Ticker

6/recent/ticker-posts

MWANAMKE ASIYEPENDA NDUGU WA MUME DAWA HUWA NI KAMA HII

 

MWANAMKE ASIYEPENDA NDUGU WA MUME DAWA HUWA NI KAMA HII

Siku moja wakiwa wamekaa pamoja mume na mke wake mume akamwambia mke wake

 "Mke wangu nimewakumbuka sana ndugu zangu (kaka zangu dada  na hata baba na mama) kesho tujumuike pamoja na kula pamoja,,,,

Nitawaalika ili tujumuike nao ktk chakula cha mchana,itabidi uandae chakula kwa ajili yao."

Mke akasema kwa unyonge "Sawa mungu akipenda." 

Asubuhi ya siku iliyofuata mume akatoka kwenda ktk mishughuliko yake lkn baada ya masaa kadhaa akarejea nymbn na kumuuliza mke wake.

"Mke wng umeandaa chakula cha mchana kwa ajili ya wageni? maana baada ya lisaa limoja watakuwa wameshafika."

Mke akajibu "hapana sijapika kwani ndugu zako sio wageni hapa watakula chochote watakachokikuta."

Mumewe akamwambia Mungu akusamehe mke wangu kwa nini unayasema hayo ilihali tokea jana nilikuambia ya kuwa wazazi wangu wanakuja?

Na kwa nin hukuniambia mapema kuwa hutopika ilihali baada ya lisaa limoja wazazi wangu watakuwa hapa  "nini sasa unafanya mke wangu." 

Mke akamjibu "waache waaje nitawataka radhi kwani wao si wageni hapa watakula chochote watakachokikuta."

Basi mume ikambidi aondoke pale nymbn kwa kukwepa fedheha.

Baada ya dakika kadhaa mlango ukagongwa mke akaenda kuufungua.

Kwa mshangao mkubwa alipofungua mlango akakuta wageni waliokuja hapo ni wazazi wake babaake mamaake dada zake pmj na kaka zake. 

Akastuka kwa mshangao na kuwakaribisha ndani,

Baba akamuuliza kuwa mume wake yupo wapi?

Akajibu yule mwanamke kuwa alikuwepo hapa ametoka dakika chache kabla hamjafika.

Baba akamwambia "mumeo jana alitupa taarifa kuwa Leo anatuarika hapa tuje kula pmj chakula cha mchana sasa vipi yy ametoka si busara." 

Yule mwanamke akastuka kwa taarifa hiyo na kuanza kujifikicha mikono yake huku akiipiga piga hali ya kuchanganyikiwa."

Ikambidi aingie ndani na kumpigia simu mume wake akamwambia "kwa nn hukuniambia kuwa wazazi wng ndio wanaokuja?"

Mumewe akamjibu "Wazazi wng na wazazi wako wote ni kitu kimoja/hawana tofauti
Mke akamwambia " Lete chakula huku kilichokuwepo hakiwatoshi kwani ni kichache sana hakitawatosheleza"
Mume akamjibu " Mimi nipo mbali na hao sio wageni watakula chochote kilichopo kama wewe ulivyokuwa ukitaka kuwalisha wazazi wangu"

SOMO: Watendee watu kama vile unavyopenda kutendewa wewe.

Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();