Changamoto hatuwezi kuziepuka japokuwa hakuna ambaye hajapata kuishi bila changamoto lakini zikitokea utaona watu wanakuwa na taharuki
Binadamu huwa anaishi kwa mazoea ya siku zilizopita hata kama atajilazimisha kujenga tabia mpya bado atapata ugumu kuziondoa tabia za zamani
Ubongo wa binadamu hauwezi kubadilika ghafla hivyo huwa inachukua muda mrefu kujenga tabia mpya na kuifanya sehemu ya mazoea
Kama leo umevunjwa moyo kwa mtu kukusema vibaya kesho ukisemwa vibaya utaumia na kesho kutwa ukisemwa vibaya utaumia
Kama leo unalalamika sana kuhusu ubaya wa tabia za wengine kesho pia utalalamika na kesho kutwa pia utalalamika kama kitendo kilekile kikirejewa
Hali ya kulalamikia kama maisha yamekuja tofauti huwa inakuja automatically bila kujizuia kama umekuwa mwenye kulaumu kwa muda mrefu
Kama ukiona mtu anasaidia sana watu bila hata kuombwa misaada huwa ni kwa ya mazoea ya muda mrefu ya kufanya kitendo hicho
Kama ukiona mtu hawezi kusamehe makosa ya watu hata makosa madogo madogo ni kwa sababu ameishi kwa kubeba chuki muda mrefu hivyo anapata ugumu kusamehe
Hii ndiyo sababu kama mtu akiambiwa samehe na hajawahi kusamehe anaona ni kitu ambacho haliwezekani
Wala hutakiwi kubishana na mtu kama akisema kitu tofauti na mtazamo wako kwa sababu kila mmoja huona vitu kwa mujibu wa imani yake
Kama humuamini mtu hata akijitetea kiasi gani na akitoa ushahidi kiasi gani huwezi kumuamini sio kwa sababu anaongea vitu havieleweki Lah ni kwa sababu ya mazoea yako kwa mtu huyo
Hivyo tambua kuwa kama usipojiandaa kukabiliana na matatizo endapo ukipata matatizo utapaniki na kufanya maamuzi kwa hisia badala ya akili
Kama akili haipo kwenye utulivu huwezi kufanya maamuzi sahihi
Wapo watu hata wakifanyiwa uadui bado huendelea kuwafanyia wema maadui zao sio rahisi kwa sababu chuki huwa inakuja automatically kama ukivunjwa moyo
Ili uweze kuwa na utulivu kipindi unapokea taarifa mbaya labda kukosolewa,kutukanwa,lawama,kejeli,mafumbo n.k unatakiwa kukabiliana na hali hizo kwanzia sasa sio kusubiri matukio makubwa ndio ujaribu kamwe huwezi na hutaweza
Watu huchukua mafunzo
ya kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi kipindi
hakuna ajali na ikitokea
ajali ndio hutumia
fursa hiyo kuonyesha ubora wao lakini kama
wakisema wajifunze kutoa huduma ya kwanza
kipindi cha ajali
wanakuwa waechelewa
Huwezi kujifunza kukabiliana na lawama kipindi umefanya makosa makubwa
Huwezi kukabiliana na kuvunjwa ahadi kipindi ahadi kubwa imevunjwa
Huwezi kujifunza kukabiliana na hasira kipindi umefanyiwa uadui mkubwa sana
Ili uweze kujenga uwezo wa kukabiliana na tatizo lolote anza na matatizo madogo madogo kisha ukiwa na uzoefu utaweza kukabiliana na matatizo makubwa
Wapo watu huishi kwa kutegemea ipo siku watakuwa na uwezo wa kukabiliana na matatizo makubwa haiwezekani
Utafanya maamuzi kwa mazoea yako sio kile umesoma kwenye maandiko
Tumia muda mwingi kufanyia kazi yale unajifunza ili iwe sehemu ya tabia yako
Kama unataka kufanya kitu kwa ubora fanya iwe sehemu ya tabia yako
Kupata matatizo ni kawaida kabisa japokuwa watu wengi hupata hasira
Hasira haiwezi kusaidia chochote kukabiliana na matatizo
Hasira huwa inafanya mtu kutafuta njia za mkato na mwisho wa siku unajuta sana kuliko mwanzo
Kama ukitumia nguvu na hasira kukabiliana na matatizo utajuta baadaye
Watu wazima hujikuta na tabia kama ya watoto wadogo kwa kuishi huku wanatarajia mambo mazuri tu kuwatokea
Kuishi huku unatarajia vitu vizuri tu kukutokea ni kujitafutia maumivu bure
Lazima ujue kuwa matatizo lazima yawepo bila hata mualiko
Ukiwa makini sana utagundua kuwa kwenye maisha huwa ni hatua mbili mbele na hatua moja nyuma yaani hatuendi moja kwa moja
Uwezo wako wa kujiandaa kukabiliana na vikwazo utakupa furaha ya kudumu na utaishi bila lawama kwa wengine
Njia tatu za kukabiliana na kila changamoto
1.BADILISHA KILE KIPO NDANI YA UWEZO
Kama unatatizo jiulize kama lipo ndani ya uwezo kama lipo ndani fanya haraka kukabiliana nalo
Ikiwa huwezi kukabiliana nalo jifunze jinsi ya kukabiliana nalo huku ukiwa unavuta subira
Kama tatizo linahitaji maarifa basi tafuta maarifa
Kama pesa ndio suluhisho tafuta pesa
Kama talaka ndio suluhisho tumia talaka
Kama tatizo lipo nje ya uwezo basi hilo sio sehemu ya wewe kuteseka
2.ACHA KILE HUWEZI KUDHIBITI
Huwezi kudhibiti tabia za wengine,. maamuzi ya wengine,imani za wengine,maoni ya wengine,hisia za wengine,watu kukupa ushirikiano
Huwezi kudhibiti sheria za nchi
Huwezi kudhibiti hali ya hewa
Huwezi kudhibiti mporomoko wa uchumi n.k
Hivyo kitu chochote ambacho sio sehemu ya maamuzi yako kiache kisikutese bure
Kama kuna mtu amevunja ahadi sio kosa lako
Kama kuna mtu amekusaliti sio maamuzi yako
Kama kuna mtu hajajibu sms sio maamuzi yako
Kile hujapanga wewe kitokee kiache kisikutese
3.TARAJIA MATATIZO
Tarajia kuna mtu atavunia ahadi,tarajia kuna mtu ataonyesha utovu wa nidhamu,
Tarajia huduma kuchelewa
Tarajia wateja kukulaumu hata kama huduma zako ni nzuri
Tarajia watu uliowapa pesa watachelewa kurejesha
Tarajia sheria za nchi kubadilika na kuwa ngumu
Tarajia kupata wagonjwa
Tarajia kupokea taarifa mbaya
Tarajia watu unaowaamini kukusaliti na kukuonyesha tabia tofauti
Kama ukifanikiwa kujenga tabia ya kutarajia watu kufanya makosa huwezi kuwalaumu
Tarajia watu kukuvunja moyo,tarajia wapendwa wako kufanya makosa ikiwa unajua watafanya makosa huwezi kushangaa wakifanya makosa kwelikweli
Mwisho wa makala asante kwa kusoma mpaka mwisho wa makala yetu karibu kwa maswali maoni na ushauri ikiwa una tangazo unahitaji tukutangazie Humu pia
*BADILI MAISHA*
*Ukitaka kufahamu njia ya kutengeneza Dora 100 mtandaoni kwa mtaji wa Sh:35,000 njoo inbox nikupe huo mchongo*Whatsapp
kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇
Bonyeza hapa Download App ya MAHABA |
Makala nyingine
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Video Jifunze haya mwanaume Hawezi kuchomoka
Sababu kubwa inayo sababisha mwanaume Kupunguza mapenzi kwako
Fursa ya kujiajiri kupitia blog
Tambua sababu zinazo sababisha wanawake wengi kuachwa na waume zao
0 Maoni