UKWELI HALISI..
JIFUNZE HAYA ULINDE NDOA YAKO/UCHUMBA WAKO
1. Ukiwa Kama mwanamke, pale panapotokea maudhi dhidi ya mpenzi wako, nyamaza kimya, ukimya wa mwanamke humsumbua akili mwanaume. Atahisi kuna jambo fulani kichwani mwako na kama anabusara atatafuta njia ya kusuruhisha. Usiwe mtu wa tit-for-tat.
2. Kama atakutumia ujumbe wa maudhi katika simu, usimjibu kwa maneno ya kuudhi pia. Muandikie "Samahani" au "Asante sana."
3. Hakuna mwanaume anapenda mwanamke anayemrudishia maneno, kama wewe ni mke uliye na busara, funga mdomo wako. Pale atakapokuwa ametulia ongea nae mmalize mgogoro.
4 Usiringie uzuri wako. Hujawaona wanawake wazuri wengi tu bado wako single, huvaa nguo za kuacha miili yao wazi, ziwa linaonekana wazi bila kujua wanaume hawapendi hivyo nao wanaishia kuwa wezi wa waume za watu na uzuri wao kama wameshushwa toka mbinguni? Tabia yako itakuhifadhi katika moyo wake.
5. Kamwe usimfananishe na EX wako au mwanaume mwingine, huwezi jua huyo mwanaume nae ana mapungufu gani katika mahusiano yake. Binadamu hatuko 'perfect' na hatufanani.
6. Usiwe wa kupokea tu, mnunulie chochote, haijalishi kama anavyo vingi au ni kidogo sana, ila kilichotoka kwako siku zote kina umuhimu mkubwa kwake.
7. Kuwa mwanamke mwenye mawazo 'mtambuka' usifikirie jambo moja tu, mshauri masuala ya maendeleo, miradi, kununua vip-longa na mengineyo. Usiwaze habari za kucha, nywele, mapochi na shopping za kibabe pekee, nguo za kuacha miili wazi kama hivi kwenye picha hii!!! Hayo mambo kwa mwanaume yamepita kushoto. Na ni ya ziada tu.
8. Mheshimu yeye pamoja na familia yake, usidharau wadogo zake, dada zake na kaka zake, hana namna hao ndio ndugu zake na kimbilio alilo nalo, hata kama hawana hali nzuri.
9. Mambo madogo ila yana maana kubwa, mpigie simu, kamwe usisubiri yeye ndio akutafute. Mapenzi ni 'two way traffic'
10. Jithamini wewe kwanza na yeye atakuthamini.
11. Kwa kuwa hana ukwasi leo, haimfanyi kuonekana ndio atakuwa na ukata milele, tizama sana ni nini kinamuendesha kichwani mwake. Tizama sana mawazo yake chanya na njaa ya kutafuta mafanikio. Ila kama yeye awaza ngono na pombe tu, hilo ni jipu uchungu.
12. Kama utashindwa kuibadili tabia yake hivi sasa mkiwa kwenye mahusiano, am sorry katika ndoa itakuwa vigumu sana kumbadili, au utatumia maisha yako yote kumbadili. Hapa inahitaji moyo kweli kweli! Usikubali tendo la ndoa kabla ya Ndoa
13. Kama mpo katika mahusiano tu na amekuwa akikupiga ukikosea jambo fulani. Sorry pale utakapoolewa nae chumba chenu kitageuka kuwa ulingo wa masumbwi.
14. Kila muda amekua akikutishia kukuacha, unalia na kumwambia kama akikuacha utakufa...hahahaaa nani amekwambia? Mtu sahihi kwako kutamka maneno kama hayo ni vigumu kinywani mwake. Huyo hakufai anakuchukulia faida.
15. Jiulize nafsini mwako, tokea umeanza mahusiano nae, kuna mchango wowote chanya katika maisha yako amekuletea? Aitha kiroho, kiakili, na kiuchumi. Kama bado hebu tafakari tena upya kama anakufaa. Kusomeshwa na mchumba ni hatari sana
MAOMBI YANGU KWAKO
Mwenyezi Mungu akufungue macho katika mahusiano yako, na kama bado hujapata akuongoze vema ukampate yule aliye sahihi, maana lengo la mahusiano sio kuumizana kihisia, bali ni kuziunganisha furaha zetu tulizokuwa nazo hapo mwanzoni kabla ya mahusiano na kutengeneza furaha kubwa zaidi.....
AMEN!!
Mwisho wa makala asante kwa kusoma mpaka mwisho wa makala yetu karibu kwa maswali maoni na ushauri ikiwa una tangazo unahitaji tukutangazie Humu pia
*BADILI MAISHA*
*Ukitaka kufahamu njia ya kutengeneza Dora 100 mtandaoni kwa mtaji wa Sh:35,000 njoo inbox nikupe huo mchongo*Whatsapp
kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇
Bonyeza hapa Download App ya MAHABA KWA HABARI ZA BISHARA NA BIDHAA MPYA TAZAMA MAUZO TV |
0 Maoni