Niko kwenye mahusaino na huyu Dada huu ni mwaka 5, nilikua nampenda sana na nilishapanga kumuoakabisa, kila kitu kilikua vizuri, mwaka jana tulikubaliana abebe mimba kabla ya ndoa kwani nilikua na hamu sana ya mtoto na bado tulikua hatujajipanga kuhusu mambo ya ndoa.
Kweli alikubali, yeye alikua ni Mwalimu anafanya kazi mkoani, kutokana na umbali na tulishakubaliana kuwa nikimuoa basi yeye atafanya Biashara na mimi ndiyo nitaajiriwa kwani na mimi ni Mwalimu serikalini basi alipokaribia kujifungua aliaha kazi, alienda kwetu kujifungua mpaka sasa hivi yuko kwetu.
Mambo yalikua mazuri lakini kuna kipindi yuko kwetu nilianzisha mahusiano na Dada mmoja ambaye naye tunafanya naye kazi, katika mahusino nilimuona kama ana akili ya maisha, ni mchaprikaji nikajikuta kuwa nampenda yeye zaidi. Tulichukuana na wkenda kufunga ndoa ya serikalini, mimi ndiyo nilimuambia kuwa nina haraka.
Sababu ya kuja kwako ni hivi, X wangu yeye bado yuko kwa Mama kila akitaka kuja namuambia kuwa bado kuna mambo najipanga lakini ukweli nikuwa natafuta namna ya kumuacha. Shida ni mke wangu, anataka tuende kwetu kwanza kwnai hakuna ndugu yangu hata mmoja anamfahamu au anajua kuwa nimeoa.
Naomba unsiaidie, namuondoaje yule mwanamke kwa Mama, sio kama nimemuacha au sitamhudumia, hapana nitaendelea kumhudumia mpaka apate kazi nyingine kwani ana mwanangu. Shida ni huyu niliyenaye, akijua kuwa nina mwanamke mwingine ana mtoto wangu sijui kama atachukuliaje, naomba ushauri wako!
NB: *Dada zangu upendo upo ila mambo yanabadilika!* OMBA DAIMA.
|
Makala nyingine
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Video Jifunze haya mwanaume Hawezi kuchomoka
Sababu kubwa inayo sababisha mwanaume Kupunguza mapenzi kwako
Fursa ya kujiajiri kupitia blog
Tambua sababu zinazo sababisha wanawake wengi kuachwa na waume zao
0 Maoni