Ticker

6/recent/ticker-posts

FAHAMU KINACHO HAMISHA THAMANI YA MPENZI ULIYE NAE 🙄


 Ukweli ni kwamba ULIYE NAE AMA ALIYEPO ndiye wa thamani kubwa kuliko anayeonekana kama mpya, mara nyingi ni namna mtu mpya alivyo jiweka ila kwa uhalisia MAVAZI YANAWEZA KUTENGENEZA UZURI WA MTU ila nguo hizo zikivuliwa huondosha kile wengi hukitazama, Nataka kusema kwamba;-

👉 DEREVA ULIYE MZOEA NI MZURI ZAIDI KULIKO DEREVA AMBAYE NI DEREVA ILA HAKUWAHI KUKUENDESHA. 

Kuzoea ni hatua kufikia IMANI na hapo hujengwa kitu kinaitwa KUAMINIWA💯 Kama hujaaminiwa huwezi kupendwa, mara nyingi watu hawajui kama MTAZAMO MPYA HUFUBAZA IMANI ULIYOIJENGA KWA MIAKA KADHAA na hata kusababisha hali ya utulivu wa FIKRA kutoweka na kuyumbisha maana halisi ya kuwa na uliyemzoea, ndo maana kwa sasa mtu kuharibu alichokijenga ni rahisi bila kujua yeye kuaminiwa huko aliko anzisha uhusiano ni ngumu kuiweka DHAMANA YA UPENDO mwisho kabisa wengi hutamani kurudi walipotoka baada ya kuona hakuna jipya zaidi ya MUONEKANO ambao Pengine ulikuwa wa namna mtu anavyojiweka😂😂

Mheshimu aliyekupa nafasi mkajenga DHAMANA YA UPENDO kuliko kuona madhaifu yake na kutaka kutafuta Mwingine, Kuna wakati MAJUTO huja na usipate ufumbuzi, Mapenzi mazuri na yenye radha ni yale unayatengeneza mwenyewe kwa Mtu uliyempa dhamana ya NAFSI pamoja na MOYO wako.
Mwisho wa makala  asante kwa kusoma mpaka mwisho wa somo letu karibu kwa maswali maoni na ushauri ikiwa una tangazo unahitaji tukutangazie Humu pia
kama bado huna App ya MAHABA tafadhali Download kuendelea kupata masomo yetu👇
Reactions

Chapisha Maoni

0 Maoni

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();