Ticker

6/recent/ticker-posts

NAOMBA USHAURI WAKO TAFADHARI

 

Mimi ni Mama wa miaka 35, nimeolewa, nimeishi kwenye ndoa kwa miaka kumi bila kupata mtoto, nimekua nikienda hospitalini naambiwa kuwa sina tatizo, mume wangu yeye aligoma kwenda kupima kabisa na kusema yeye hana tatizo lolote. Alikua ni mtu wa wanawake, alikua akibadilisha wanawake kama nguo akitafuta mtoto, mama mkwe wangu alikua ni mtu wa kunitukana tukana kila siku, alikua akiniambia waziwazi kuwa nimuache mwanae atafute wanawake wenye vizazi.

SEMINA,Fahamu njia zitakazo kukwamua katika maisha ya dhiki na kuwa milionea

Nilivumilia mpaka mwaka jana, nilienda yumbani kwenye harusi, lengo lilikua ni mume wangu kunitunmia nauli lakini aligoma, nilipokuja kuchunguza nikakuta kuwa kumbe tayari anaishi na mwanamke mwingine. Ile kuondoka tu akapata upenyo wa kutafuta mwanamke mwingine akaishi naye. Nikiwa katika hali ya mawazo nilikutana na Kaka mmoja ambaye alikua X wangu, tukakumbushia na kwa bahati mbaya nilipata ujauzito, baaada ya kupata ile mimba nilipaniki, nilijua mume wangu hataitaka.

Kwakuhofia kuharibu ndoa yangu niliamua kuitoa, nilikunywa dawa lakini haikutoka, nilienda hospitalini kuitoa lakini daktari ambaye likua rafiki yangu aliniambia nikiitoa nakufa na naweza nisizae tena, niliogppa lakini nampenda mume wangu, sikutaka kuvuruga ndoa yangu na nilijua kuwa atajisikia vibaya kama akijua nina mimba si yake. Nilienda hospitali nyingine ambapo napo waligoma kuitoa, nililazimika kuibeba, nilimuambia mume wangu lakini aliikana. Alisema si yake nimtafutie mwanaume mwingine, alimuambia kila mtu kuwa mimi Malaya nimemsaliti na kubeba mimba ya mwanaume mwingine.

SEMINA,Fahamu njia zitakazo kukwamua katika maisha ya dhiki na kuwa milionea

Kuona vile nilijua kabisa ndoa imeisha, nilimuambia X wangu kuwa nina mimba yake, kumbe nayeye alikua akitafuta mtoto kwenye ndoa yake, akakubali kunihudumia. Nikitegemea kuwa mume wangu atanaicha kwakua kashanidhalilisha kwa ndugu zangu, marafiki na ndugu zake nilipojifungua alikuja na kumdai mtoto, alianza kuhudumia na anamtaka mtoto wake. Wakati huo huo X wangu ambaye ndiyo Baba wa mtoto anasema mtoto ni wake na hawezi kumuachia mume wangu. Kusema kweli nimechanganyikiwa sijui hata mtoto nimpe nani, X wangu au mume wangu?

Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();