Bonyeza hapa Download App ya MAHABA |
MONALISA
SEHEMU YA: 11
Monalisa baada ya kumaliza kumfanyia shopping ya mavazi baba yake wakaingia kwenye gari na sasa Monalisa akawa anataka kujua nini kilipelekea Mzee Mussa kuwa na maisha haya. Mzee Mussa akamtaka Monalisa warudi kwanza kule hotelini halafu ndio atamwambia kila kitu kilichotokea katika maisha yake mpaka yeye kutengana na mke wake (Bi Sophia) na pia vile walivyomkuta na Yale maisha yake ya kifukara! Monalisa alifurahi sana kusikia hivyo akaiondoa gari yake na safari ya kuelekea Sinza kule hotelini alikompangia baba yake ikaanza. Wakiwa wapo ndani ya gari waliendelea kuongea mazungumzo mbalimbali na Monalisa akamgundua Mzee Mussa ni mtu mcheshi na mkarimu tofauti na pale mwanzo alivyokuwa anamchukulia.
Baada ya mwendo wa nusu saa tayari wakawa wameshafika pale hotelini Monalisa akamsaidia baba yake kushusha ile mizigo waliyonunua huko mjini walipotoka na halafu wakaenda mpaka pale mapokezi ili kuchukua ufunguo wa kuingilia kule chumbani na kumkuta yuleyule muhudumu ambaye aliwapokea ile siku ya kwanza walimkuta ameketi kwenye kiti chake akiwa bize na simu yake akipekua kwenye mitandao ya kijamii. Muhudumu kwanza akashangaa sana kumuona Mzee Mussa huyu wa sasa ni tofauti na yule ambaye alikuja Jana yake akiwa mchafu wa mavazi na mwili wake kiasi cha kumchukulia kama ni mtu mwenye uwendawazimu! Mzee Mussa huyu wa sasa alipendeza sana. Monalisa ndio akachukua ufunguo na kisha hao wakapanda ngazi kuelekea juu ghorofani kilipo chumba na huku nyuma wakimuacha yule muhudumu wa kike akiwaangalia huku bado akiwa aamini Kama ni kweli yule mtu ambaye Jana alikuja mchafu na leo anaonekana kuwa ni mtanashati mawazoni mwake alijua kuwa yule mtu na Monalisa kuwa ni wapenzi. Kwa sababu Monalisa alipomuandikishia baba yake hapa hotelini akuweka wazi uhusiano wake na baba yake upoje!
Baada ya kufika chumbani Monalisa akaenda kuketi kwenye sofa kubwa la watu wawili lililokuwa mle chumbani na moja kwa moja Monalisa akamtaka baba yake amsimulie sasa kisa na mkasa jinsi ilivyokuwa. Mzee Mussa baada ya kuweka mizigo yake ya nguo na viatu alivyonunuliwa na mwanae Monalisa akajiweka vizuri na kuketi kitandani na kisha akasema: "Kwanza mwanangu nakushukuru sana, kwa haya yote uliyonifanyia ya kuniweka sehemu nzuri kama hii na kunifanyia yote haya uliyoyafanya! ." Mzee Mussa alisema. "Usijali baba hiyo mbona ni kawaida tu, na ni wajibu wangu mimi kukufanyia hivyo baba wala usijali .." Monalisa alimwambia baba yake. "Nafurahi kusikia hivyo mwanangu, kwanza sikutegemea kabisa kama wewe ungenikubali mimi baba yako na ufukara huu nilionao! .." Mzee Mussa alisema huku akitabasamu. "Kwanini nikukatae baba yangu, na ikiwa mama yangu tayari ameshanithibishia kuwa wewe ndio baba yangu mzazi? .." Monalisa alisema na baada ya hapo sasa akamtaka baba yake amueleze huo ukweli uliojificha kuhusu maisha yake! Mzee Mussa kwanza akashusha pumzi halafu akasema: "Mwanangu kwanza nasikitika kuona hata jina lako nililokupa wakati upo mdogo wamekubadilisha, na sasa unaitwa Monalisa! .." Mzee Mussa alisema kwa huzuni kubwa. Monalisa alishtuka sana halafu akamuuliza baba yake: "Kwani baba mimi nilipokuwa mdogo nilikuwa naitwa nani? ." Mzee Mussa akacheka kidogo halafu akasema: "Kuhusu hilo jina lako la utotoni mwanangu leo sitakuambia, labda ukamuulize mama yako yeye atakuambia kuwa ulikuwa unaitwa nani utotoni! .." Monalisa ikabidi awe mpole tu maana huyu mtu mwenyewe Mzee Mussa anaonekana ni mtu mwenye misimamo yake. "Sawa baba haina shida, haya sasa niambie hayo mengine uliyoahidi utaniambia tukifika hapa ." Monalisa alisema. "Kwanza mwanangu inabidi tukubaliane, kuwa haya nitakayokueleza hapa usiyawekee chuki kwa mama yako na pia kwa huyo baba yako aliyekulea umenielewa? ." Mzee Mussa aliuliza kwa msisitizo. "Nimekuelewa baba ." Monalisa alijibu kwa unyenyekevu. "Maisha yangu yameharibiwa vibaya na huyo mtu anaeitwa Mr Brown ambaye ndie amekulea wewe, na kujifanya yeye ndio baba yako! .." Mzee Mussa aliongea kwa uchungu mwingi sana! Monalisa alibaki kimya anamsikiliza. "Ameninyang'anya furaha yangu, ambayo ni wewe pamoja na mama yako kwa sababu ya nguvu yake ya pesa alizonazo! ." Mzee Mussa bado aliendelea kutiririka huku machozi sasa yakianza kumtoka machoni kwake! "Amenipora mke na mtoto na pia akaona haitoshi, akataka kuniua ili kunipoteza kabisa duniani kwa kuniletea majambazi wanimalize!.." Monalisa bado aliendelea kubaki kimya akimsikiliza kwa umakini huku maneno Yale yakionekana kumuingia na kumchoma. "Lakini mama yako astahili kupewa lawama kwa haya yote yaliyotokea, kwani maisha yetu yalikuwa ni duni sana na Mr Brown alimuahidi kuwa ataishi naye vizuri na kumpa kila anachotaka ili mradi tu waishi wote," Mzee Mussa alisema. "Mr Brown shida yake ilikuwa ni mtoto katika maisha yake, kwani hakuwa na uwezo wa kupata mtoto maishani mwake baada ya kuthibitishiwa hivyo na madaktari licha ya pesa nyingi alizonazo!.." Hapo Monalisa ndio alichoka kabisa! "Huo ndio ukweli mwanangu , tangu niliponusurika kuuawa na majambazi wale wa Mr Brown maisha yangu yalikosa amani na furaha na ndio kama hivi unavyoniona.." Mzee Mussa alisema huku machozi yakimtoka. Monalisa akanyanyuka na kwenda kumfuta machozi baba yake! "Pole sana baba sikuwa najua kama ukweli upo hivyo!.." Monalisa alisema huku na yeye machozi yakimtoka kwa mbali. "Hiyo ndio historia kwa ufupi mwanangu, ukitaka kujua kwa urefu zaidi nenda kwa mama yako atakueleza vizuri.." alimaliza kusema Mzee Mussa! Basi baada ya hapo Monalisa akamuaga baba yake na kumuahidi kuwa atakuja tena jioni kumuona akitoka kwenye shughuli zake, na akaweza kumpa pesa nyingi baba yake za kutumia. Mzee Mussa alimshukuru sana Monalisa na akamsindikiza mpaka chini ya hotel hii na akamsisitiza kuwa asionyeshe chuki kwa mama yake na pia kwa baba yake mlezi (Mr Brown) asiwachukie kwa sababu ya haya aliyomueleza. Baada ya kuagana Monalisa akaingia kwenye gari yake na kuondoka maeneo ya pale hotelini!
Monalisa akiwa yupo ndani ya gari yake akirudi tena mlimani city mawazo bado yaliendelea kukiandama kichwa chake. Yale maneno aliyoambiwa na Mzee Mussa kule hotelini yalimchanganya sana hakuweza kuamini kabisa kuwa Mr Brown mtu aliyemchukulia kama ni baba yake kwa muda mrefu tangu anapata ufahamu hapa duniani kuwa ni mkatili kiasi hicho cha kutaka kuua mtu! Monalisa pia akaweza kukumbuka jinsi ambavyo Mr Brown alivyomlea kwa upendo wa hali ya juu sana na kumpa kila kitu alichokihitaji kama vile nyumba anayoishi kule mbezi beach pamoja na Yale maduka ya nguo mlimani city amepewa na Mr Brown na hata hii gari anayoendesha pia amenunuliwa na Mr Brown baba yake mlezi. Monalisa alipagawa kwa habari alizopewa na Mzee Mussa kuwa Mr Brown hana uwezo wa kupata mtoto maishani kwake na ndio maana akataka kumuua Mzee Mussa kwa wakati huo zamani ili ampate mama yake (Bi Sophia) na yeye Monalisa alipokuwa bado mtoto mdogo! Monalisa alijiuliza ni vipi mama yake alikutana na Mr Brown mpaka wakaanzisha mahusihano, swali alipanga kumuuliza mama yake pindi atakapokutana naye na pia kuhusu hilo jina lake la utotoni nalo alitamani sana kulijua. Safari ikamfikisha Monalisa maeneo ya mlimani city na Monalisa akapigwa na butwaa Mara baada ya kuiona gari ya baba yake mlezi (Mr Brown) imepaki maeneo haya! "Mungu wangu! , ina maana baba amekuja huku? .." Monalisa alijiuliza yeye mwenyewe huku akiipaki gari yake kwenye Maegesho!,
MONALISA
SEHEMU YA: 12
Wakati Monalisa akiwa anarudi tena mlimani city akitokea kule Sinza hotelini alipokuwa Mzee Mussa Monalisa alipigwa na butwaa baada ya kuikuta gari ya baba yake mlezi (Mr Brown) imepaki hapa. "Mungu wangu! Ina maana baba amekuja hapa?.." alijiuliza mwenyewe huku na yeye akiipaki gari yake kwenye sehemu ya Maegesho. Baada ya hapo Monalisa akashuka kwenye gari na kwenda moja kwa moja mpaka dukani kwake ambapo alimkuta Suzzy yupo na Mr Brown huku Mr Brown akionekana kukosa furaha! Monalisa akaingiwa na hofu kwa kudhani labda Suzzy atakuwa amemuambia Mr Brown zile habari zake na yule mtu fukara (Mzee Mussa) ambaye ndie ni baba yake. Monalisa huku akiwa na wasiwasi akamsalimia Mr Brown: "Shikamoo baba.." Mr Brown akaitikia salamu ya Monalisa: "Marhaba mwanangu, utanisamehe kwa kuja ofisini kwako bila taharifa." alisema Mr Brown huku akijilazimisha kutabasamu. 'Hamna baba wala usijali, mbona mara nyingi tu huwa unakuja kwa kunishtukiza kama hivi leo.." Monalisa akasema huku na yeye akitabasamu basi wakaongea maneno mawili matatu pale kisha Mr Brown akamwambia Monalisa: "Samahani binti yangu, nilikuwa na maongezi muhimu na wewe naomba twende kwenye gari tukazungumze .." Monalisa aliposikia hivyo moyo wake ukashtuka sana akawa anajiuliza ni mazungumzo gani tena hayo! "Sawa baba hakuna tatizo, tunaweza kwenda.." alisema Monalisa huku moyoni akionekana kukosa amani kabisa. Basi wakamuaga Suzzy na kisha wakatoka mpaka nje kabisa ya mjengo ule wa pale mlimani city Mr Brown akapendekeza maongezi yao wakayafanyie kwenye gari yake na Mr Brown Baada ya kufungua milango ya gari yeye na Monalisa wakaingia ndani yake. Mr Brown akawasha gari na kuiacha ikiunguruma kisha akawasha A/C (Kiyoyozi) na bila kupoteza muda akaanza kuongea: "Narudia tena mwanangu, kukuomba samahani kwa kukujia huku ofisini kwako..." Mr Brown aliongea! "Jamani baba mimi si nimeshakuambia, kuwa usijali baba yangu?.."Monalisa alisema. "Ok nashukuru kusikia hivyo binti yangu, kitu chenyewe ni hivi nilikuwa naomba kujua Jana usiku wewe na mama yako mlienda wapi?.." Mr Brown aliuliza huku akimkazia macho yake Monalisa, Monalisa ghafla akajikuta ameingiwa na mchecheto hata akujua amjibu nini huyu baba yake mlezi. "Kwanini umeniuliza hivyo baba?." Monalisa alijikuta anauliza swali bila kutoa jibu la swali aliloulizwa! Mr Brown akacheka kidogo kisha akasema: "Hapana mwanangu mimi nimekuuliza hivyo nataka kujua tu." Mr Brown alisema huku akiuona waziwazi mchecheto aliokuwa nao Monalisa. "Kwani mama alikuambia tumeenda wapi?" Monalisa aliuliza, kitendo hicho kilionekana kumkera Mr Brown. "Yaani Monalisa mimi nakuuliza swali badala ya kunipa jibu, na wewe tena unaniuliza swali Why?." Mr Brown alifoka! Monalisa aliogopa sana kwani akujua mama yake alimjibu nini baba yake juu ya ile safari yao ya Jana kule manzese midizini na pia aliingiwa na hofu kuhusu Suzzy kuwa labda naye atakuwa ameulizwa swali hilo na Mr Brown pale alipowakuta muda ule na akujua naye amejibu nini. Monalisa alijikuta anachanganyikiwa! "Kwahiyo umekosa jibu la kunipa si ndio?." Mr Brown aliuliza na kumshtua Monalisa kwenye mawazo, "Sio hivyo baba .." Monalisa alisema. "Sio hivyo nini sasa? nijibu basi jana usiku mlienda wapi?." Mr Brown alikazia tena swali lake. Monalisa alibaki kimya akashindwa kujibu! "Ok naona swali limekuwa gumu, basi ngoja mimi niondoke zangu nirudi ofisini lakini hilo swali unitafutie jibu lake!." alisema Mr Brown kwa msisitizo na baada ya hapo wakaagana na Monalisa akashuka kwenye gari na Mr Brown akaondoka zake na kumuacha Monalisa akiwa na mawazo lukuki kichwani mwake!
Mr Brown baada ya kuachana na Monalisa na sasa akiwa yupo ndani ya gari yake akienda ofisini kwake, Mr Brown akachukua simu yake na kupiga Sehemu. Haikuchukua muda simu yake ikapokelewa na sauti nzito na yenye kukwaruza kama spika ya redio mbovu! "Aloo boss wangu niambie!.." Ilisema ile sauti nzito kutoka upande wa Pili wa simu, "Kuna kazi nataka uianze leo jioni ya kumfuatilia yule binti yangu Monalisa kutoka mlimani city na mpaka sehemu anapokwenda, halafu unipe ripoti!." Mr Brown alitoa maelekezo. "Aaahaaah hiyo boss ondoa shaka, mpaka hapo uhesabu kazi imekwisha tayari!.." alijitapa yule mtu mwenye sauti nzito. "Ok nakuaminia Jembe langu, najua hauwezi kukosea kazi!." alisema Mr Brown huku akitabasamu na baada ya kumaliza kuongea na yule mtu mwenye sauti mbaya Mr Brown akakata simu yake na safari ya kuelekea ofisini kwake ikaendelea!
Jioni ilipofika kama kawaida yao Monalisa na Suzzy wakafunga maduka yao na kisha wakaingia kwenye gari na safari ya kurudi nyumbani ikaanza, Lakini Monalisa akakumbuka kuwa alimuahidi Mzee Mussa (Baba yake mzazi) kuwa jioni atamtembelea tena kule Sinza hotelini Monalisa akaona sio mbaya kwanza aende akamuone baba yake. Monalisa akiwa njiani akampigia simu mama yake na kumwambia Yale maswali aliloulizwa na Mr Brown kuhusu Jana ni wapi walipokwenda lakini akumpa jibu! Bi Sophia naye akasema na yeye pia aliulizwa hivyohivyo muda ule wa usiku walipomrudisha nyumbani na akuweza kumjibu kitu Mr Brown, Bi Sophia pia akamsisitiza Monalisa na kumwambia kuwa hiyo waifanye kuwa ni siri na Mr Brown asitakiwe kabisa kuijuà Monalisa akamjibu mama yake kuwa ni sawa amemuelewa hatomwambia. Lakini kwa wakati huo Monalisa na rafiki yake Suzzy wakiwa wapo wanae wanaelekea kule Sinza hotelini kwenda kumuona Mzee Mussa hawakujua kuwa kwa nyuma yao kulikuwa na gari aina ya NOAH ya rangi nyeusi yenye vioo vya Giza ilikuwa inawafuatilia kwa ukaribu sana!!, ITAENDELEA SEHEMU YA 13 ENDELEA
MONALISA
SEHEMU YA: 13
Monalisa na rafiki yake Suzzy wakiwa wapo njiani kuelekea kule hotelini Sinza kwenda kumuona Mzee Mussa hawakujua kama kwa nyuma yao kulikuwa na gari aina ya NOAH ya rangi nyeusi yenye vioo vya Giza ikiwafuatilia kwa ukaribu sana. Ndani ya hiyo gari aina ya NOAH kulikuwa na vijana watatu ambao awakuwa ni watu wazuri na ndio waliagizwa na Mr Brown baba yake mlezi na Monalisa kuhakikisha wanamfuatilia Monalisa nyendo zake zote jioni hii ya Leo kuanzia kule mlimani city mpaka na Sehemu anayokwenda na kisha taharifa au ripoti wampe Mr Brown kama vile alivyoagiza! Baada ya muda Monalisa na Suzzy wakawa wamefika mpaka kwenye hiyo hoteli aliyokuwa Mzee Mussa na Monalisa akaiingiza gari yake ndani ya uzio mkubwa uliokuwa katika hoteli hii ile gari ya watu wabaya ikajifanya kupitiliza na kwenda kusimama mbele kidogo haikuingia ndani ya uzio. Monalisa baada ya kupaki gari yake Sehemu ya Maegesho hotelini hapa yeye na Suzzy wakashuka kwenye gari na kuingia moja kwa moja mpaka ndani kwenda kumuona Mzee Mussa na baada ya kufika chumbani kwake walimkuta Mzee Mussa yupo anaangalia TV alipowaona Monalisa na Suzzy wamekuja alifurahi sana! "Ooho karibuni sana watoto wangu.." alisema Mzee Mussa huku akitabasamu na kuwakaribisha mle chumbani, "Ahsante sana baba shikamoo, na habari za muda?." Monalisa alimsalimia. "Marhaba mwanangu, habari za muda ni nzuri nashukuru Mungu nimeshinda salama sijui nyinyi huko mtokapo?." Mzee Mussa aliuliza, "Huko na sisi pia tu nashukuru ni salama, tumekuja kukuona baba.." Basi baada ya kusalimiana pale waliweza kuongea Maneno mawili matatu kisha Monalisa akamwambia baba yake: "Baba unaonaje usiku huu wa leo tukatoka pamoja tukaenda Sehemu kupata chakula cha usiku halafu tutakurudisha tena hapa!." Monalisa alisema. Mzee Mussa akatabasamu kisha akasema: "Hakuna shida mwanangu, unajua nikiwa na wewe najisikia amani na furaha, kwahiyo usihofu kabisa kuhusu hilo binti yangu.." Basi baada ya Mzee Mussa kusema vile wakatoka mle chumbani na kuteremsha ngazi kushuka chini ya hoteli hii. Suzzy kwa upande wake alishangaa sana kumuona jinsi Mzee Mussa alivyobadilika na kuwa mtanashati kwa mavazi na muonekano mzuri aliokuwa nao hivi sasa tofauti na pale mwanzoni alivyokuwa mpaka wakawa wanamdhania kuwa labda pengine ni mwendawazimu. Basi wakashuka chini ya hoteli hii!
Kule nje ya hoteli wale wakora waliokuwa wametumwa na Mr Brown kumfuatilia Monalisa walibaki wamekaa mle ndani ya ile gari yao wakimsubiri Monalisa atoke ili wajue anaenda wapi tena, wakora au majambazi wale hawakujua Monalisa amefuata nini hotelini hapa hivyo wakampigia simu na kumjulisha boss wao aliyewatuma kazi hii (Mr Brown) na kumwambia kuwa wamemfuatilia Monalisa kutoka kule mlimani city mpaka pale kwenye ile hoteli maeneo ya Sinza Mr Brown akawaambia waendelee kusubiri mpaka watakapomuona Monalisa akitoka hotelini hapo basi wale majambazi wakasubiri. Punde gari ya Monalisa ikaonekana inatoka nje ya geti la hapa hotelini na kumkamata barabara na kuondoka pale hotelini huku ndani ya gari kukiwa na Monalisa na rafiki yake Suzzy pamoja na Mzee Mussa, gari ya wale majambazi nayo ikawaungia kwa nyuma na kuanza kuwafuatilia tena Monalisa mpaka sasa bado ajajua kama kuna watu wapo kazini wanamfuatilia!
Safari yao kutoka kule Sinza hotelini ikawafikisha mpaka kwenye mgahawa mmoja mzuri sana maeneo ya Kijitonyama na baada ya kushuka kwenye gari wakaingia ndani ya mgahawa huo ambao ulikuwa ni mzuri na wa kisasa kwa huduma ya vyakula vyote vizuri na vinywaji, wakatafuta Sehemu nzuri na kuketi ambapo aikuchukua muda muhudumu akawajia na kutaka kujua ni aina gani ya vyakula wangekula baada ya kuangalia kwenye karatasi maalumu vyakula vilivyokuwa kwenye mgahawa huo basi kila mmoja akapata kuchagua aina gani ya chakula akipendacho. Mzee Mussa ikabidi wamchagulie chakula maana yeye hakuwa na uzoefu wa kuja na kuchagua chakula kwenye hoteli Kama hii, baada ya vyakula vyao na vinywaji kuletwa basi wakaanza kula huku wakipiga story mbalimbali na kuonekana wakiwa na furaha wale majambazi nao wakaingia mpaka ndani ya mgahawa huu na wao wakapata kuketi jirani kabisa na pale walipoketi wakina Monalisa majambazi nao wakaagiza pombe Kali na kuanza kunywa huku wakiwa wapo makini na Monalisa. Wakaanza kuwasiliana na Mr Brown kwa njia ya ujumbe mfupi na kumpa habari zote za Monalisa na wakamwambia pia kuwa kumbe kule kwenye ile hoteli ya Sinza Monalisa na Suzzy walienda kumfuata Mzee mmoja ambao wao majambazi hawakumjua ni nani na hivi sasa wapo hapo kijitonyama kwenye mgahawa wakipata chakula cha usiku. Mr Brown akawaagiza majambazi wale wakiwa hapo wafanye juu na chini wampige picha huyo mzee (Mzee Mussa) na kisha picha hiyo wamtumie kwenye mtandao (WhatsAp) ili apate kumjua na kisha awape maelekezo ya nini cha kufanya baada ya hapo! ITAENDELEA
MONALISA
SEHEMU YA: 14
Mr Brown aliweza kuwaagiza majambazi wale wampige picha Mzee Mussa na kisha picha hiyo walimrushie kwa kupitia mtandao wa WhatsAp ili apate kumjua huyo mtu mwenyewe ni nani, sasa kazi ikabaki kwa majambazi wale wakawa wanawaza ni namna gani wanaweza kupiga hiyo picha bila kugundulika waliona hapa ni muhimu kupata hiyo picha na kumtumia Mr Brown kabla hawa wakina Monalisa hawajaondoka kwenye eneo hili la mgahawa kwani endapo kama wakiondoka itakuwa ni ngumu tena kuwapata na wao hawakutaka kwanza kutumia nguvu katika hili jambo la kumfuatilia Monalisa. Jambazi mmoja akapata wazo na kuwaambia wenzake kuwa kwa kuwa mgahawa huu ulikuwa na Sehemu kwa juu kama vile ghorofa basi ni vizuri mmoja aende huko kwa juu na kisha ataweza kupaona chini kwa urahisi na aweze kupiga hiyo picha inayotakiwa na Mr Brown basi kwa haraka bila kuchelewa jambazi mmoja akaenda hiyo Sehemu ya juu ya mgahawa huo ambapo pia kulikuwa na baadhi ya wateja wengine! Baada ya kufika kule juu jambazi yule akaweza kuangalia na kuweza kupaona chini kwa urahisi na pia wakina Monalisa walikuwa wanaonekana vizuri sana, jambazi bila kuchelewa akachukua simu yake kubwa aina smart phone na kupiga picha pale kwenye ile meza waliyoketi wakina Monalisa na Suzzy pamoja na Mzee Mussa picha aliyopiga jambazi yule iliweza kutokea vizuri sana kwani iliwachukua wote watatu kama vile walivyokuwa pale mezani kwao walipokuwa wanakula chakula. Baadhi ya watu wengine walimuona jambazi yule alivyokuwa anapiga ile picha lakini walimchukulia labda anapiga picha tu ya kumbukumbu hivyo walipuuzia na kuona ni kitu cha kawaida, jambazi Baada ya kumaliza kupiga ile picha akashuka mpaka chini na kuwaonyesha wale wenzake picha ile na wakampongeza kwa kupiga picha nzuri kama ile na bila kuchelewa wakamtumia Mr BzisizokuwaMonalisa mpaka sasa bado alikuwa ajajua kitu kilichokuwa kinaendelea hapo Baada ya kumaliza kula chakula Monalisa akalipia bili na baada ya hapo wakatoka nje ya mgahawa ule na kuingia kwenye gari na kuondoka zao kurudi tena Sinza kumrudisha Mzee Mussa kule hotelini na majambazi nao hawakuwaacha bado walikuwa wanaandama kwa nyuma kwa kuwafuatilia tena!
Mr Brown akiwa yupo nyumbani kwake mikocheni alikuwa ameketi Sehemu ya kwenye Sehemu ya bustani huku akinywa Wine ndipo alipoapata mshtuko baada ya kuiona ile picha aliyotumiwa na wale majambazi aliowatuma kazi ya kumfuatilia Monalisa "Shiit ina maana yule kenge kumbe bado ni mzima hajakufa!?," Mr Brown alijiuliza huku akiikazia macho simu yake iliyokuwa ikimuonyesha picha hiyo ambayo Monalisa na rafiki yake Suzzy pamoja na Mzee Mussa walionekana wanakula chakula, Mr Brown alipagawa baada ya kumuona Mzee Mussa kuwa bado yupo hai "Pumbavu kabisa! hapa ni lazima nimpeleke kuzimu huyu mbwa haraka sana!," Mr Brown alisema huku akiwa amejawa na hasira zisizokuwa na kifani na moja kwa moja akawapigia simu vijana wake ili awape maelekezo.
Majambazi wakiwa kwenye gari yao wanawafuatilia wakina Monalisa waliokuwa wanarudi Sinza hotelini kumrudisha Mzee Mussa Mara simu ikaita na mmoja wapo akapokea simu hiyo, "Aloo boss tunasubiri muongozo wako tu," alisema jambazi yule. "Sasa ni hivi huyo kunguni atakiwi kuishi tena duniani, kesho asubuhi na mapema mumfuate hapo hotelini na mumteke halafu mumpeleke kule kinyerezi kwenye nyumba ya siri akamalizwe umenielewa?," Mr Brown aliongea kwa msisitizo, "Ndio boss nimekuelewa tutafanya hivyo unavyotaka boss wetu," baada ya hapo Mr Brown akakata simu na yule jambazi akawaambia wenzake kile alichoambiwa na Mr Brown! Monalisa akiwa hajui hili wala lile safari yao ikawarudisha tena mpaka Sinza kwenye ile hoteli na kumrudisha Mzee Mussa kwa kuwa usiku tayari ulishakuwa mwingi basi awakuongea sana wakaagana pale na Mzee Mussa na kisha Monalisa na rafiki yake Suzzy wakaingia kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea mbezi beach nyumbani kwa Monalisa ikaanza huku wakimuahidi Mzee Mussa kuwa kesho yake asubuhi na mapema watakuja tena kumsalimia, baada ya wakina Monalisa kuondoka na Mzee Mussa naye akaenda chumbani kwake kulala kwenye hii hoteli alikopangiwa na Monalisa!
Alfajiri na mapema kwenye majira ya 11:48 ile gari aina ya NOAH nyeusi ya wale majambazi ikapata kuwasili pale kwenye ile hoteli aliyokuwa amelala Mzee Mussa majambazi wawili huku wakiwa wamevaa mavazi ya kitanashati wakashuka kwenye gari na kuingia moja kwa moja mpaka mapokezi na kujieleza kuwa wameagizwa kumfuata mtu hapa hotelini na walipohojiwa ni nani huyo aliyewaagiza wakamtaja ni Monalisa na wakatoa simu na kumuonyesha picha yule muhudumu waliyemkuta pale ambapo baada ya kuona ile picha iliyopigwa Jana yake usiku kule kijitonyama kwenye ule mgahawa aliweza kumtambua Mzee Mussa na akawatajia mpaka chumba anacholala Mzee Mussa majambazi wakamshukuru sana muhudumu yule na baada ya hapo wakapanda ngazi kuelekea kule kwenye chumba cha Mzee Mussa. Muhudumu hakujua kama wale watu ni majambazi na pale wamekuja kumteka Mzee Mussa ili wakamuue kama walivyoagizwa na boss wao Mr Brown!, ITAENDELEA
MONALISA
SEHEMU YA: 15
Wale majambazi baada ya kuruhusiwa na kuelekezwa na yule muhudumu wa hoteli sasa wakawa wanapanda ngazi na kuelekea chumbani kwa Mzee Mussa ili wakamteke na kwenda kumuua kama walivyoagizwa na boss wao Mr Brown baada ya kukifikia chumba cha Mzee Mussa majambazi wale wakabisha hodi mlangoni na punde Mzee Mussa akafungua mlango na kukutana na sura ngeni kabisa mlangoni pale. "Habari za asubuhi mzee wetu!.." Majambazi walimsalimia Mzee Mussa ambaye bado aliendelea kiwashangaa watu hawa. "Nzuri sijui niwasaidie nini vijana?." Mzee Mussa aliwauliza majambazi wale bila kujua Kama hawa ni wakora. "Tumeagizwa na Monalisa tuje kukufuata anataka kukubadilishia hoteli ya kuishi.." Majambazi walimdanganya Mzee Mussa. "Mbona sina taharifa hiyo na usiku wa jana nilikuwa na Monalisa mbona ajaniambia hivyo..?" Mzee Mussa alihoji, wale majambazi wakaangaliana wakaona hapa wanauweka usiku kwa haraka wakatoa bastora zao na kumuelekezea Mzee Mussa ambaye alishtuka sana Mara baada ya kuona ameelekezewa bastora. "Mzee inabidi uwe mpole na ufuate vile tutakavyokuambia sawa..?" Majambazi waliunguruma na kumuamuru awaingize mle chumbani na wakamwambia abadilishe nguo zake haraka ili waondoke naye kwa sababu walimkuta Mzee Mussa yupo na nguo za kulalia. "Lakini vijana mimi kosa langu ni nini..?" Mzee Mussa alijaribu kuwauliza. "Kimyaa! hautakiwi kujua kosa lako hapa, utaenda kujua huko mbele ya safari.!" Mzee Mussa ikabidi awe mpole kwa Kunyamaza na baada ya kumaliza kuvaa nguo na viatu majambazi wakaamuamuru sasa waondoke mle chumbani, Mzee Mussa akafunga chumba cha hoteli ile na kisha wakaanza kushusha ngazi kushuka chini pia majambazi wakamuonya Mzee Mussa na kumwambia asijionyeshe kama ametekwa watakapofika mapokezi basi wakawa wanatembea kiurafiki kama vile hakuna jambo baya linaloendelea kati yao. Baada ya kufika mpaka mapokezi Mzee Mussa akamkabidhi ufunguo wa chumba yule muhudumu wa ile hoteli na majambazi nao wakamshukuru muhudumu kisha baada ya hapo wakaondoka na Mzee Mussa huku yule muhudumu hakujua chochote kile. Mzee Mussa akawa na mawazo hakujua huko anakopelekwa ni wapi na wataenda kumfanya nini Mzee Mussa pia akamfikiria binti yake Monalisa pindi atakapokuja hapa hotelini na kumkuta hayupo Mzee Mussa akajikuta chozi la kiutu uzima likimdondoka. Wakamuingiza kwenye ile gari yao na majambazi wale wakaondoka naye Mzee Mussa ili kwenda kumuua!
Huku nyuma sasa Monalisa na Suzzy ndio wakawa wanaingia pale hotelini kuja kumsalimia Mzee Mussa baada ya kuteremka kwenye gari Monalisa na Suzzy wakaenda mpaka mapokezi na walipofika pale walipatwa na mshtuko baada ya muhudumu kuwaambia kuwa Mzee Mussa amekuja kuchukuliwa muda sio mrefu na watu waliodai wamegizwa na yeye Monalisa kuja kumchukua hoteli hapa! Monalisa aliishiwa nguvu kabisa. "Jamani mimi mbona sijamuagiza mtu yeyote aje kumchukua baba yangu, wapoje hao watu wenyewe?.." Monalisa alimuuliza yule muhudumu huku akiwa amechanganyikiwa, "Ni wanaume wawili ndio waliokuja kumfuata." alijibu muhudumu. "Walipokuja kumchukua walisema wanampeleka wapi?.." Monalisa alizidi kuhoji. "Kiukweli awajasema wanampeleka wapi, kwani wewe ni kweli aujawaagiza kumfuata?." Muhudumu aliuliza. "Mimi sijamugiza mtu, ningewaagiza ningeuliza hivi?." Monalisa alisema na kuanza kulia machozi kwani kwa vyovyote vile alijua baba yake amekuja kuchukuliwa na watu wabaya na huko walikompeleka wanaenda kumfanyia jambo baya, Suzzy ikabidi am'bembeleze Monalisa na kumshauri waende wakaripoti kituo cha polisi suala lile la kupotea kwa Mzee Mussa na kuchukuliwa na watu wasiojulikana Monalisa kwanza akamwambia Suzzy wasubiri kwani yupo mtu anamuhisi kuhusika na jambo hilo. Basi ikabidi waondoke pale hotelini na kumwambia yule muhudumu kuwa watarudi tena baadae kuja kuchukua vitu vya Mzee Mussa!
Monalisa baada ya kutoka pale hotelini akiwa yupo ndani ya gari yake mawazo yake yakawa yanamuelekeza kuwa ni Mr Brown ambaye ni baba yake mlezi ndio anahusika na hili tukio la kupotea kwa baba yake (Mzee Mussa) Monalisa alijikuta uchungu mwingi sana ukimfukuta ndani ya moyo wake, licha ya rafiki yake Suzzy kumliwaza na kumfariji lakini Monalisa akukubali kupoa kirahisi. Monalisa kwanza alichokifanya ni kumpeleka Suzzy mpaka mlimani city kwenye biashara yao na baada ya hapo bila kuchelewa Monalisa akaiondoa gari yake kwa mwendo wa kasi na kuelekea ofisini kwa Mr Brown kwenda kumpa habari yake Monalisa alijawa na hasira sana na Mr Brown kwani alijua ni yeye ndie muhusika mkuu wa hili jambo na sio mtu mwingine yeyote yule. Monalisa alisimamisha gari nje ya jengo ambalo ndani yake ndio ipo ofisi ya baba yake mlezi (Mr Brown) akapaki gari yake Sehemu ya Maegesho na kisha akateremka na kuanza kuingia ndani ya mjengo ule na moja kwa moja akaenda mpaka ofisini kwa Mr Brown ambapo kwanza alikutana na secretary wa baba yake na kumuuliza kama Mr Brown ameshaingia ofisini, secretary yule kwa vile alikuwa anamjua Monalisa kama ni mtoto wa boss wake akamwambia amefika na yupo ofisini kwake hivyo akamruhusu aingie akamuone. Monalisa bila kupoteza muda akaingia mpaka ndani ya ofisi na kumkuta Mr Brown anaongea na simu alipomuona Monalisa amekuja haraka sana Mr Brown akakata simu ile na kumuangalia Monalisa huku akiwa anatabasamu, Monalisa alimuangalia Mr Brown kwa hasira ya hali ya juu sana!,
ITAENDELEA.Alhamisi Ijayo
Mwisho wa makala karibu kwa maoni kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇
Bonyeza hapa Download App ya MAHABA
Makala nyingine
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Bonyeza hapa jisajiri tangaza biashara yako Bure
Video Jifunze haya mwanaume Hawezi kuchomoka
Sababu kubwa inayo sababisha mwanaume Kupunguza mapenzi kwako
Fursa ya kujiajiri kupitia blog
Tambua sababu zinazo sababisha wanawake wengi kuachwa na waume zao
Mapenzi pasua kichwa fahamu zaidi
0 Maoni