi kwenye semina
Kwa maana walikuwa kwenye semina ya mahusiano jinsi ya kudumisha uhusiano kwa wanandoa
Kila kitu ambacho Dr.David Burns aliongea yule mwanasaikolojia alikuwa anakosoa tu kwa lugha mbaya ili kumfanya aonekane hajui chochote mbele ya watu kwenye semina
Kitendo cha kumjibu kuwa hujui lolote,unaongea hoja hazina mashiko na kutaja dosari kwa kila kitu ilikuwa changamoto sana kwa Dr.David Burns
Lakini Dr.David Burns aliweza kumdhibiti kwa kumkubalia kila hoja na tuhuma kwa kuzifafanua zaidi
Pale mkosoaji aliposema umezungumzia mahusiano lakini hujagusia kuhusu wivu hivyo hoja zako hazina mashiko
Dr.David Burns aliweza kumdhibiti kwa kumwambia "Upo sahihi unachosema ni kweli kabisa kuwa kama mtu ameelezea mahusiano bila kugusia suala la wivu anakuwa ameacha hoja ya msingi sana"
Kitendo cha kumuunga mkono mkosoaji na kufafanua vizuri hoja za mkosoaji kiliweza kuvunja nguvu ya mkosoaji
Kwa mfano mwingine kuna mtu anadai wewe ni mbishi ukianza kusema wewe sio mbishi maana yake unathibitisha kwamba wewe ni mbishi kweli
Njia ya kumshinda ni kumwambia "upo sahihi kwa hicho usemavyo na nimekuwa mbishi kwa kipindi kirefu hata kwa mambo hayana mashiko"
Ukifanya hivyo unakuwa umebadilisha mjadala kuwa mazungumzo na unakuwa mshindi kirahisi
Mtu mjeuri hawezi kushindana na mtu mnyenyekevu hata siku moja
Kama mtu ni mjeuri ukiwa mnyenyekevu anainua mikono juu yeye mwenyewe bila kupenda
Mwisho wa makala asante kwa kusoma mpaka mwisho wa makala yetu karibu kwa maswali maoni na ushauri ikiwa una tangazo unahitaji tukutangazie Humu Bonyeza hapa Wasiliana nasi kwa Email kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇
Bonyeza hapa Download App ya MAHABA |
Makala nyingine
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Video Jifunze haya mwanaume Hawezi kuchomoka
Sababu kubwa inayo sababisha mwanaume Kupunguza mapenzi kwako
Fursa ya kujiajiri kupitia blog
Tambua sababu zinazo sababisha wanawake wengi kuachwa na waume zao
0 Maoni