Ticker

6/recent/ticker-posts

JINSI YA KUKABILIANA NA WATU WENYE KUKUKOSOA KWA LUGHA MBAYA

 


JINSI YA KUKABILIANA NA WATU WENYE KUKUKOSOA KWA LUGHA MBAYA

Kuna kitu huwatesa watu wengi sana duniani hasa kukosolewa na watu wengine kwa lugha mbaya 

Kama ukiweza kujifunza jinsi ya kukabiliana na watu wenye kukukosoa kwa lugha mbaya utakuwa huna mpinzani duniani

Wasomi wakubwa, wafanyakazi, wanasiasa, viongozi, wasanii, matajiri,watu wenye nguvu kubwa ya ushawishi hupata wakati mgumu sana kukabiliana na watu wenye kuwakosoa kwa lugha mbaya

Kwa sababu ya hasira wengi wakikosolewa huwa wanakuja juu na kujihami au kuwakosoa wenye mawazo tofauti ili kuonekana wapo sahihi

Hili ni kosa kujitetea kama kuna mtu anakukosoa au kutaja mapungufu yako hata kama anatumia lugha mbaya kiasi gani ukimjibu tu unakuwa umefeli kila kitu

Kwenye mapenzi watu wengi huteseka kwa sababu wakikosolewa tu badala ya kusikiliza malalamiko huanza kujihami na kujitetea sana ili kuficha makosa yao 

Kitendo cha kujihami huwa hakubadilishi imani ya mkosoaji wala hakileti mapatano kwa mpinzani

Lengo la mkosoaji ni kufikisha ujumbe tu na huwa mkosoaji anataka kuwa mshindi tu hata kama anatumia njia ambayo sio sahihi

Ili uweze kumshinda unatakiwa kumpa ushindi yaani "You win by loosing"

Kwa maana unapoteza mjadala kisha ugomvi unafika mwisho papohapo

Ila ukianza kumkosoa tu anakuja juu na kujihami na kukishambulia kwa tuhuma nyingi zaidi kisha mnaweza kupigana au kumwaga damu

Huenda upo na mwanamke mjeuri sana au mwanaume mjeuri sana bingwa wa kukuzushia tuhuma za usaliti,kukupa kesi,kukutukana matusi ya nguoni,kukusema vibaya mbele za watu,kukukosoa vibaya sana kwa kila jambo ambalo unafanya 

Njia ya kukabiliana na mtu huyo ni nyepesi lakini kwako itakuwa ngumu mwanzo lakini ukiweza kuifanya kuwa tabia atainua mikono juu mwenyewe

Kitu cha kwanza usitake kumshinda kwa sababu huwezi na ukijaribu ndio ugomvi unakuwa mkubwa sana 

Kingine usimkosoe kwa lolote hata kama upo kwenye haki kwa sababu huwa hawataki kusikia ukweli kuhusu tabia zao na vilevile huwa wakosoaji hawataki kukosolewa na vilevile huwa wanataka kuwa washindi tu 

Hivyo ukiwapa ushindi tu wanakuwa hawana nguvu ya kukupa hasira 

 Kwa mfano kuna mtu anadai wewe ni mbishi sana au anasema watu wa jamii fulani au mji fulani ni washamba sana hapa unaweza kupata hasira kama unatokea mji huo lakini kama ukikaa kimya unakuwa mshindi 

Kama kuna mtu anadai wewe ni mbishi kisha ukianza kumkosoa na kujitetea kuwa wewe sio mbishi hapo ndio unakuwa umethibitisha kuwa kweli wewe ni mbishi 

Kingine ukikosolewa huwa kuna ukweli ndani yake hata kama ni kidogo sana na lawama nyingi lakini kama ukituliza akili utaona sehemu ya kujirekebisha ila ukianza kumkosoa na kujitetea unabaki hivyohivyo na utazusha mjadala na ugomvi 

Soma mkasa huu ambao majina sio halisi  mwanamke jina lake Hannah mkewe Hassan.
Hasan alikuwa analalamika kuwa mkewe (Hannah) huwa hamsikilizi kabisa 
Hassan alisema "Huwa hunisikilizi "
Hannah hakujibu chochote alimpuuza mumewe.
Hannah aliona tuhuma zile sio za kweli na aliona hakuna sababu ya kujibu chochote

Pale Hannah alithibitisha kuwa huwa hamsikilizi mumewe kwa sababu kile mume amelalamikia ndio mkewe amefanya tena waziwazi

Wapo ukiwaambia ni wajeuri huonyesha ujeuri kweli hilo ni kosa kwa sababu inaonekana unafanya makusudi

Hata kama huoni kosa lako acha hasira na ujeuri wa kudai huna makosa 

Katika kila tuhuma kuna ukweli ndani yake kama ukiacha ujeuri utaona sehemu ya kujirekebisha

Tatizo watu wengi wakiambiwa ukweli kuhusu ubaya wa tabia zao hupata hasira kwa maana huwa wanataka kusikia mazuri yao tu 

Kwanza hakuna binadamu ambaye anakosolewa tu siku zote au kusifiwa tu siku zote 

Kila mmoja huwa anakosolewa baadhi ya nyakati na kusifiwa baadhi ya nyakati

Hata kama unaona upo kwenye njia sahihi bado kuna makosa huwa unafanya jambo la kwanza ni kukubali kuwa wewe sio mkamilifu hata kama huwa huoni makosa yako 

Kitendo cha kutokubali makosa yako ndio huwa kinafanya watu wenye kukukosoa kupata hasira na kuzidi kukutuhumu kila wakati na wewe kinafanya uzidi kuwa na hasira na kujitetea sana

Mtu akikukosoa hata kama ni adui yako usitazame uadui wala mfululizo wa matukio yenye ugomvi bali sikiliza kile anachokosoa kisha fanya marekebisho sio kujitetea

Unaweza kuwa mfanyakazi umefanya kazi nzuri sana na unaona unastahili pongezi na kusifiwa kutoka kwa boss wako 

Lakini ghafla unashangaa Boss wako hatoi shukurani wala pongezi zaidi anatoa dosari za kazi zako 

Kwa sababu ya kiburi na majivuno unaona mwajiri anaroho mbaya,hakupendi,anataka uharibikiwe,anataka kukutesa jambo ambalo sio sahihi

Kama kuna tuhuma au UNAKOSOLEWA kwenye kazi zako sikiliza kwanza acha kujitetea na kujiona malaika 

Hata kama unasifiwa kwa kutoa huduma nzuri kama ukisikia tuhuma mbaya sana sikiliza sio kujitetea

Mwenye kukukosoa hata kama ni adui kuna ukweli ndani yake hata kama unaona hujafanya makosa popote pale tulia hasira ziondoke angalia makosa yako utayaona tu 

Kuna watu wakikosolewa kwenye mitandao ya kijamii hujibu tuhuma kwa matusi au kumkosoa mwenye lengo la kukosoa tabia ya mtu husika

Ile tabia ya kuita watu "Haters" sio sahihi hata kama huoni unapokosea usijibu chochote mpaka akili iwe imetulia 

Kukosolewa husaidia kuboresha huduma bila wakosoaji huwezi kuboresha huduma wala kujua dosari zako 

Kama hujui dosari zako utakuwa bingwa wa kukosoa wengine muda wote na kuwaona wengine wabaya muda wote 

Mara ngapi watu ambao unawapenda wanakukosoa na unakubali tuhuma?

Hivyohivyo hata watu ambao unawacchukia wakikosoa hhat kama lugha sio nzuri ujue kuna kitu hakipo sawa 

Jinsi ya kukabiliana na mkosoaji kama akili ipo kwenye utulivu unaweza kumuuliza aeleze kwa undani kuhusu tuhuma hizo kisha atoe pendekezo la maboresho 

Kama ni mwanamke au anakutuhumu kwa tabia fulani kila wakati hata kama huoni makosa yako acha kiburi pembeni kisha uliza nini urekebishe kwa sauti ya chini

Hapa ni pagumu sana kwa sababu kuna ile tabia ya umimi ya kuona atakupanda kichwani lakini kama mwenzio ni mjeuri wewe ukiwa mpole ujeuri wake unaisha 

Dawa ya mtu mjeuri ni wewe kuwa tofauti nae kitabia 

Usiwe kama adui zako kuwa tofauti na wao wanaishiwa nguvu ya ushawishi dhidi yako

Mwisho wa makala  asante kwa kusoma mpaka mwisho wa story yetu karibu kwa maswali maoni na ushauri ikiwa una tangazo unahitaji tukutangazie Humu pia

*BADILI MAISHA*

*Ukitaka kufahamu njia ya kutengeneza Dora 100  mtandaoni kwa mtaji wa Sh:35,000 njoo inbox nikupe huo mchongo*Whatsapp 

kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇
Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();