Ticker

6/recent/ticker-posts

MAMBO 4 YA KUFANYA NYAKATI UNAPOHISI KUKATA TAMAA

 


MAMBO 4 YA KUFANYA NYAKATI UNAPOHISI KUKATA TAMAA


Kukata tamaa ni kawaida hasa maisha yako yanapokuonyesha kila dalili ya kufeli mipango yako na kila juhudi unafanya haileti matokeo mazuri

Kuna kitu huitwa Overthinking na kuna kitu huitwa Deep thinking

Watu wengi huwa wanafanya overthinking kwa maana wanafikiria sana matatizo yao bila kufikiria ufumbuzi hivyo huchanganyikiwa haraka na kupoteza matumaini

Wachache hufanya deep thinking kwa maana kufikiri sana nini tatizo,chanzo,na suluhisho la matatizo

Unatakiwa kutafuta ufumbuzi wa matatizo sio kulalamika kuhusu matatizo au kuanza kulaumu wengine kama chanzo 

Kwa vyovyote itakavyokuwa kama ukianza kumkosoa mwenzio,kulaumu wengine,kutuhumu wengine kama chanzo cha tatizo kamwe huwezi kupata ufumbuzi bali utajenga chuki na utazidi kuteseka kwa hasira 

Mambo 4 ya kufanya KUEPUKA kukata tamaa
1.TAZAMA MAKOSA YAKO 
kwa kawaida watu siku zote hutazama makosa ya wengine ili kupata nguvu ya kuwasema vibaya na wao kuonekana malaika

Ukweli ni kuwa huwezi kubadili tabia ya mwengine hata kama amefanya kosa waziwazi kwanza asili ya binadamu ni kukataa makosa hata kama kila mtu ameona 

Kama ukitazama ubaya wa maamuzi yako utaona sehemu ya kurekebisha lakini ukitazama ubaya wa wengine utaishia kuwalaumu tu 
Mtu yeyote hata kama amefanya makosa hadharani ukianza kumlaumu atakuja juu kujihami na kutaja ubaya wa makosa yako ambayo ulifanya zamani badala ya kukiri kosa lake 

Kama ni kwenye mahusiano na umeanza kubishana na mwenzio utaeelezaa makosa yaje yote na ikiwa ni ya kweli kama akikosa hoja atasema "Hujui unacho kiongea"

Au atasema huna cha kuniambia ,kaa kimya huna jipya n.k kwa lengo usimkosoe kwa makosa yake 

Watu wote kwa ujumla wakifanya makosa huwa hawataki kukosolewa bali huwa wanakuja juu kujihami

Kama unaelezea hoja ya wazi na ushahidi upo wazi na mwenzio anakujibu kwa jeuri kuwa hujui ambacho unaongea utazidi kupata hasira na utaanza kulalamika na kumshambulia kwa maneno makali sana

Kitendo cha kulaumu sana huzaa mabishano na mijadala ambayo huleta chuki na kuibua siri nzito ambazo zinaweza kusababisha kuvunjika kwa mahusiano yenu 

2.TAFUTA UFUMBUZI WA MATATIZO
Kama umeona makosa yako anza kwa kutazama wapi uanze kurekebisha 

Badala ya kutazama ubaya wa watu wengine tazama ubaya wako 

Kutazama ubaya wa tabia zako ni jambo gumu sana na watu wengi huwa wanakosa uvumilivu

Kama kulizuka mjadala na mabishano kati yako na watu wengine hata kama ilikuwa miaka kibao nyuma bado msimamo wako ni kuwa wewe ulikuwa sahihi na mwengine hakuwa sahihi

Kama tatizo lipo nje ya uwezo wako liache kisha tumia muda huo kujifunza tabia mpya za uvumilivu

Kipindi huoni matokeo mazuri ndio watu hujifunza uvumilivu

Huwezi kuwa mvumilivu kama maisha yako yanakuja vile umepanga na utagundua kuwa kiburi huletwa na mafanikio ya haraka bila kupata vikwazo 

Kama maisha yako yanakuja vile umepanga huwezi kuwa mvumilivu wa makosa ya wengine na vilevile huwezi kuona ubaya wako 

3.MSAIDIE MTU MWENYE MATATIZO
Binadamu huteseka sana kama muda mwingi anafikiria nini apewe badala ya nini atoe kwa wengine

Utagundua kuwa wale watu ambao huwa wanataka kupewa huduma za kipekee sana huteseka sana kwa malalamiko

Kusaidia mtu mwenye maumivu huondoa chuki kwako na kukupa hamasa ya kuendelea kupambana

Binadamu hukata tamaa kwa kujiona hana thamani kwa wengine 

Lakini kama utafanya jambo lenye kuonyesha kuwa unaweza kugusa maisha ya mtu yeyote utaona unapata nguvu 

Kama utakuwa huna tabia ya kusaidia watu utakuwa na ile hali ya kupoteza mood ya kazi mara kwa mara

Kuacha kusaidia watu huleta chuki kwako na kukufanya ukose uvumilivu

Kama huna tabia ya kuangalia makosa yako utakuwa bingwa wa kusema ubaya wa tabia za wengine

Ukiona mtu hana desturi ya kukosoa tabia za watu ujue ameona mapungufu yake ya tabia 

Kama huoni makosa yako na ubaya wako kwa wengine huwezi kukiri kosa hata siku moja na mara nyingi utakuwa bingwa wa lawama kwa wengine

Ukigundua kuwa huwa unaumiza hisia za watu kamwe huwezi kumshambulia mwengine kwa tabia ya kulaumu mwenendo wake

Kama huoni sehemu ambazo unaumiza hisia za watu siku zote utakuwa unateseka kwa sababu ya ubaya wa tabia za wengine

Kama unajua kuwa huwa unafanya makosa hata wengine wakifanya makosa huwezi kuwajia juu utakumbuka jinsi ambavyo umefanya kama wao 

4.THIS TOO SHALL PASS
Hakuna kitu chenye kudumu 
Furaha huwa haidumu na huzuni huwa haidumu

Kama upo na matatizo ya kifedha kumbuka ni kipindi cha muda tu 

Usiwe serious sana na maisha kwa sababu maisha siku zote huleta maumivu kwa vitu ambavyo unavicchukulia serious sana 

Watu tunaowapenda huondoka na kutuacha 

Kazi ambazo watu hujitoa muhanga sana kuzifanya huwa wanaziacha 

Pesa watu hutafuta kwa nguvu lakini hawadumu nazo siku zote 

Hakuna kitu ambacho utadumu nacho siku zote 

Afya yako HUBADILIKA,sura yako hubadilika,tabia zako hubadilika
Malengo yako hubadilika
Kipato chako hubadilika
Morali ya kazi hubadilika


Hata kama unapitia hali ngumu sana kumbuka hicho ni kipindi cha mpito tu 

Hasira huwa zinakuja na kuondoka zenyewe kama ukiacha kuziondoa kwa nguvu 

Watu wanakusema kwa mabaya leo kesho wanakwenda kumsema mwengine 

Watu leo wanakusifia sana kesho watamsifia mwengine 

Kwa kifupi kila kitu ni cha mpito tu

Mahusiano yako yenye kukufanya ujione bora sana huwezi kuyafurahia siku zote 

Cheo huwezi kukifurahia siku zote 

Kuna watu watakuja kwako na kisha wataondoka hilo ni jambo la kawaida

Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();